Kikao changu na makampuni ya simu kuhusu kesi ya kuibiwa vifurushi

Tuko pamoja mkuu mie ni miongoni mwa watu watakaotia sahihi kwenye hyo hati ya mshtaka.
 
Halafu vifurushi vimekuwa bei juu mpaka mtu mzima naingia JF kwa freebasics😭😭
 
Hawa jamaa ni wasanii, mimi nilikuwa nanunua kifurushi cha Pinduapindua cha 24hrs,cha 2000 kila siku, mwanzoni nikawa naongea Hadi Nachoka hakiishi muda tu ndio Unaisha.l didn't have a problem with that, Baadaye nikawa naweza kununua vifurushi hata 4 kwa siku nikawa sielewi ni nini. Siku moja nikanunua kifurushi nikakifuatilia mara kimeisha ikabidi niwapigie simu voda, majibu niliambiwa unit zinatumika mpaka kwenye Data, lakini mimi natumia office Wi-Fi kila Mara, nikazima data lakini bado ni yale yale. Kitu cha kukera kwenye unit wanakuonyesha convertion ya unit to minutes voda to voda na voda to other networks lakini convertion ya data haipo kabisa wakati kimatumizi ipo. I was so disappointed.
 
Na Mungu akuongoze, nami niko nyuma yako na niko tayari kusaini hiyo fomu. Tunahitaji watu kama nyinyi; maana watanzania tumezidi woga, tunachojua ni kunung'unika vyumbani!
 
Kuhusu kifurushi kuisha bila kutumika, kwa mara ya kwanza limenikumba juzi.

Nilinunua GB 2 za internet na wakati huo nilikuwa na MB 200. Nilinunua saa nne usiku na bahati mbaya sana simu yangu ilikuwa imejaa storage hvyo sikuweza kudownload chochote. Niliperuz jf kwa kutumia free basics na ilipofika saa tano nikazima data nikalala. Lahaula!! Saa tisa usiku nikaamka ili nifanye mambo fulani mtandaoni, kuwasha data tu, nikakutana na ujumbe wa kifurushi kuisha. Sikutilia maanani maana nilijua ni kile cha MB 200 labda japo nachenyewe haikuwa kawaida kwakuwa jf hata niperuz siku nzima simalizi MB 70. Nikajaribu kuwasha hotspot, pc ikawa inagoma😲😲

Kufupisha stori niliwapigia simu usiku ule wakaniambia nisubiri masaa 24 (toka tarehe 14/11/2019) hadi leo hii nikipiga napigwa kalenda. Natumia Vodacom
 
Hoja hii ITV wangeiweka kama kipima joto hope mitandao ya simu ingejua ukubwa wa tatizo hili kwa wateja wao..Naahidi kuiunga mkona hoja kwa kuweka sahihi ya mcharango na dole gumba.
 
Hivi majuzi nimeumia sana; nilikuwa na bando ya wiki kutoka tigo 10GB na mtandao ulikuwa mbovu karibu wiki nzima. nikawa nimebakiwa na 7GB mara nikapata ujumbe kwamba kifurushi changu kimekwisha muda wake. Nilitamani nimtafune mdudu tigo kwa hasira!
 
NIMESEMA AIRTEL N WEZI KUPITIIZA ACANENI NAO KABISAA NILIKUWA KWA MWAMPOSA TOKA MCHANA NKAZIMA DATA NAWASHA NAPOKEAA HUU UPUUZIIII HUU UNGESE LAZIMA UISHEEE
 
[emoji3][emoji16][emoji3][emoji16]degree 80 wanambwela sana
 
Wanatumia udhaifu wa kutoelewa maswala ya mtandao kutupa hapo hapo, kwenye maswala ya internet kuna automatic update inawala watu bando bila wao kujijua, na hz simu kubwa kuna mavitu yana run background yanayumia data....

Elimu inahitajika pia, japokuwa wanatumia udlhaifu huu kutupiga
 
Nyumba gari na ahadi tamu tamu toka kwa unaotarajia kuwashitaki ziko karibu nawe kaza hivyo hivyo. Kila mtu ashinde match zake naamini zikianza miminika zawadi na uzi ndio hatutousoma tena mrejesho wake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…