Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Wivuu mkaliAngekua kichwa hao wazungu wasingekubali kumuachia..ila mpaka wameruhusu aondoke basi hana jipya.
OkaySalim is undisputed aisee, Nimekuwa nikifatilia BBC Kwa muda mrefu Sasa achilia mbali kiu ya kupata taarifa ila uwepo wake pia ulikua unaongeza chachu ya kufurahia kipindi Kwa kiasi kikubwa. Pia Wazir Khamsin Yuko vizuri sana. Hawa Kaka zetu ni real professionals, Hongera kwake na namkaribisha Tanzania Kwa mara nyingine Tena.
Mtangazaji mahiri Salim Kikeke ambaye mwezi April 2023 alitangaza rasmi kuacha kazi kwenye Shirika la Utangazaji la BBC, ameamua kurejea nyumbani Nchini Tanzania baada ya kuishi Uingereza kwa miaka 20.
Kwenye mahojiano mafupi na Millard Ayo, Kikeke baada ya kuulizwa kama anarudi Tanzania kufanya kazi kwenye Media alisema "Waandishi wa Habari ni kama Wanajeshi, kamwe hatuwezi kuondoka kwenye media moja kwa moja kwahiyo nitakuwepo kwa njia moja ama nyingine kwenye media, nimeamua kurudi nyumbani kusaidia na ku-share uzoefu wangu niliopata Kimataifa"
Salim Kikeke ambaye ni mmoja wa Watangazaji mahiri kuwahi kutokea Tanzania alianza kazi ya Utangazaji mwaka 1998 kituo cha CTN kisha akajiunga na Radio Tanzania (kwa sasa TBC) kisha akaenda DTV, ITV na baadaye BBC mwaka 2003 alikokwenda kwa mkataba wa miezi mitatu lakini kutokana na ufanyaji kazi mzuri Mwajiri (BBC) akamuongezea mikataba mingine na kumtaka abakie nchini Uingereza.
View attachment 2693061