Kikokotoo kipya cha NSSF

Kikokotoo kipya cha NSSF

Mparee2

JF-Expert Member
Joined
Sep 2, 2012
Posts
3,092
Reaction score
5,386
Nilikuwa nasikiliza clip ya ya mwaka jana (Jul) ya Afisa mafao wa mkoa wa Mwanza (James Oigo)
akielezea ukokotoaji mpya wa mafao ya mstaafu na pension (33%).

Akatolea mfano kwa Mstaafu aliyekuwa na mshara wa shs milioni mbili (2000,000) kwa mwezi; Akasema ataishia kulipwa shs Milioni 30 (malipo ya mkupuo) na kuendelea kulipwa pension ya shs laki nne (415,000) kila mwezi? Mbona malipo ya mwezi ni kidogo sana?

Hivi kama mtu aliyekuwa na Mshahara wa shs milioni mbili na aliyechangia zaidi ya miaka 15 anaishia kupata (415,000), hawa wafanyakazi wa kawaida walio wengi wenye mishahara chini ya laki nane watapata nini?

Nimeanza kuelewa kwa nini watu wanataka walipwe hela zao zote wanapo staafu

Ukweli imenishangaza sana; Kwa hayo mamiradi yooote wanayomiliki/wanayo anzisha kwa hela za wanachama, kwa nini wasingeongeza malipo ya kila mwezi yafike angalau 50% ya mshahara?
 
Nilikuwa nasikiliza clip ya ya mwaka jana (Jul) ya Afisa mafao wa mkoa wa Mwanza (James Oigo)
akielezea ukokotoaji mya wa mafau ya mstaafu na pension (30%)
Akatolea mfano wa Mstaafu aliyekuwa na mshara wa shs milioni mbili (2000,000) kwa mwezi; Akasema ataishia kulipwa shs Milioni 30 (malipo ya mkupuo) na kuendelea kulipwa pension ya shs laki nne (415,000) kila mwezi? Mbona malipo ya mwezi ni kidogo sana?
Hivi kama mtu aliyekuwa na Mshahara wa shs milioni mbili na aliyechangia zaidi ya miaka 15 anaishia kupata (415,000), hawa wafanyakazi wa kawaida walio wengi wenye mishahara chini ya laki nane watapata nini?
Nimeanza kuelewa kwa nini watu wanataka walipwe hela zao zote
Ukweli imenishangaza sana; Kwa hayo mamiradi yooote wanayomiliki/wanayo anzisha kwa hela za wanachama, kwa nini wasingeongeza malipo ya kila mwezi yafike angalau 50% ya mshahara ?
Hahaaa!!umekosea hiyo ni 33% ndiyo unalipwa kwa mkupuo mmoja inayobakia 67% ndio wanakutunzia wanakuwa wanakulipa kidogo kidogo kila mwezi!!!wanajua huna mrefu utakufa!!ukisikia mtu anapata pensheni hiyo jua alikuwa boss!!
 
Back
Top Bottom