Kikokotoo kipya mafao ya wastaafu kutoka 25% hadi 33%

Hoana

Kuna mhimili unatakiwa ufutwe. Iwe taasisi yakutunga Sheria, kujadili na kifuatilia (kamati) speaker na wengine sijui wabunge wasiwepo. Kiundwe chombo huru. Ukizingatia Tanzania Ina Masuala common ktk jamii. Halmashauri na madiwani watatosha kuibua ishu huko kwenye mashina(kaya).

Kuwe na Chombo mbadala kiwe na wasomi wasifikie idadi ya 50 na sio bunge. Wawe wachache iwezekanavyo. Wawe Wasomi sio wahuni wahuni. Mchakato wa kuwapata madiwani uwe na maboresho na wawe huru pia. Parliamentary kimekuwa chombo flan hivi sikielewielewi kila mtu, maprof, madaktari wanakilimbilia Kupiga sarakasi, kupora pesa, kutunga vitu walivyo na selfnterest navyo. Wabunge sio wote lkn kundi kubwa linaenjoi maisha ya raia isivyotakiwa. Kwanza hawajali.

Kwa mfano pensheni wanayopewa ni baada ya kufanya nini Cha maana kuliko Dr aliyehudumu kuokoa maisha, mhandisi aliyesaidia ktk umri wake wa kazi kuijenga nchi. Mbunge amejenga nini. Na watakwenda kuongeza umri wa kustaafu wakijua hakuna mtumishi atakayefikia huko, kwa nini wanashindwa kusapoti kustaafu at 55? Ni ubinadamu huo?
Ni Kweli kabisa ndugu, Jimbo liwe mkoa Kwa size, wabunge wawe idadi sawa na mikoa iliyopo. Serikali 3 itahusika hapo.

Mbona pale U.K mbunge analipwa mshahara usozidi professionals, mbunge ni mwakilishi wa wananchi. Wenye Upendo na uzalendo ndo wanagombea maana hakuna manufaa ya kifedha makubwa pale.

Na Ukiwa kiongozi unakaguliwa Mali zako na biashara unakabidhi Ili usitafute maslah kupitia uongozi.
Nchi hii UMASKINI wa watu CHANZO ni UONGOZI mbovu wa CCM, Wala Si vita,corona au kingine chochote. Amen
 
HATIMAYE serikali imetangaza kikokotoo kipya cha mafao ya wastaafu, safari hii kukishuhudiwa kuwapo kwa usawa na uwiano kati ya watumishi wa umma na sekta binafsi.

Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira, Vijana na wenye Ulemavu, Prof. Jamal Katundu, akizungumza na waandishi wa habari, jijini Dodoma jana, wakati akitoa taarifa kuhusu kanuni mpya za kikokotoo cha mafao ya watumishi nchini. PICHA: IBRAHIM JOSEPH

Kutangazwa kwa kanuni hizo ni hitimisho la sintofahamu ya mafao hayo iliyodumu kwa takribani miaka nne tangu mwaka 2018 serikali ilipositisha utekelezaji wa kanuni mpya za mafao kwa wastaafu zilizotaka kiwango cha mkupuo kiwe asilimia 25.

Kutokana na kuwapo kwa malalamiko ya wadau dhidi ya kanuni hizo Rais wa wakati huo, Dk. John Magufuli alilazimika kuzisitisha mwaka huo ili kutoa muda kujadili na Mei 14 mwaka huu, Rais Samia Suluhu Hassan aliliridhia ombi la wadau wa hifadhi ya jamii kupandisha kiwango cha kikokotoo kutoka asilimia 25 hadi 33.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini hapa jana, mwenyekiti wa kamati elekezi ya kanuni hizo ambaye ni Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Prof. Jamal Katundu, alisema waziri wenye dhamana na masuala ya hifadhi ya jamii aliunda kamati hiyo ili kutekeleza maelekezo ya serikali ya kukubaliana kanuni itakayowianisha mafao kwa wafanyakazi wote.

Alisema kamati hiyo ilifanya kazi yake kwa kuzingatia mambo makubwa mawili ambayo ni kuhakikisha kanuni mpya inayopendekezwa inatoa mafao bora kwa wastaafu na pia mifuko inakuwa endelevu kwa manufaa ya wananchi wote.

“Kazi ya kamati ya kuandaa kanuni itakayotumika baada ya kipindi cha mpito imekamilika na kuridhiwa na wadau, kanuni mpya iliyoridhiwa itaanza kutumika rasmi Julai Mosi mwaka 2022,” alisema.

MAFAO YATAKAVYOKUWA

Prof. Katundu alisema kiwango cha mkupuo cha asilimia 33 ni kwa mifuko yote na kikokotoo limbikizi kitakuwa 1/580 kama ilivyokuwa kwa mfuko wa NSSF na ilivyokuwa mifuko ya PPF, GEPF na baadhi ya wanachama wa iliyokuwa PSPF na LAPF.

“Makadirio ya miaka ya kuishi baada ya kustaafu ni 12.5 kama ilivyo kwa mfuko wa NSSF na iliyokuwa mifuko ya PPF, GEPF na baadhi ya wanachama wa iliyokuwa PSPF na LAPF,” alisema.

Alisema mshahara wa kukokotolea mafao ya pensheni utakuwa wastani wa mishahara bora ya miaka mitatu ndani ya miaka 10 kabla kustaafu na umri wa kustaafu kwa lazima utaendelea kuwa miaka 60.

“Pia niwafahamishe kuwa pensheni za wastaafu watakaotumia kanuni hizi zitakuwa zikihuishwa mara kwa mara kwa kuzingatia mfumuko wa bei na uwezo wa mifuko hiyo ya pensheni,” alisema.

FAIDA ZA KANUNI MPYA

Katibu Mkuu huyo alisema kanuni hizo zitaongeza kiwango cha malipo ya mkupuo kutoka asilimia 25 iliyokataliwa mwaka 2018 hadi asilimia 33 kwa wanachama 1,364,050 sawa na asilimia 81 ya wanachama wote 1,690,187 wa mifuko ya pensheni.

Pia alisema inaongeza pensheni ya mwezi kutoka asilimia 50 ya sasa hadi asilimia 67 kwa waliokuwa wanachama wa PSPF na LAPF ambao ni asilimia 19 ya wanachama wote wa mifuko ya pensheni.

“Faida nyingine ni mifuko ya pensheni ya PSSSF na NSSF itaimarika na kuwa endelevu, pia kwa kuwa kanuni mpya inaimarisha mifuko na kuwa endelevu, mifuko itaweza kuongeza pensheni ya kila mwezi kwa kuzingatia tathmini zitakazofanyika kila baada ya miaka mitatu,” alisema.

Vilevile, alisema wanachama wote wanaochangia kwenye mifuko ya pensheni watatumia kanuni moja ya mafao na hivyo kuweka uwiano na usawa wa mafao baina ya wastaafu.

Katibu huyo alisema serikali imeweka utaratibu wa kutoa elimu kwa wanachama na umma kuhusu kanuni hizo ili kuhakikisha wote wanakuwa na uelewa sahihi na faida zake.

“Nitoe rai kwa wananchi kuendelea kuiamini serikali sikivu inayoongoza na nishukuru wadau wa utatu kwa kazi nzuri ya pamoja iliyofanyika kwa weledi na uzalendo,” alisema.

KAULI ZA WADAU

Rais wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi (TUCTA), Tumaini Nyamhokya, alisema upangaji wa kanuni hizo umekuwa shirikishi na zimeridhiwa na wadau na hakuna eneo walilofichwa.

Alisema pamoja na hayo walikubaliana wasiende chini ya asilimia 35 lakini serikali na wataalamu kutoka nje walishauri kufikia asilimia 33 ili wafanyakazi wasiongeze michango ya kuchangia na mifuko iendelee kuwa endelevu.

“Tulikuwa tunapata asilimia 50 ya mkupuo halafu asilimia 50 nyingine tulikuwa tunapata malipo ya kila mwezi, lakini sasa imebadilishwa asilimia 33 ya mkupuo halafu asilimia 67 tutaipata kwa mwezi, hakuna namna inabidi tulipokee, wafanyakazi zoezi hili limekuwa shirikishi, sekta binafsi tumechukua TUICO wameshiriki ndani,” alisema.

Alisema watumishi wanaochangia mifuko ya NSSF, PPF, GEPF, mkupuo wao umepanda kutoka asilimia 25 na kufikia asilimia 33.

“Kwa wao ni furaha kubwa sana sisi tulikuwa tunapata asilimia 50 tumeshuka na sasa itakuwa asilimia 33, niwasihi tulipokee hili wafanyakazi kwetu sisi ni gumu kumeza lakini ni kwa mustakabali wa uendelevu kwa vizazi vinavyokuja, tusimame pamoja kwenye hili,” alisema.

Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Waajiri Nchini (ATE), Suzanne Ndomba, alisema waajiri, wafanyakazi na serikali walikaa wote kwa pamoja kutengeneza kanuni hizo ambazo zimezingatia utaalamu na wataalamu walikuwa wa pande wote.

“Niwasihi wafanyakazi na waajiri, serikali itaendelea kutoa elimu na wale waajiri wenye maswali waje ATE tutasaidia kuchukua na kupeleka serikalini ili kupata ufumbuzi,”alisema.

Kaimu Rais wa Chama cha Walimu (CWT), Dinnah Mathamani, alisema jambo hilo limefanyiwa kazi kwa muda mrefu na wameshirikishana.

“Kwa upande wetu ambao kikokotoo kilikuwa asilimia 50 na kushushwa kuwa asilimia 33 nadhani tutapata mshtuko lakini hali ndivyo ilivyo kwa kuwa tumeelezwa kwanini tumefikia hapa, faida zake bila kujali waliokuwa asilimia 50, au asilimia 25 lakini kubwa ni mifuko kuwa endelevu,” alisema.

Aliwaomba walimu wawe na utulivu, watapewa elimu na kueleweshwa, akisema: “Tukipata elimu kwa ujumla hakutakuwa na shida, sisi tumeshirikishwa kwenye kamati elekezi na tumepitishwa na wataalamu, sisi walimu tumelipokea na tutaendelea kutoa elimu kwa ambao hawajaelewa."
Mimi kama mfanyakazi sija participate kwenye hizo discussion zenu. Na ATE hawaja tuhusisha. Acheni kutudanganya na hizo rubber stam unions. Ni staafu at 60, nife at 65, ina maana hela mle nyie?
 
Hoana

Kuna mhimili unatakiwa ufutwe. Iwe taasisi yakutunga Sheria, kujadili na kifuatilia (kamati) speaker na wengine sijui wabunge wasiwepo. Kiundwe chombo huru. Ukizingatia Tanzania Ina Masuala common ktk jamii. Halmashauri na madiwani watatosha kuibua ishu huko kwenye mashina(kaya).

Kuwe na Chombo mbadala kiwe na wasomi wasifikie idadi ya 50 na sio bunge. Wawe wachache iwezekanavyo. Wawe Wasomi sio wahuni wahuni. Mchakato wa kuwapata madiwani uwe na maboresho na wawe huru pia. Parliamentary kimekuwa chombo flan hivi sikielewielewi kila mtu, maprof, madaktari wanakilimbilia Kupiga sarakasi, kupora pesa, kutunga vitu walivyo na selfnterest navyo. Wabunge sio wote lkn kundi kubwa linaenjoi maisha ya raia isivyotakiwa. Kwanza hawajali.

Kwa mfano pensheni wanayopewa ni baada ya kufanya nini Cha maana kuliko Dr aliyehudumu kuokoa maisha, mhandisi aliyesaidia ktk umri wake wa kazi kuijenga nchi. Mbunge amejenga nini. Na watakwenda kuongeza umri wa kustaafu wakijua hakuna mtumishi atakayefikia huko, kwa nini wanashindwa kusapoti kustaafu at 55? Ni ubinadamu huo?
Wanaudhi sana hawa.
 
Wameshapitisha ni Sheria. Kasaini Ndalichako. Wanataka kuua Wastaafu wa July 2022 ambao hawakuwaandaa kwa hicho kikokotooo. Magufuli arise uone Wanavyopindua uliyoacha.
 
huyo ndio kabisa hata usimuongelee kabisa
 
Sisi ambao hatuna ajira tunazidi kuchanganywa tu

20220412_232713.jpg
 
Hoana

Kuna mhimili unatakiwa ufutwe. Iwe taasisi yakutunga Sheria, kujadili na kifuatilia (kamati) speaker na wengine sijui wabunge wasiwepo. Kiundwe chombo huru. Ukizingatia Tanzania Ina Masuala common ktk jamii. Halmashauri na madiwani watatosha kuibua ishu huko kwenye mashina(kaya).

Kuwe na Chombo mbadala kiwe na wasomi wasifikie idadi ya 50 na sio bunge. Wawe wachache iwezekanavyo. Wawe Wasomi sio wahuni wahuni. Mchakato wa kuwapata madiwani uwe na maboresho na wawe huru pia. Parliamentary kimekuwa chombo flan hivi sikielewielewi kila mtu, maprof, madaktari wanakilimbilia Kupiga sarakasi, kupora pesa, kutunga vitu walivyo na selfnterest navyo. Wabunge sio wote lkn kundi kubwa linaenjoi maisha ya raia isivyotakiwa. Kwanza hawajali.

Kwa mfano pensheni wanayopewa ni baada ya kufanya nini Cha maana kuliko Dr aliyehudumu kuokoa maisha, mhandisi aliyesaidia ktk umri wake wa kazi kuijenga nchi. Mbunge amejenga nini. Na watakwenda kuongeza umri wa kustaafu wakijua hakuna mtumishi atakayefikia huko, kwa nini wanashindwa kusapoti kustaafu at 55? Ni ubinadamu huo?
Una hoja ya msingi sn
 
Wafanyakazi jitahidini mjenge mgali kazini,hiyo 33% ya mkupuo haitoki yote kwa mkupuo ni kusotea.

Ukifa hiyo 67% ya kila mwezi inakuwaje? Wanapewa wategemezi au ndiyo imetoka kama wapo above 18?

Je sababu za kukataliwa 2018 zimeisha au hata hazikuwepo?
 
HATIMAYE serikali imetangaza kikokotoo kipya cha mafao ya wastaafu, safari hii kukishuhudiwa kuwapo kwa usawa na uwiano kati ya watumishi wa umma na sekta binafsi.

Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira, Vijana na wenye Ulemavu, Prof. Jamal Katundu, akizungumza na waandishi wa habari, jijini Dodoma jana, wakati akitoa taarifa kuhusu kanuni mpya za kikokotoo cha mafao ya watumishi nchini. PICHA: IBRAHIM JOSEPH

Kutangazwa kwa kanuni hizo ni hitimisho la sintofahamu ya mafao hayo iliyodumu kwa takribani miaka nne tangu mwaka 2018 serikali ilipositisha utekelezaji wa kanuni mpya za mafao kwa wastaafu zilizotaka kiwango cha mkupuo kiwe asilimia 25.

Kutokana na kuwapo kwa malalamiko ya wadau dhidi ya kanuni hizo Rais wa wakati huo, Dk. John Magufuli alilazimika kuzisitisha mwaka huo ili kutoa muda kujadili na Mei 14 mwaka huu, Rais Samia Suluhu Hassan aliliridhia ombi la wadau wa hifadhi ya jamii kupandisha kiwango cha kikokotoo kutoka asilimia 25 hadi 33.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini hapa jana, mwenyekiti wa kamati elekezi ya kanuni hizo ambaye ni Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Prof. Jamal Katundu, alisema waziri wenye dhamana na masuala ya hifadhi ya jamii aliunda kamati hiyo ili kutekeleza maelekezo ya serikali ya kukubaliana kanuni itakayowianisha mafao kwa wafanyakazi wote.

Alisema kamati hiyo ilifanya kazi yake kwa kuzingatia mambo makubwa mawili ambayo ni kuhakikisha kanuni mpya inayopendekezwa inatoa mafao bora kwa wastaafu na pia mifuko inakuwa endelevu kwa manufaa ya wananchi wote.

“Kazi ya kamati ya kuandaa kanuni itakayotumika baada ya kipindi cha mpito imekamilika na kuridhiwa na wadau, kanuni mpya iliyoridhiwa itaanza kutumika rasmi Julai Mosi mwaka 2022,” alisema.

MAFAO YATAKAVYOKUWA

Prof. Katundu alisema kiwango cha mkupuo cha asilimia 33 ni kwa mifuko yote na kikokotoo limbikizi kitakuwa 1/580 kama ilivyokuwa kwa mfuko wa NSSF na ilivyokuwa mifuko ya PPF, GEPF na baadhi ya wanachama wa iliyokuwa PSPF na LAPF.

“Makadirio ya miaka ya kuishi baada ya kustaafu ni 12.5 kama ilivyo kwa mfuko wa NSSF na iliyokuwa mifuko ya PPF, GEPF na baadhi ya wanachama wa iliyokuwa PSPF na LAPF,” alisema.

Alisema mshahara wa kukokotolea mafao ya pensheni utakuwa wastani wa mishahara bora ya miaka mitatu ndani ya miaka 10 kabla kustaafu na umri wa kustaafu kwa lazima utaendelea kuwa miaka 60.

“Pia niwafahamishe kuwa pensheni za wastaafu watakaotumia kanuni hizi zitakuwa zikihuishwa mara kwa mara kwa kuzingatia mfumuko wa bei na uwezo wa mifuko hiyo ya pensheni,” alisema.

FAIDA ZA KANUNI MPYA

Katibu Mkuu huyo alisema kanuni hizo zitaongeza kiwango cha malipo ya mkupuo kutoka asilimia 25 iliyokataliwa mwaka 2018 hadi asilimia 33 kwa wanachama 1,364,050 sawa na asilimia 81 ya wanachama wote 1,690,187 wa mifuko ya pensheni.

Pia alisema inaongeza pensheni ya mwezi kutoka asilimia 50 ya sasa hadi asilimia 67 kwa waliokuwa wanachama wa PSPF na LAPF ambao ni asilimia 19 ya wanachama wote wa mifuko ya pensheni.

“Faida nyingine ni mifuko ya pensheni ya PSSSF na NSSF itaimarika na kuwa endelevu, pia kwa kuwa kanuni mpya inaimarisha mifuko na kuwa endelevu, mifuko itaweza kuongeza pensheni ya kila mwezi kwa kuzingatia tathmini zitakazofanyika kila baada ya miaka mitatu,” alisema.

Vilevile, alisema wanachama wote wanaochangia kwenye mifuko ya pensheni watatumia kanuni moja ya mafao na hivyo kuweka uwiano na usawa wa mafao baina ya wastaafu.

Katibu huyo alisema serikali imeweka utaratibu wa kutoa elimu kwa wanachama na umma kuhusu kanuni hizo ili kuhakikisha wote wanakuwa na uelewa sahihi na faida zake.

“Nitoe rai kwa wananchi kuendelea kuiamini serikali sikivu inayoongoza na nishukuru wadau wa utatu kwa kazi nzuri ya pamoja iliyofanyika kwa weledi na uzalendo,” alisema.

KAULI ZA WADAU

Rais wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi (TUCTA), Tumaini Nyamhokya, alisema upangaji wa kanuni hizo umekuwa shirikishi na zimeridhiwa na wadau na hakuna eneo walilofichwa.

Alisema pamoja na hayo walikubaliana wasiende chini ya asilimia 35 lakini serikali na wataalamu kutoka nje walishauri kufikia asilimia 33 ili wafanyakazi wasiongeze michango ya kuchangia na mifuko iendelee kuwa endelevu.

“Tulikuwa tunapata asilimia 50 ya mkupuo halafu asilimia 50 nyingine tulikuwa tunapata malipo ya kila mwezi, lakini sasa imebadilishwa asilimia 33 ya mkupuo halafu asilimia 67 tutaipata kwa mwezi, hakuna namna inabidi tulipokee, wafanyakazi zoezi hili limekuwa shirikishi, sekta binafsi tumechukua TUICO wameshiriki ndani,” alisema.

Alisema watumishi wanaochangia mifuko ya NSSF, PPF, GEPF, mkupuo wao umepanda kutoka asilimia 25 na kufikia asilimia 33.

“Kwa wao ni furaha kubwa sana sisi tulikuwa tunapata asilimia 50 tumeshuka na sasa itakuwa asilimia 33, niwasihi tulipokee hili wafanyakazi kwetu sisi ni gumu kumeza lakini ni kwa mustakabali wa uendelevu kwa vizazi vinavyokuja, tusimame pamoja kwenye hili,” alisema.

Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Waajiri Nchini (ATE), Suzanne Ndomba, alisema waajiri, wafanyakazi na serikali walikaa wote kwa pamoja kutengeneza kanuni hizo ambazo zimezingatia utaalamu na wataalamu walikuwa wa pande wote.

“Niwasihi wafanyakazi na waajiri, serikali itaendelea kutoa elimu na wale waajiri wenye maswali waje ATE tutasaidia kuchukua na kupeleka serikalini ili kupata ufumbuzi,”alisema.

Kaimu Rais wa Chama cha Walimu (CWT), Dinnah Mathamani, alisema jambo hilo limefanyiwa kazi kwa muda mrefu na wameshirikishana.

“Kwa upande wetu ambao kikokotoo kilikuwa asilimia 50 na kushushwa kuwa asilimia 33 nadhani tutapata mshtuko lakini hali ndivyo ilivyo kwa kuwa tumeelezwa kwanini tumefikia hapa, faida zake bila kujali waliokuwa asilimia 50, au asilimia 25 lakini kubwa ni mifuko kuwa endelevu,” alisema.

Aliwaomba walimu wawe na utulivu, watapewa elimu na kueleweshwa, akisema: “Tukipata elimu kwa ujumla hakutakuwa na shida, sisi tumeshirikishwa kwenye kamati elekezi na tumepitishwa na wataalamu, sisi walimu tumelipokea na tutaendelea kutoa elimu kwa ambao hawajaelewa."
Eti kuimarisha mifuko!!
Kwani aliyeidhoofisha ni nani?

Kama hii serikali inatumia fedha hizi za watumishi kujengea miradi yake ikijigamba inatumia fedha za ndani,

Kwa kweli, Siamini kama wizi wa mali ya umma utaisha tz maana serikali yenyewe ndiyo ndiyo inaanza kuiba mali ya watumishi.

Binafsi ninaanza kuwaelewa watumishi wezi wa mali ya umma thats life assurence baada ya kustafu
 
Mibunge ya CCM iliyotunisha matumbo kama vyura kule bungeni na mimacho yao mkiubwa kama ya bundi ndiyo iliyosababisha U.SENGE huu usiovumilika kwa watumishi wa umma.
 
Mibunge ya CCM iliyotunisha matumbo kama vyura kule bungeni na mimacho yao mkiubwa kama ya bundi ndiyo iliyosababisha U.SENGE huu usiovumilika kwa watumishi wa umma.
 
Wafanyakazi jitahidini mjenge mgali kazini,hiyo 33% ya mkupuo haitoki yote kwa mkupuo ni kusotea.

Ukifa hiyo 67% ya kila mwezi inakuwaje? Wanapewa wategemezi au ndiyo imetoka kama wapo above 18?

Je sababu za kukataliwa 2018 zimeisha au hata hazikuwepo?
Mkuu bado na hiyo 33% hawapewi kwa mkupuo...!?
 
Ndiyo, ila ni matokeo ya Mwajiri kutowasilisha michango kikamilifu kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii.

Na wastaafu wote wanachama wa PSSSF wanapitia kadhia hii.
 
Back
Top Bottom