Kikomo cha amkio la shikamoo

Kikomo cha amkio la shikamoo

mimi binafsi siipendi kabisa salamu hii. Licha ya kuhusisha udhalilishaji (ubwana na utwana) pia haitoi jibu sahihi kwa hali ya mtu. Mwamkiaji akisema "shikamoo", mwamkiwa hujibu "marahaba". Hata kama anaumwa au ana tatizo lolote la hali au mali, bado atajibu "marahaba". Mwamkiaji hawezi kutoa msaada wowote kwa kuwa salamu aliyoitoa haijampa nafasi ya kupata jibu lenye taarifa kamili kuhusu afya au hali ya mwamkiwa. Vinginevyo utumie muda wa ziada kumhoji mtu kama anakuhusu. Tunaambiwa "wakati ni mali". Tuko busy kufukuzia shilingi.

Nangojea tume ya katiba ikija mtaani kwangu, nitaomba hili liwekwe kwenye katiba mpya. Shimamoo marufuku.
Msinicheke, hapo ndo ukomo wangu wa kufikiri. Lol!

labda kwa kuanzia tujue sababu za msingi/ hoja ya msingi ya binadamu kupeana salamu wakutanapo ndio tutajua kama shikamoo mali au la?
 
Kwa sisi wachaga shikamoo anapewa mwenye pesa zaidi.


hahahaha hivi ni kweli???????? kuna jamaa alikuwa anatuambia kuna mzee wa kichaga alikuwa anamsalimia mtoto wake eti 'SHIKAMOO MTOTO WANGU' Kisa mtoto ana hela kumzidi mzee!!! me nilifikiri jamaa alikuwa anatudanganya hasa alivyokuwa anaigiza rafudhi ya kichaga!
 
Back
Top Bottom