Kikomo cha principle subjects kwa form 6 necta exams.

Joined
Jan 2, 2013
Posts
31
Reaction score
5
Heshima kwenu wadau.
naulizia ukomo wa principle subjects ambazo mtu anaweza fanya kwa form six necta exams.
nilimaliza form 6 2004, nilifanya mchepuo wa CBG na kufaulu vyema kuendelea university na sasa nimeajiriwa. ila kutokana na mapenzi yangu nataka kusoma kitu roho inapenda, ila natakiwa niwe nimefanya a level physics ili nijoin hiyo kozi.
hivyo nataka kuja sit kwa physics necta form six. nauliza wadau kama necta wanaruhusu.nakumbuka kuna wale wanaofanya Principle subjects 3 na bible or islamic knowledge.
NB: Masomo niliyofanya form six ni CBG plus general studies,
 
ni muhimu sana kwangu, mjuzi wa taratibu naomba achukue muda wake kidogo kunielmisha. ntashukuru sana
 
Unataka kurudi mtihani 1 wa physics au ulikuwa unataka kujua nn?
 
Hivi inawezekana mtu aliyesoma CBG akapata chance ya kusoma Medical?
 
Unataka kurudi mtihani 1 wa physics au ulikuwa unataka kujua nn?


siyo kuresit ndugu, sikufanya physics A level. nilisoma mchepuo wa CBG i.e chemistry,biology na geography. pia nilifanya GS kama sheria kwa wote. nataka nifanye A level physics necta exam. ndiyo nauliza kama naruhusiwa na taratibu za necta. asante
 
siyo kuresit ndugu, sikufanya physics A level. nilisoma mchepuo wa CBG i.e chemistry,biology na geography. pia nilifanya GS kama sheria kwa wote. nataka nifanye A level physics necta exam. ndiyo nauliza kama naruhusiwa na taratibu za necta. asante


Nimekuelewa vyema unaruhusiwa kwani vigezo vya kufanya mtihani wa kidato cha 6 sharti uwe na credit 3 O level au uwe umemaliza kidato cha 6 hapo nyuma na sikuhizi application zinafanyika online unapata jibu papo hapo km unavigezo au hapana.
 
Am sorry, but being a graduate you would surely know that you need not sit for a form six exam again? Unauliza kweli au unachangamsha kijiwe tu?
 
Hongera sana ni watu wachache sana wanaweza kuwa na uwamuzi huo, tafadhali usikate tamaa ni VEMA KABISA KUSOMA KILE UPENDACHO HATA KWA GHALAMA ZAIDI, Pili km jamaa mmoja alivyogusia tayari km wewe ni graduate ulizia University zetu kama unaweza kusoma Physics pekee University level au utueleze LENGO LAKO KAMILI ILI WAKUSHAURI VEMA
 
Unajua kurisiti mtihani ni tofauti na kusoma kabisa? Necta wana kigezo cha credit hours, kwamba lazma usome kiasi fulani kabla ya kuendelea na mtihani kama ni fresher.
Maisha marahisi mamii. Ingia google necta. Chukua hotline watangie uwaulize. Na mie nina ndoto ya urubani since i was a kid, nangojea nikinunua kandege kangu nianze kujibabu sambeke.
 
physics tena?? we jamaa kwel hujipendi


mbona umeanza kunitisha mapema? kuhusu uwezo ondoa shaka namshukuru Mungu alinipa IQ kubwa (though siyo superior IQ). nahakika ntafaulu tu. nshaanza kusoma mechanics,nafurahia kurusha ndege na kusafiri hadi mwezini nikiwa mezani home kwangu. taratibu zikiruhusu nafanya, ila nilijaribu pitia practicals zake naona kautata kidogo. ila yote yanawezekana.
 
Am sorry, but being a graduate you would surely know that you need not sit for a form six exam again? Unauliza kweli au unachangamsha kijiwe tu?


asante, ndugu sisi watu wa mikoani wengi wetu tukiwa sec tunakuwa na exposure ndogo sana,ndo maana wengi tukifika university tunajutia maamuzi yetu. wapo wengi sana, nakumbuka nilishawahi tembelea rafiki zangu wakati wanasoma chuo kikuu kishiriki cha muhimbili wengi walikuwa wanajuta walikosea njia kwenda pale. nadhani mentoring ni poor kwa sisi wengi wa up countries.
nipo serious,lazima nikasome na kufanya kazi nayopenda toka mtoto. muda nimepoteza, ila kipesa sitalost sana najipanga.
 


asante kwa info. vigezo ninavyo. nilifanya masomo kumi O level, nilipata A na B kwa yote. A level nilipata C flat kwa CBG na pass ya GS.
ni habari nzuri kama necta wanaruhusu
 


asante kwa mawazo yanayojenga. ntawapigia simu.
mh king`asti ule ucheshi wako wa MMU kumbe unatumika hadi huku elimu forum? teh teh! vp Mr. nice alikuimba wewe nn kwenye wimbo wake wa king`asti?
 


thanks alot for your constructive ideas, nishaulizia kozi nayataka fanya, moja ya kigezo cha kujiunga lazima uwe umefanya A level physics,na hakuna jinsi unaweza join ndo ukaisoma pale. hivyo natakiwa nifaulu kwanza kabla sijajoin.
Nishakata shauri tayari, inachangamoto zake, nakabiliana nazo, nataka baada ya miaka 2-3 nijoin kusoma kitu roho inapenda. real sifurahii kazi ninayofanya kwa sasa japokuwa inanilipa kiac tosha.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…