Kikosi cha Rapid Force (UVCCM) kivunjwe

Hismastersvoice

JF-Expert Member
Joined
Jan 26, 2013
Posts
21,741
Reaction score
26,735
Umoja wa Vijana CCM umejigeuza kuwa kikosi cha wapiganaji kuilinda CCM, kikosi hiki kimefanya mafunzo ya uaskari na baadhi yao tunawaona wakiwa kwenye sare za kiaskari wakilinda mikutano na viongozi wajuu wa nchi!

Kitendo hiki hakikubaliki kwani ni tishio kwa amani ya nchi maana hawa vijana wanajiamini pia wanaamini hawawezi kichukuliwa hatua na serikali na hawajaanza leo kujiamini huko.
 
Alooooooooo.
kwani red brigade waliishiaga wapi maana wangekuwepo vita ingeanza kati ya green guards vs red brigades.
 
Sheria hairuhusu lakini ndio vile tena. Sheria yetu sio msumeno, inamakali upande mmoja.
 
Tatizo la vikosi hivi ni pale CCM ikishindwa kwenye uchaguzi wowote havitakubali, kama alivyowahi kusema mama kuwa chawa wake hawatakubali akisemwa.
 
Mapigano yanayoendelea Sudani yanatokana na kikosi kama hiki cha CCM, tukumbuke huko Malawi Banda alikuwa na kikosi kama hiki ambacho kilijitutumua na kuwa tishio kwa jeshi na nchi, bahati nzuri siasa za Malawi ni nzuri hivyo jeshi likakisambaratisha na Malawi ikawa huru!
 
Kuna watu wamekipaisha nakiita wagner acheni uongo Hakina madhara ni panya rod tu wale kazi yao kurusha mawe kama vibaka wengine.
 
Kwa wale waliofuatilia vitisho vilivyokuwa vikitolewa huko kanda ya ziwa dhidi ya viongozi wa Chadema watagundua kuwa Uvccm wanamaanisha utayari wao kama jeshi.
Your browser is not able to display this video.
 
UONGO
UONGO
UONGO...

UVCCM ni wakakamavu tu na si askari....

#SiempreJMT[emoji120]
 
iLA wajue kuwa upinzani wakiunda chao wasilalamike!
Sidhani kama hawa vijana nyoronyoro wa ccm kama wanaweza hata kupambana na vijana wakakamavu wa kike upinzani!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…