Kikosi cha Simba Kifumuliwe

Patroman

JF-Expert Member
Joined
Nov 12, 2018
Posts
809
Reaction score
1,222
Kwanza kabisa niwapongeze wachezaji, bechi la ufundi na uongozi kwa ujumla wake. Robo fainali ni hatua kubwa sana.

Kwa mimi naona bora tumetolewa kwani hata kama tungeshinda mbeleni tungepata aibu kubwa zaidi.Uwezo wa wachezaji wetu wengi ni mdogo sana kwa levo ya kimataifa. Hawana uwezo wa kukaa na mpira,jawana kasi, hawawezi kukaba pia hawana nguvu kuanzia beki line, viungo mpaka washambuliaji.

Kwa mimi anaestaili kubaki kikosi cha kwanza ni Aishi Manula, Erasto, Niyonzima, Chama, Kagere na Kapombe. Wengine warudishwe kikosi cha pili na baadhi waachwe kabisa.

Mechi ya Jana viungo vilikufa kabisa MTU kama Mkude hakutakiwa kumaliza mechi.
 
mnahela?

[emoji375][emoji375]
 
Kuna mambo nakubaliana na wewe ila kwa wachezaji umeweka wachache mno. Kwa maoni yangu Niyonzima hapaswi kuwa kikosi cha kwanza badala yake aanze Chama, pia Beki 3 yuko vizuri anahtaji marekebisho tu. Bocco bado ni mchezaji muhimu na anastahili kuwemo. Mchezaji MAALUM ninayetaka kumsema Leo ni huyu anayekula mpunga mrefu kwa kazi nyepesi anayofanya, Coulibaly!! Huyu hata mechi za ndani achezeshwe na Alliance, Lipuli, African Lyon na WanaKino.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa kweli coulybal hatufai..ukizingatia ni wakimataifa.. Ni mzuri kama timu inashambulia..lakini mkishambuliwa ni mzigo..Nina uhakika Kapombe angekuwa fiti ..coulbaly asingegusa nyasi za uwanja.
 
Kuna Mwamba wa Lusaka,Kagere,Okwi,Bocco,Niyonzima mliwapa misifa mingiiii leo hii mnataka kikosi kifumuliwe na kile kipana vp

Sent from Nokia 7 Plus
 
Ndio maisha ya mpira yalivyo ..nikusajiri na kuacha pale unapoona malengo hayajatimia..sio simba tu hata huko kwa wenzetu walio tutangulia kimpira.
 
Huyu niyonzima pamoja na kwamba ndiyr aliyoasist bao pekee la simba lakini mipira mingi amenyanganywa yeye na mwisho wa siku ikaleta maafa. Yeye amekariri kuwa anacheza na akina mbao na lipuli kila akipata mpira anataka kupiga chenga zake za kizamani za kurudi nyuma, yale majamaa yalishamjulia yanajichukulia mpira kiulaini mguuni mwake.
 
Kwa mfano kotei na mkude ni viungo lakini hawana uwezo wa kukaa na mpira na kupandisha timu.. Kotei akikaba na kumiliki kinachofuata ni kuanua mbele..pia mkude.
 
Kuna Mwamba wa Lusaka,Kagere,Okwi,Bocco,Niyonzima mliwapa misifa mingiiii leo hii mnataka kikosi kifumuliwe na kile kipana vp

Sent from Nokia 7 Plus
Wewe bakuli fc mambo ya simba yanakuwasha nini...mukiona thread ya mume wenu simba lazima muishobokee
 
Reactions: Tui
Hela si tumepata kutoka CAF..baada ya kufuzu makundi na robo fainali.. Alafu pia Simba ni kampuni.
Humjui vizuri muwekezaji mfanyabiashara Mo Dewji...jitingishe kusema Simba mmepata hela toka CAF na pia ni Kampuni.

Ndio utajua Dewji ni mtu was Singida au India...

Pokes [emoji460][emoji460][emoji460][emoji460] zawadi toka Lubumbashi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nakubaliana na ww kutokukubaliana, naomba nisaidie kitu ili utoe solution ya tatizo baada ya hao unaotaka waachwe je ni mchezaji gani wa ndani au nje ya mipaka yetu ungependa asajiliwe??
Japo mm naomba wafuatao waachwe kabisa Gyan, kwasi, mo Ibrahim, Ndemla, mzamiru, Salamba, Okwi ,Wawa.
Halafu atafutwe mbadala wa mkude, mbadadala wa okwi,

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wakigeni wa kuachwa.. Juko murshidi..Giani..coulrybali..kwasi..kotei..okwi . wa ndani salamba..mohamedi Ibrahim..ndemla..bukaba,, mlipili..ally saleh...na yule alieingia Jana mwenye mbio nyingi
 
Wakigeni wa kuachwa.. Juko murshidi..Giani..coulrybali..kwasi..kotei..okwi . wa ndani salamba..mohamedi Ibrahim..ndemla..bukaba,, mlipili..ally saleh...na yule alieingia Jana mwenye mbio nyingi
Mwenye mbio nani Rashid Juma?? Km ni huyo abaki ksb bado mdogo na kwa baadaye atakuja kuwa mzuri ksb hana uzoefu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wewe bakuli fc mambo ya simba yanakuwasha nini...mukiona thread ya mume wenu simba lazima muishobokee
Bakuli n chombo chenye heshima sana hapa Duniani,maana ina kaz nyingi sana mkuu.

Sent from Nokia 7 Plus
 
Kwa Manula umekosea sana, huyu ni kipa mbovu sana na stars walimtumia afcon tutafungwa sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…