Mnashangaza sana,
Simba inahitaji muda kidogo na uwekezaji makini kuanzia kwenye usajili na benchi la ufundi.
Mtoa mada, nafikiri mihemko na hasira zakufungwa akazihamishia kwa wachezaji directly.
Simba ina wachezaji wazuri, wasio na uzoefu na mashindano ya kimataifa
Kwa sasa tunahitaji top level players walau 6 kikosini kwa ajili ya kuleta ushindani mkubwa kikosini.
Determination ya wachezaji wetu Ni muhimu sana, lazima wafahamu wapo uwanjani kwa sababu zipi na wanafanya nini wawapo uwanjani, hii inahitaji muda kidogo.
Si vyema sana Ku expose mapungufu ya mchezaji mmojammoja na kuwabebesha lawama.
Simba inahitaji nguvu maeneo yafuatayo;
1. Ufungaji, tusajili top players mfano wa Meshaki Elia kijana wa Tp Mazembe,
Au wachezaji wenye kariba ya vilabu tulivyokuwa tukipambana navyo kipindi hiki hasa kuanzia makundi
2. Usajili uzingatie vigezo muhimu katika kuimarisha nafasi muhimu kama
Ulinzi, na kiungo kwa kuzingatia scouting ya maana iliyofanywa kipindi chote.
Huu si wakati wa kujaribu wachezaji
3. Simba imefanya vizuri sana, kuliko matarajio ya wengi, wala hawakuwahi kuwa na ndoto za kutwaa ubingwa wa afrika!
Lakini wamejaribu kupenya mpaka walipofika,
Tutafika, lakini umakini unahitajika sana!
Unaweza kuona Mbwana Samatta alikuwa akishindana na wachezaji wa aina gani pale Mazembe,
Sent using
Jamii Forums mobile app