Kikosi cha Taifa Stars CHAN na AFCON chatajwa

Alipata majeraha, ila bila hivyo alikua na namba ya kudumu mpaka vilabu vikubwa vilianza kumfuatilia. Bado haja recover kwa asilimia mia.
 
Naona kuna mchezaji kutoka timu ya England ,kuna mwenye rekodi yake
 
Hawa madogo wa u20 kwanini hawamo kwenye list

1. Ally ngazi ( jamhuri ya cheki)
2. Dickson Job ( captain u20)
 
Nampongeza kwa kumwingiza kelvin John.
 
Jamani mimi ni shabiki wa mpira, vitu technical sijui....naomba kuuliza..Rashidi Juma na Paul Godfrey watakua na tatizo gani technically mpala bench la ufundi la Taifa stars haliwaoni?
Japo utapita mchujo DANTE, SHAIBU NINJA, BOXER, AIYEE na R.JUMA walitakiwa kuitwa
 
Kati ya Kapombe na Paul Godfrey ( boxer) yupi alistahili kuitwa kikosini ukizingatia ufanisi wao katika ligi! Kapombe nusu ya msimu alikuwa majeruhi
 
Ujumbe uko wazi, hao ndio wanatesa Bongo maana yake hatuna wachezaji, hili ndilo linawagharimu England miaka yote.
Acha kabisa huo utani wa kufananisha England na Taifa stars. England ana nyota 1 ya World Cup aliyoipata kabla hata ya kina argentina na ufaransa . Amefika nusu fainali mara 2 ya World Cup ikiwemo mwaka jana .
 
Uncle ngassa wamemwacha vipi na ndiyo mzoefu kuliko wote na kiwango kimerudi?🤔
 
Kocha sijui Hugo Mwantika alimuona wapi maana hata mechi za azam zenyewe huwa anakaa benchi!!!
Kuna vijana wameonyesha uwezo mkubwa sana na walifaa kuwepo katika timu ya taifa
Mfano: Paulo Godfrey, Mapinduzi Balama,Rashid Juma.
 
Pata picha Salum Aiyee angekuwa mchezaji wa Simba au Yanga na hajaitwa kwenye hiki kikosi. Unafki wa Soka la Bongo.
 
Huyu kocha aulizwe. .wakina Kanu walivyokuwa under 17 waliitwa timu ya wa kubwa Nigeria. .unamuacha vipi Dida wakati makipa wengine wote hawana uzoefu ukimtoa Manula. ..Ninje huyo kocha mchagulieni wachezaji Sonso anaitwaje anaachwa Dante au Bukabu..arrgg
 
Hahahaaa goli 4 za kufikia tu tena mechi ya kwanza Himid mao, Yahya zaid, Shaban chilunda, Abdi banda, Shiza kichuya, Thomas ulimwengu, na Farid musa ni WAKAA BENCHI WAKUBWA SASA SIJUI WANAKUJA KUFANYA NINI.
hao ndio wakuwaacha! huku sio majaribio tena.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…