Kikosi cha Vipers kina wachezaji wa nje wangapi na wazawa wangapi?

data

JF-Expert Member
Joined
Apr 9, 2011
Posts
26,858
Reaction score
23,768
Na je waliocheza leo wa nje wako wangapi!?? Msaada wadau kuna kitu nataka hitimisha.. maana TZ nafikiri akili zetu nyeusi sanaa...

Mods please!
 
Hii timu wachezaji wake wengi ni wazawa ukiondoa wachache. Pia wengi ni vijana ukiondoa kama Dan senkuruma ambaye aliwahi kuichezea Simba. Taifa stars ijiandae mechi yao na Uganda kwani inaonyesha Uganda wachezaji wazawa ni wazuri
Hiyo tunatolewa na kocha tunafukuza.
Wenzetu uganda wanajielewa kidogo. Wametambua kuwa kupata wachezaji tuanzie mashuleni huko. Sie tulifutaga michezo mashuleni.
Leo tuna mashindano ya u20 lakini imejaa mijeba tuu.

Ligi timu zinasajili wachezaji 12 wakigeni alafu unataka kuwa na national team nzuri...vichekesho hivyo
 
Nawashukuruni sana ndugu wachangiaji!!
Tulishasema mara nyingi sana humu ndani kwamba Simba na Yanga ndio wanauwa soka la Tanzania na na hawana faida yeyote kwa Taifa.

Hamna mahala Taifa litafika kwa kuendekeza wachezaji wa nje.. Inasikitisha sana tunawacelebrate wachezaji wa nje wasio na faida. Usitegemee uzalendo kwa wachezaji wa nje kupigania hivi vilabu vyetu....Africa bado hatujafika huko..

Tuwekeze kwa wachezaji wa ndani... Hakuna haja ya kuendelea subiri.

Ile sio Yanga...na mimi sihesabu ile ni Yanga na ninaacha washabikia Yanga dakika hii... Ile ni Africa..wachezaji wameokotwaokotwa huko wa Kiafrika kuja Tanzania.

Sijui lini litaeleweka hili..
 
Acha ujinga wewe,kwani timu mbili tu?
Kama wapo hao wachezaji si waoneshe uwezo wao kwenye timu nyingine kama Ruvu shooting ?
Mnaendekeza majungu tu na mkicheza timu kubwa mnahongwa na gsm kucheza chini ya kiwango ili kinye washinde.

Leo ni aibu ya kinye FC tu maana ushindi wao wanaupata kwa kubebwa na kuhonga timu pinzani na waamuzi
 
Sikulazimishi kuamini maoni yangu mkuu. Na nyie mpo wengi tu na huwa mnapinga mtizamo huu.. mtizamo wa kisayansi kabisa..

Endeleeni.
 
Na je waliocheza leo wa nje wako wangapi!?? Msaada wadau kuna kitu nataka hitimisha.. maana TZ nafikiri akili zetu nyeusi sanaa...

Mods please!
Mijitu kazi myeusi ya Uganda! Jamaa ni nouma!
,,,,,, Kipindi cha kwanza Yanga walicheza mpira kyliko kipindi cha pili πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€
 
Mie nilijuaga wee ni wa udaku tuu kumbe mambo ya mpira umo....
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] ni mwana lunyasi kindaki ndaki na wa kutupwaaaaa!!!

[emoji881][emoji881][emoji881][emoji881][emoji881][emoji881]
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] ni mwana lunyasi kindaki ndaki na wa kutupwaaaaa!!!

[emoji881][emoji881][emoji881][emoji881][emoji881][emoji881]
Kubembe kwa wana lunyasi kunanpisi kali kali tuu....aya kesho nanyi msitie aibu
 
Nkuu nimekupa like kwa kusoma tu aya yako ya kwanza, sina haja ya kuendelea. That has been my opening remark kila ninapo discuss soka letu la bongo tunalolipenda but lenyewe halitupendi coz hatulilei na kulitendea haki. Kula gwala jingine tena
 
Hii timu wachezaji wake wengi ni wazawa ukiondoa wachache. Pia wengi ni vijana ukiondoa kama Dan senkuruma ambaye aliwahi kuichezea Simba. Taifa stars ijiandae mechi yao na Uganda kwani inaonyesha Uganda wachezaji wazawa ni wazuri
Waganda wengi ni smart kichwani,vijana wengi wamesoma na wanafanya vitu angalau kwa malengo ya kufika mbali. Tofauti na hapa kwetu tunafanya mambo yetu kwa makelele na ushabiki mwingi,vijana wetu nao elimu hawana,wanaishi bila malengo ya mbali,na viongozi wetu wanafanya mambo kwa msukumo wa mashabiki na sio kwa utaalamu.

Mchukue mchezaji mmoja tu wa kiganda kijana mdogo kama Bobosi Byaruhanga na mchukue mchezaji mdogo tu wa kitanzania kama Dickson job,kaa uwasikilize!utagundua Bobosi ana IQ kubwa na malengo makubwa kuliko Job.

Mfano mwingine Lawrence mulindwa Rais wa vipers fc,ametengeneza timu yake ya vijana wadogo vizuri amejenga mpaka uwanja wake ambao kwa sasa ndio uwanja wenye sifa zote kwa mechi za kimataifa pale Uganda,st Mary katende stadium,na wala bwana Lawrence sio tajiri mkubwa ni mipango yake mizuri tu.

Ila kwetu timu haina hata uwanja wa mazoezi ila inanunua mchezaji wa millioni mia nne, ml 400!! ili tu kufurahisha mashabiki!! Bado tuna safari ndefu kwenye sekta ya michezo haya mafanikio ya misimu minne yameletwa na Simba ila sio uhalisia wa hali halisi ya soka letu
 
Mawazo yako ni mazuri sana hasa kwenye kuzalisha wachezaji wazawa hapo nakuunga mkono,ila Tatizo kubwa sio Simba na yanga! Tatizo ni elimu ya watanzania,wachezaji wetu wengi wana elimu ndogo,licha ya vipaji ila elimu bado ni tatizo.

Waganda Wenzetu asilimia kubwa wachezaji wao wana elimu kubwa angalau wanajitambua na ndio maana wanajituma kwa nia ya kwenda mbali!
Wachezaji wetu wazawa kwasababu ya elimu ndogo wakishapata gari used kutoka japani na akapata nyumba tabata na anacheza Simba au yanga kwao ndio mafanikio makubwa!! Mentality hii ikiondoka vichwani mwao mafanikio watayaona na watajituma zaidi, Na mpira wetu utapiga hatua.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…