Kikosi cha Vipers kina wachezaji wa nje wangapi na wazawa wangapi?

Kukuza vijana wazalendo kwenye mpira tulishachelewa. Soka limeshaingia ulimwengu wa kibiashara Tanzania, so kila club inataka mafanikio si ya ndani tu bali hata nje. Swali, utayapata hayo mafanikio kwa wachezaji wa ndani tu katika kupambana na wachezaji wa mataifa na wenye skills mbalimbali kimataifa? Jibu, hapana lazima team zitasajiri wachezaji wa nje ili kusaka mafanikio kibiashara
 
Simba na yanga zimewekeza kununua wachezaji Kwa Bei kubwa angalia makocha wao wa timu za vijana wanashindwa hadi na mtibwa
 
Tanzania sahv mpira umehamia kwenye mipasho tu

Ova
 
Hizi falsafa za kuamini kila Mara wageni ndio Bora,ndicho kinachotuangusha wazawa na timu yetu ya taifa

Sent using Jamii Forums mobile app
Ligi ya Zanzibar kuna wageni wangapi ? Kwenye mashindano ya CAF timu za zanzibar zina mafanikio gani maana asilimia karibu 100 ni wazawa?

Tatizo kubwa wala sio hao wageni. Tatizo kubwa ni kuanzia klabu na taifa kwa ujumla hatuna mifumo sahihi ya soka.

Klabu zetu zikiwemo simba na yanga hawana timu halisia za vijana. Timu za vijana zinatengenezwa panapokuwa na mashindano ya vijana kwa kuokoteza vijana mtaani. Hakuna muendelezo sahihi wa timu za vijana.

Kipindi cha Malinzi walikusanywa vijana kutoka nchi nzima kwamba watengeneze timu ya taifa , walifeli vibaya. Walifeli sio kwa sababu hawajui mpira bali kutopita katika mfumo sahihi wa mpira.
Mpira ni zaidi ya kupiga chenga, kupasia na control. Mchezaji anatakiwa awe na stamina, umakini, nidhamu, kujua mifumo n.k yote haya mchezaji anakuwa nayo akipita kwenye mifumo sahihi ya soka kuanzia akiwa kijana.

Mnasahau kwamba soka halijaanza leo na Taifa stars haijaundwa mwaka jana. Taifa stars ipo tangu enzi hizo ligi yetu haina hata mgeni mmoja, lakini je kuna cha maana cha kujivunia kutoka kwa taifa stars ya enzi hizo?
 
Nkuu nimekupa like kwa kusoma tu aya yako ya kwanza, sina haja ya kuendelea. That has been my opening remark kila ninapo discuss soka letu la bongo tunalolipenda but lenyewe halitupendi coz hatulilei na kulitendea haki. Kula gwala jingine tena
Tuna kitu cha kufanya kama taifa..hakuna mahali tutafika
 
Timu ya Taifa achaneni nayo ata ifike kombe la dunia haijawai kuwa na mvuto
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…