A
Anonymous
Guest
Kuna jambo linaniumiza sana kuhusu utendaji kazi wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji (Fire), imekuwa ni tabia iliyozoeleka kwamba tukio la dharura kama moto likitokea, badala ya kufika kwa haraka kuokoa jahazi, wanafika wakati kitu kimeshaungua na kuteketea kabisa ndiyo wanaonekana!
Kwa mfano, juzikati katika eneo la Maili Moja - Kibaha karibu kabisa na stendi mpya, kulikuwa na basi lililoshika moto na kuteketea, cha kushangaza, umbali kutoka Kituo cha Zimamoto na Uokoaji mpaka pale mahali basi lilipokuwa linaungua hata kilomita moja haifiki.
Pamoja na kwamba umbali ni mfupi hivyo na taarifa walipewa mapema kabisa, basi liliteketea lote mpaka likawa majivu kabla hawajafika!
Wamekuja kuwasili dakika za mwisho kabisa wakati gani limeshaungua lote, sasa mtu unajiuliza huduma kama hiyo ya zimamoto ni ya nini kama wanakuja kushuhudia majivu?