Kikristo, uchawi haupo

Kutoka 22:18 Usimwache mwanamke mchawi aishi.

Mleta mada, kwanini unaongelea vitu usivyovijua?
Kila dini ina kanuni zake.

Dini zote zina pande mbili, wa giza, na wa nuru

Kikristo giza ni la shetani, nuru ni ya mungu

Nataka nione mahali bibilia inasema uchawi umetoka kwa shetani/ni kazi ya shetani

Uchawi uliozungumziwa hapo, unatoka kwenye dini zingine, yaani huyo mwanamke anafuata ibada za kipagani
 
1. Ni imani za jadi tumechanganya na ukristo. Muulize Kiranga kama huko mambele wakristo wanaamini kwenye ulozi.

2. Ukristo unatambua uchawi ndio. Lakini hausemi kwamba umetoka kwa mungu wala shetani. Uchawi ilikua ni kufuata dini zingine mfano kina Baal, Dagon...
 
Soma na hapa Mkuu Kumbukumbu la Torati 18:11–12 “alogaye, au mtu alogaye kwa pepo, au mwenye pepo, au awaulizaye wafu .
 
Je, huo uchawi aliutoa wapi?
 
Uelewa wako Bado ni Mdogo sana kuweza mimi kukujibu.
Unahitaji kusoma sana juu ya imani ya Ukristo.
Andiko lako lina makosa mengi sana ya kuwa chini ya viwango.
 

ukristo baada ya kuanzishwa ulienea sana ulaya kipindi cha mediaval age ( middle age) kipindi hiki ( canon laws) ama sheria zilizokuwa zinatumika kuendesha taifa ( state laws) ni sheria za kikristo ama sheria za kanisa. kitu kilichoandikwa kwenye biblia ndio kilikuwa kinafatwa.

uchawi hapo ndipo ulipovuma pia. watu waliokuwa anti church ama hawaeleweki walitambulika kama wachawi na hukumu yao walikuwa wanauwawa kwa kunyongwa hadharani, maana biblia imeandika usimuache mchawi aishi.

mbeleni kwenye modern era wazungu wakagundua uchawi haupo ndipo wakaachana na hizo laws. baada ya kutenganisha sheria za kanisa na sheria za nchi

Ukristo na uchawi ni vitu vinavyosapotiana yaani kama Mungu na Shetani

ukiamini ukristo ni lazima uamini na uchawi upo
 
New revised standard version ndo toleo sahihi kuliko yote ya bibilia
View attachment 2925335
Toleo zuri la biblia yoyote ni toleo kabla ya mambo ya feminism ina maana toleo la 1970 kurudi nyuma. Hayo ndio yako sawa.

Mfano usishangae ukakuta biblia.za sasa zinazosema usimuache Mtu mchawi aishi. yaani wametoa neno Mwanamke na kuweka Mtu. Sasa haya matoleo mapya sio matoleo bora kiivyo.
 
Ni wapi bibilia inasema kwamba uchawi umetokana na mungu au shetani?

Tunaambiwa tukipata shida tuombe na tutubu

Tutoe sadaka

Ni wapi imeandikwa 'shetani alileta uchawi duniani, ili kuwatesa watu wa mungu'?

Umenielewa?

Uchawi sio sehemu ya ukristo, ni mapokeo ya kijamii
 
theologists ndo wanatumia...
 
umeandika utumbo
 


unashindwa kunielewa, mimi siamini biblia na hakuna sehemu nimeweka mstari wa biblia.

mimi naongela imani ya uchawi na imani juu ya ukristo jinsi zinavyo relate. na nimekueleza maisha ya ulaya kipindi cha medieval age, nikakueleza canon laws zilitoka wapi na jinsi hizo laws zilivyokuwa zinahukumu wachawi.

hata leo hii ukienda kanisani lazima uchawi uongelewe, ni lazima shetani aongelewe.

sababu ukristo unatambua uchawi upo na wachawi na shetani ni adui ya ukristo,


hivyo haiwezekani mtu awe anaamini ukristo ni imani ya kweli halafu asiamini uchawi upo, wakati mafundisho ya ukristo yanautaja uchawi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…