Kikristo, uchawi haupo

Kikristo, uchawi haupo

Kutoka 22:18 Usimwache mwanamke mchawi aishi.

Mleta mada, kwanini unaongelea vitu usivyovijua?
Kila dini ina kanuni zake.

Dini zote zina pande mbili, wa giza, na wa nuru

Kikristo giza ni la shetani, nuru ni ya mungu

Nataka nione mahali bibilia inasema uchawi umetoka kwa shetani/ni kazi ya shetani

Uchawi uliozungumziwa hapo, unatoka kwenye dini zingine, yaani huyo mwanamke anafuata ibada za kipagani
 
mbona uhahamisha mada, hapa hatuongelei majini

hapa tunaongelea uchawi, yaani imani juu ya uchawi, jiulize je bibilia ama kanisani Uchawi ama wachawi hawazungumziwi kwenye ibada ama maombi ?

mfano mimi ni Atheist siamini dini yoyote, na wala siamini uwepo wa Mungu, naanzia wapi kuamini uwepo wa Uchawi ama wachawi ? maana biblia iliyotaja kuhusu wachawi sina imani nayo, quran iliyotaja kuhusu wachawi sina imani nayo.

Ukiona unaamini Ukristo maana yake unaamini uchawi upo pia, maana mafundisho ya ukristo yanatambua uchawi upo
1. Ni imani za jadi tumechanganya na ukristo. Muulize Kiranga kama huko mambele wakristo wanaamini kwenye ulozi.

2. Ukristo unatambua uchawi ndio. Lakini hausemi kwamba umetoka kwa mungu wala shetani. Uchawi ilikua ni kufuata dini zingine mfano kina Baal, Dagon...
 
Kila dini ina kanuni zake.

Dini zote zina pande mbili, wa giza, na wa nuru

Kikristo giza ni la shetani, nuru ni ya mungu

Nataka nione mahali bibilia inasema uchawi umetoka kwa shetani/ni kazi ya shetani

Uchawi uliozungumziwa hapo, unatoka kwenye dini zingine, yaani huyo mwanamke anafuata ibada za kipagani
Soma na hapa Mkuu Kumbukumbu la Torati 18:11–12 “alogaye, au mtu alogaye kwa pepo, au mwenye pepo, au awaulizaye wafu .
 
Matendo 8:18
Simoni aliyekuwa mchawi alipoona Roho Mtakatifu anatolewa kwa watu kwa kuweka mikono juu yao. Aliwapa pesa mitume. 19 Akasema, “Nipeni na mimi nguvu hii ili nitakapoweka mikono yangu juu ya mtu yeyote, atampata Roho Mtakatifu.”
Je, huo uchawi aliutoa wapi?
 
Soma na hapa Mkuu Kumbukumbu la Torati 18:11–12 “alogaye, au mtu alogaye kwa pepo, au mwenye pepo, au awaulizaye wafu .
New revised standard version ndo toleo sahihi kuliko yote ya bibilia
www.bible.com_sw_bible_2016_DEU.18.11.NRSV(Samsung Galaxy S20 Ultra) (2).png
 
Napinga.

Uchawi upo kwenye dini zingine ila sio ukristo

Najikita kwenye mantiki

Hakuna mahali popote kwenye bibilia shetani au mungu amehusishwa na uchawi

Ni kama majini, wao ni wahusika wa kiislamu tu, wanatumika kwenye misaafu ya kiislamu tu

Huwezi bibilia inazungumzia majini

Kila dini ina Lore(Simulizi) yake ya kipekee juu ya mungu, nguvu za giza na viumbe wasioonekana. Haziingiliani.
Uelewa wako Bado ni Mdogo sana kuweza mimi kukujibu.
Unahitaji kusoma sana juu ya imani ya Ukristo.
Andiko lako lina makosa mengi sana ya kuwa chini ya viwango.
 
1. Ni imani za jadi tumechanganya na ukristo. Muulize Kiranga kama huko mambele wakristo wanaamini kwenye ulozi.

2. Ukristo unatambua uchawi ndio. Lakini hausemi kwamba umetoka kwa mungu wala shetani. Uchawi ilikua ni kufuata dini zingine mfano kina Baal, Dagon...

ukristo baada ya kuanzishwa ulienea sana ulaya kipindi cha mediaval age ( middle age) kipindi hiki ( canon laws) ama sheria zilizokuwa zinatumika kuendesha taifa ( state laws) ni sheria za kikristo ama sheria za kanisa. kitu kilichoandikwa kwenye biblia ndio kilikuwa kinafatwa.

uchawi hapo ndipo ulipovuma pia. watu waliokuwa anti church ama hawaeleweki walitambulika kama wachawi na hukumu yao walikuwa wanauwawa kwa kunyongwa hadharani, maana biblia imeandika usimuache mchawi aishi.

mbeleni kwenye modern era wazungu wakagundua uchawi haupo ndipo wakaachana na hizo laws. baada ya kutenganisha sheria za kanisa na sheria za nchi

Ukristo na uchawi ni vitu vinavyosapotiana yaani kama Mungu na Shetani

ukiamini ukristo ni lazima uamini na uchawi upo
 
New revised standard version ndo toleo sahihi kuliko yote ya bibilia
View attachment 2925335
Toleo zuri la biblia yoyote ni toleo kabla ya mambo ya feminism ina maana toleo la 1970 kurudi nyuma. Hayo ndio yako sawa.

Mfano usishangae ukakuta biblia.za sasa zinazosema usimuache Mtu mchawi aishi. yaani wametoa neno Mwanamke na kuweka Mtu. Sasa haya matoleo mapya sio matoleo bora kiivyo.
 
ukristo baada ya kuanzishwa ulienea sana ulaya kipindi cha mediaval age ( middle age) kipindi hiki ( canon laws) ama sheria zilizokuwa zinatumika kwenye maisha ni sheria za kikristo ama sheria za kanisa. kitu kilichoandikwa kwenye biblia ndio kilikuwa kinafatwa.

uchawi hapo ndipo ulipovuma pia. watu waliokuwa anti church ama hawaeleweki walitambulika kama wachawi na hukumu yao walikuwa wanauwawa kwa kunyongwa hadharani, maana biblia imeandika usimuache mchawi aishi.

mbeleni kwenye modern era wazungu wakagundua uchawi haupo ndipo wakaachana na hizo laws.

Ukristo na uchawi ni vitu vinavyosapotiana yaani kama Mungu na Shetani

ukiamini ukristo ni lazima uamini na uchawi upo
Ni wapi bibilia inasema kwamba uchawi umetokana na mungu au shetani?

Tunaambiwa tukipata shida tuombe na tutubu

Tutoe sadaka

Ni wapi imeandikwa 'shetani alileta uchawi duniani, ili kuwatesa watu wa mungu'?

Umenielewa?

Uchawi sio sehemu ya ukristo, ni mapokeo ya kijamii
 
Toleo zuri la biblia yoyote ni toleo kabla ya mambo ya feminism ina maana toleo la 1970 kurudi nyuma. Hayo ndio yako sawa.

Mfano usishangae ukakuta biblia.za sasa zinazosema usimuache Mtu mchawi aishi. yaani wametoa neno Mwanamke na kuweka Mtu. Sasa haya matoleo mapya sio matoleo bora kiivyo.
theologists ndo wanatumia...
 
Kibongo bongo wakristo wengi wanaamini kwenye uchawi.

Ndio wanauchukulia kama kitu kibaya, lakini kwa vile wanakubali uwepo wake basi inamaanisha wanaamini upo.

Lakini cha kushangaza, kimantiki, bibilia haiongelei kabisa kuhusu uchawi.

Nikimaanisha kwamba hakuna mahali ilipoandikwa kwamba mungu au shetani wana uhusiano wowote na uchawi.

Vimekatazwa kwasababu ni njia za ibada za mataifa mengine kama canaanites, romans nk, ni kutoka nje ya misingi ya dini...

Bibilia imelaani vitu kama kuabudu sanamu, kuongea na wafu, foreseeing(kutumia uchawi kutabiri nyakati) lakini haijasema kwamba hivyo vitu vinahusiana na shetani.

Na hata hadithi zote za mapepo, hakuna mahali ulozi umetajwa kama chanzo, na imesemwa mapepo ni wale malaika waasi.

Ninachokiona ni kwamba haya mambo ya uchawi ni ya kwetu sisi, ukristo uliyakuta, tukayachanganya na ukristo.

Mambo kama irizi, matambiko, misukule nk ni imani za jadi kabisa.

Na ndio maana wakristo wa nchi zilizoendelea hawaamini kwenye uchawi, wanaamini kwenye mapepo.

Hata mambo ya nyota, sijui nyayo, anga, viganja hayapo kwenye bibilia, ni mistari inatafsiriwa kitofauti.

Kwahiyo kikristo kweye upande wa mwanga kuna Yahweh na malaika wake, kwenye giza kuna shetani na mapepo yake.

Kimantiki mkristo ukiamini uchawi maana yake unahama dini/unachanganya dini tofauti.
umeandika utumbo
 
Ni wapi bibilia inasema kwamba uchawi umetokana na mungu au shetani?

Tunaambiwa tukipata shida tuombe na tutubu

Tutoe sadaka

Ni wapi imeandikwa 'shetani alileta uchawi duniani, ili kuwatesa watu wa mungu'?

Umenielewa?

Uchawi sio sehemu ya ukristo, ni mapokeo ya kijamii

unashindwa kunielewa, mimi siamini biblia na hakuna sehemu nimeweka mstari wa biblia.

mimi naongela imani ya uchawi na imani juu ya ukristo jinsi zinavyo relate. na nimekueleza maisha ya ulaya kipindi cha medieval age, nikakueleza canon laws zilitoka wapi na jinsi hizo laws zilivyokuwa zinahukumu wachawi.

hata leo hii ukienda kanisani lazima uchawi uongelewe, ni lazima shetani aongelewe.

sababu ukristo unatambua uchawi upo na wachawi na shetani ni adui ya ukristo,

hivyo haiwezekani mtu awe anaamini ukristo ni imani ya kweli halafu asiamini uchawi upo, wakati mafundisho ya ukristo yanautaja uchawi
 
Back
Top Bottom