Kikristo, uchawi haupo

Kikristo, uchawi haupo

Kibongo bongo wakristo wengi wanaamini kwenye uchawi.

Ndio wanauchukulia kama kitu kibaya, lakini kwa vile wanakubali uwepo wake basi inamaanisha wanaamini upo.

Lakini cha kushangaza, kimantiki, bibilia haiongelei kabisa kuhusu uchawi.

Nikimaanisha kwamba hakuna mahali ilipoandikwa kwamba mungu au shetani wana uhusiano wowote na uchawi.

Vimekatazwa kwasababu ni njia za ibada za mataifa mengine kama canaanites, romans nk, ni kutoka nje ya misingi ya dini...

Bibilia imelaani vitu kama kuabudu sanamu, kuongea na wafu, foreseeing(kutumia uchawi kutabiri nyakati) lakini haijasema kwamba hivyo vitu vinahusiana na shetani.

Na hata hadithi zote za mapepo, hakuna mahali ulozi umetajwa kama chanzo, na imesemwa mapepo ni wale malaika waasi.

Ninachokiona ni kwamba haya mambo ya uchawi ni ya kwetu sisi, ukristo uliyakuta, tukayachanganya na ukristo.

Mambo kama irizi, matambiko, misukule nk ni imani za jadi kabisa.

Na ndio maana wakristo wa nchi zilizoendelea hawaamini kwenye uchawi, wanaamini kwenye mapepo.

Hata mambo ya nyota, sijui nyayo, anga, viganja hayapo kwenye bibilia, ni mistari inatafsiriwa kitofauti.

Kwahiyo kikristo kweye upande wa mwanga kuna Yahweh na malaika wake, kwenye giza kuna shetani na mapepo yake.

Kimantiki mkristo ukiamini uchawi maana yake unahama dini/unachanganya dini tofauti.
Farao aliita wachawi na waganga.............
Musa akatupa fimbo ikawa nyoka....nao wakatupa fimbo zikawa nyoka.....lakini nyoka ya Musa ikameza nyoka za wachawi.......
 
Napinga.

Uchawi upo kwenye dini zingine ila sio ukristo

Najikita kwenye mantiki

Hakuna mahali popote kwenye bibilia shetani au mungu amehusishwa na uchawi

Ni kama majini, wao ni wahusika wa kiislamu tu, wanatumika kwenye misaafu ya kiislamu tu

Huwezi bibilia inazungumzia majini

Kila dini ina Lore(Simulizi) yake ya kipekee juu ya mungu, nguvu za giza na viumbe wasioonekana. Haziingiliani.
asa hao viumbe wasio onekana waliumbwa kwaajili yanini mbon hawana faida nasisi.? au ndo hao virus na bacteria hadi tutumie binoculars.?
 
ukristo baada ya kuanzishwa ulienea sana ulaya kipindi cha mediaval age ( middle age) kipindi hiki ( canon laws) ama sheria zilizokuwa zinatumika kuendesha taifa ( state laws) ni sheria za kikristo ama sheria za kanisa. kitu kilichoandikwa kwenye biblia ndio kilikuwa kinafatwa.

uchawi hapo ndipo ulipovuma pia. watu waliokuwa anti church ama hawaeleweki walitambulika kama wachawi na hukumu yao walikuwa wanauwawa kwa kunyongwa hadharani, maana biblia imeandika usimuache mchawi aishi.

mbeleni kwenye modern era wazungu wakagundua uchawi haupo ndipo wakaachana na hizo laws. baada ya kutenganisha sheria za kanisa na sheria za nchi

Ukristo na uchawi ni vitu vinavyosapotiana yaani kama Mungu na Shetani

ukiamini ukristo ni lazima uamini na uchawi upo
mungu kwanin asimuue mwenyew tu huyo mchawi anatuambia sisi.? natena anasema tusihukumu tutahukumiwa.? tena kasema tusiuwe.? mbon mambo yanakua na process nyingi ivi😳.? hapo ndo napishana na waislamu ivi wale wapiganaji wakiislamu kwanin hua wana mfanyia mungu majukumu yake mfano mtu akiacha uislamu inabini auwawe. ivi mungu simuweza wayote ashindwi na chochote.? ivi kweli atakosa chakumfanya mtu alie msaliti.!? 🤔
 
Back
Top Bottom