PreGE2025 Kikulacho kinguoni mwako Chadema inarudishwa Nyuma na wanachadema wenyewe

PreGE2025 Kikulacho kinguoni mwako Chadema inarudishwa Nyuma na wanachadema wenyewe

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

DuaZaMama

JF-Expert Member
Joined
Jun 2, 2025
Posts
1,882
Reaction score
4,153
Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kinaendelea kukumbwa na changamoto za ndani baada ya Mahakama Kuu kutangaza kusitisha shughuli zake za kisiasa kwa kipindi cha siku 14.

Kesi hiyo yenye namba 8323 ya mwaka 2025, imefunguliwa na mwanachama wa chama hicho, Said Issa Mohamedi pamoja na wenzake wawili, na kusikilizwa na Jaji wa Mahakama Kuu, Hamidu Mwanga.

Uamuzi huu umeongeza matatizo ndani ya Chadema, hasa baada ya Msajili wa Vyama vya Siasa kutokutambua baadhi ya viongozi wa chama hicho, ikiwemo Katibu Mkuu John Mnyika, kwa madai ya dosari katika taratibu za uteuzi wao.

Soma Pia: Rasmi, Mahakama yapiga marufuku shughuli zote za CHADEMA


Kwa kufungiwa kwa shughuli za kisiasa, Chadema italazimika kusitisha ziara zake mikoani zinazolenga kuinua kampeni na kutangaza chama katika mikoa mbalimbali ya Tanzania.

Wakuu

Ni ngumu kiasi kutokuisikia No reforms No election Kwa siku 14?
-1320143392.jpg
 
Kwa hiyo Hamudu ni mwanachama wa chadema au ndio upeo wako wa kuwaza umeishia hapo
 
Back
Top Bottom