Kikundi cha Wakali Mawe

Kikundi cha Wakali Mawe

karv

JF-Expert Member
Joined
Dec 26, 2019
Posts
1,802
Reaction score
3,253
Habari ya wakati huu

Leo katika pekua pekua yangu nikakutana na picha niliyopiga nikiwa olevel zile zenye negative kwa nyuma [emoji1787] Dah nikakumbuka maisha yangu ya olevel. Hasa kundi moja linaitwa WAKALI MAWE

Naamini wengi wetu wakati tupo olevel iwe shule ya kutwa au bweni mlikuwa na makundi au mshawahi kuyaona makundi mbali mbali ambayo mnasaidiana mambo kama vile masomo, kazi, kupata pisi kali, kula chakula kwa pamoja wakati mwingine adhabu pamoja na maswali mbali mbali ya shuleni.

Sasa niliposoma mimi palikuwa na kundi la wanafunzi kama 10 - 12 wenyewe walikuwa wanajiita WAKALI MAWE. Ilikuwa ni shule ya kutwa hivyo mambo mengi mtaani walikuwa wanafanya pamoja.

Hawa jamaa wanaojiita wakali mawe walikuwa wanafahamika hadi kwa mkuu wa shule na ili ujiunge hapo lazima uwe na sifa kama:-
~Ufahamu kupigana/kareti (kama hujui watakufundisha)
~Ujue kuogelea
~Lazima uwe unajua mchezo wowote ambao unaweza kukupeleka UMISETA
~Usiwe muoga wa kutongoza
~Utoe michango.
~Uwe na ratiba ya sherehe na matukio mbalimbali pale kijijini yenye uwepo wa chakula.

Hao jamaa wanaojiita wakali mawe shuleni walikuwa wapole sana na sio wagomvi lakini nje ya eneo la shule Member wake wamefanya matukio ya ajabu sana pale mtaani kama :-
~Kuna mmoja wao alimpiga mwalimu na mabati baada ya kuzinguana shuleni akasimamishwa shule akawa anasubiri kikao cha bodi ya shule kesi haijawahi kuisha.
~Kuna mwingine alimchana mwanafunzi mwenzie na viwembe ugomvi wa shuleni akauhamishia mtaani
~Mkuu wao alienda kumdai mwalimu viatu vyake nyumbani baada ya kupokonywa shule.
~Matukio ya kupigana mtaani na kugombea wanawake ndio usiseme kabisaa.

Hao WAKALI MAWE walikuwa na michezo hatari sana nakumbuka siku moja mto ulikuwa umejaa maji basi wakajichanga wakanunua wali wa elfu moja yule anayejua kuliko wote akaenda kuogelea hadi mtoni kwenye kina kirefu halafu kila mwanachama unaenda unapiga tonge moja la ubwabwa kuogelea unaondoka. Tonge lako likiingia maji ndio basi tena.

Pia hawa WAKALI MAWE walikuwa hawapitwi na shuhuri kama msiba, harusi, vigodoro, maulidi nk. Walikuwa na mtu wao huyo msiba ukitokea mahala anaweka mawe arobaini halafu kila siku anatoa jiwe moja likibaki moja anawaambie wenzake wanaenda kwenye arobaini ya msiba wanakula.

Hawa WAKALI MAWE nimewakumbuka katika tukio hili.

Siku moja kulitokea shughuli ya Arobaini ya msiba na maulid ya mtoto katika vijijini viwili tofauti na vijiji hivyo vimetenganishwa na mto tu.

Basi baada ya jamaa kupata taarifa kwanza wakaenda mtoni wakaogelea sana wakafanya kila aina ya fujo pale mtoni ilipofika saa 6 wakaamua kwenda kwenye Arobaini wakale zao wali waondoke.

Walivyofika pale wakakuta chakula bado ila watu wanasoma dua na mambo mengine.Yule mtoa taarifa wao sasa akawaambia waende kwanza kwenye kile kijiji chenye maulid wakale huko halafu ndio warudi kula huku.

Kutoka kwenye hiko kijiji ni mwendo wa saa moja na nusu ukipita mtoni kwa kuogelea na masaa mawili ukipita kwenye daraja.

Basi jamaa wakapita zao mtoni wakaogelea hadi upande wa pili safari ya kwenda kwenye maulid ikaanza. Walipofika kule wakakuta watu washakula tayari. Wakaamua wawahi warudi huku kwenye hitima wakayakata maji mtoni chap kwa haraka. Kufika kwenye hitima wakakuta watu ndio wanatawanyika, wanawake wanaosha vyombo [emoji1787].

Hawa jamaa wakiendaga kwenye shughuli walikuwa wanaenda na mifuko yao ya plastiki. Wakati nyie mnagombania kula wao wanapiga tonge wanaweka kwenye mifuko. Wanazunguka kwenye sinia hata sita [emoji1787].

Pamoja na kuripotiwa sana pale shuleni na mtaani lakini kundi hilo halikuwahi kuvunjika hadi wanamaliza kidato cha nne.

Pia walikuwa na mazuri yao
~walituwakilisha vizuri sana kama shule katika swala zima la michezo.


.......MUNGU AWABARIKI POPOTE MLIPO WAKALI MAWE.....
 
Back
Top Bottom