Kikundi cha washangiliaji wa Taifa stars chaomba msaada bungeni kipelekwe Misri wenyewe hawana hata senti moja!

Kikundi cha washangiliaji wa Taifa stars chaomba msaada bungeni kipelekwe Misri wenyewe hawana hata senti moja!

johnthebaptist

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2014
Posts
97,869
Reaction score
171,716
Mwenyekiti wa kikundi cha wahamasishaji na washangiliaji wa Taifa stars wameomba kuchangiwa na wabunge, wanasiasa na wananchi ili waweze kwenda Cairo, Misri.

Kikundi hicho kina jumla ya vijana 30 wa amsha amsha ambao wote hawana passport hivyo kwa kuanzia wameomba jumla ya sh milioni 5 ili wapatiwe passport. Mwenyekiti amesema RC Makonda amewasaidia kwa kiasi fulani taratibu za pale Uhamiaji na kilichobakia ni malipo tu.
Baada ya hapo bunge linaweza kuwasaidia tiketi za ndege ili wananchi wengine wawachangie gharama za hoteli na usafiri wa ndani wakiwa Cairo.

Mwisho Mwenyekiti wa kikundi hicho amedai hii ni vita kama ile ya Kagera iliyomfurusha nduli Amini hivyo shime wananchi wachangieni vijana hawa 30 wakatutoe kimasomaso.

Source ITV kumekucha michezo

Maendeleo hayana vyama!
 
Kuna waheshimiwa wabunge kama 80 hivi wameshajipanga kwenda kushangilia. Hivi hao waheshimiwa ni washangiliaji au ni watu tu wanaoenda kutalii na kula posho. Waache huo upuuzi wawape posho hao vijana wakashangilie timu siyo hao wauza sura
Wale akina Ndugai, Ngeleja, Mbowe nk.....wanaenda kutalii tu makoo yamejaa bia watashangilia nini!
 
NIPO TAYALI KUWACHNGIA. NAWAKUBALI SANA HAWA JAMAAA MWANZO MWISHO
 
[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]

Tufungwe tu, tufungwe kabisa, hadi akili zitukae sawa.....

Taifa Stars ingekuwa timu bora watu wangefurika kwenda kuishangilia kwa moyo mkunjufu kabisa na wala sio mambo ya uhamasishaji na blaa blaa kibao zisizokuwa na mashiko..

Muarobaini katika hili ni kufuma kikosi imara chenye kuleta ushindani, hapo mashabiki watavutiwa na kwenda kuishangilia wenyewe popote itakapoenda kupambana.
 
Back
Top Bottom