johnthebaptist
JF-Expert Member
- May 27, 2014
- 97,869
- 171,716
Mwenyekiti wa kikundi cha wahamasishaji na washangiliaji wa Taifa stars wameomba kuchangiwa na wabunge, wanasiasa na wananchi ili waweze kwenda Cairo, Misri.
Kikundi hicho kina jumla ya vijana 30 wa amsha amsha ambao wote hawana passport hivyo kwa kuanzia wameomba jumla ya sh milioni 5 ili wapatiwe passport. Mwenyekiti amesema RC Makonda amewasaidia kwa kiasi fulani taratibu za pale Uhamiaji na kilichobakia ni malipo tu.
Baada ya hapo bunge linaweza kuwasaidia tiketi za ndege ili wananchi wengine wawachangie gharama za hoteli na usafiri wa ndani wakiwa Cairo.
Mwisho Mwenyekiti wa kikundi hicho amedai hii ni vita kama ile ya Kagera iliyomfurusha nduli Amini hivyo shime wananchi wachangieni vijana hawa 30 wakatutoe kimasomaso.
Source ITV kumekucha michezo
Maendeleo hayana vyama!