KIKUU wataacha lini kuuza bidhaa feki?

KIKUU wataacha lini kuuza bidhaa feki?

Cytochrome p450

JF-Expert Member
Joined
Mar 19, 2019
Posts
5,638
Reaction score
15,044
Wakuu,

Hawa jamaa nimewachoka sasa. Mara ya kwanza niliagiza mzigo mwaka jana, ilikua ni Flash ya 128 GB kwenye Limited Offer.
Cha kushangaza ilidumu kwa siku 5 tu, ikawa haifanyi kazi tena kwenye computer.

Chengine kinachoboa zaidi ni muda unaochukua mpaka kupata bidhaa yako.
Mali yako inakaa mpaka unasahau kama uliagiza mzigo.

Juzi kati hivi, kuna jamaa yangu aliagiza Projector kwa ajili ya kuonyeshea mpira, quality imekuja mbovu kabisa ukilinganisha na specification walizoweka kwenye mtandao wao.

Kuna mwengine nilimsikia eti alinunua iPhone 6 kwenye Limited Offer kwa 290, kuja kuiwasha ni fake! fake! fake! Haifai!!

Hakuna namna nyengine zaidi ya kuwakimbia tu.

Tuendelee kuingia Kariakoo, maisha yaendelee.
 
Alibaba au?
ali express
Screenshot_2020-01-25-23-45-25.png
 
Kwanini wasirudishe kama bidhaa hiyo haijakidhi matarajio yao.

Na akirudisha ndani ya siku3 Ukitaka kutudishiwa hela unarudishiwa
Ukitaka bidhaa utasubir kidogo
Duh! Inawezekana hiyo? Sikuwahi kujua kabsaa.
 
Back
Top Bottom