Kila kitu au jambo linalotaka kufanyika au kutimizwa lazima awepo kiongozi na wahamasishaji, Jaman wananchi mtaani walio wengi wanasubiri mtu wa kuhamasisha maandamamo ya kimapinduzi.
Hali ya maisha imekuwa ngumu sanaa, sanaaa sanaaa imagine bidhaa kama mafuta ya taa imefika 2000 kwa lita hili ni balaa kwani wananchi wengi hawawezi kumudu gharama za mkaa na gesi sasa kimbilio lao la umeme ndo huo nao haupo.
Ukiachilia gharama kama mkate, mchele, unga, maharage na nafaka nyinginezo yaani kila kitu kimepanda.
Imagine, hii hali inamkumba mtu wa aina moja tuu naye ni mtu wa kipato cha chini ambaye kwake milo mitatu kwa siku kwake ni anasa, jaman tumesalitiwa na viongozi wetu.
My take:
1. presidar hawezi kujiuzuru kwa hiari mpaka kinuke
2. Kwa jinsi navyoona mwelekeo wa wanasiasa wa upinzani itakuwa ngumu kumobilize mapinduzi nchi nzima kwani kunawasaliti ndani yao.
3. Vyama vya kilaia na wapigania haki za binadamu waungane kuhamasisha mapinduzi.