Gottee,
Nakuhakikishia kitu kimoja, sina nia ya kuzuia mijadala kuhusu matatizo mkoani Mbeya. Binafsi ni mwumini wa uhuru wa kujadili jambo lolote.
Ninachopinga mimi ni watu kuja na madai makubwa sana ambayo hayana ukweli. Inabidi tuwe responsible kidogo kwasababu haya mambo yote yanaikwamisha Mbeya. Kuna vijana kule kwasababu ya ujinga wao, wanaona kila kitu kilichoandikwa magazetini ni ukweli na wanaanza kuamini.
Hata nikiwa Kyela au Mbeya nawaambia hivyo hivyo kama nilivyoandika hapa, kwamba sio kweli. Ukiwauliza umesikia wapi, wanasema yaliandikwa gazetini.
Prof. Mwandosya na JK walikuwa makundi tofauti na sio marafiki wa karibu kwa miaka mingi, huo ni ukweli lakini je kunachuki kubwa kati yao kwasasa? Siamini hivyo na wala sijaona ushahidi huo.
Kuna watu kwenye kundi la JK wangependa kuendeleza huo mgogoro kama ambavyo wangependa kuendeleza mgogoro wa JK na Salim. What matters here ni msimamo wa JK na profesa mwenyewe. Pia kuna watu wa prof. ambao wangependa kuendeleza mgogoro na JK.
Kuna watu wanafikiri hata kuanguka kwa Lowassa ni njama za prof. eti Dr. Mwakyembe alitumiwa na prof. kumlima JK na kundi lake. Jamani, ina maana wajumbe wale wote wa ile kamati, wataburuzwa na Mwakyembe kwa faida ya prof.?
Kuhusu vijana kumwita Prof. rais wao, kuna tofauti gani na vijana wa CHADEMA kumwita Mbowe rais? Kuna tofauti gani na TLP au NCCR huko nyuma kumwita Mrema rais? Ni kundi dogo la vijana ndio wanaendeleza hayo mambo kwenye vijiwe vyao badala ya kwenda kwenye uzalishaji mali.
Kule Mbeya kuna watu wamefanya ni career kupeleka majungu kwa Mwakipesile au Mwakyembe. Na kukiwa na wanasiasa njiwa, ni rahisi mno kukubaliana na watu kama hao ambao kwa kweli ni waganga njaa.
Nikupe mchapo wangu mmoja wa kweli. Nikiwa likizo Kyela, wakati napita ile barabara ya Kyela, nilimwona diwani mmoja ambaye mimi nilisoma naye msingi, alikuwa pamoja na diwani mwenzake ambaye nilikuwa simfahamu kabla ya hapo. Nikaenda kuwasalimia, tukaanza michapo mbalimbali, baadaye wakaniomba kama kuna mtu namjua Dar awasaidie, wametumwa na wilaya kwenda kutafuta wanunua Kokoa wameuza kiasi gani nje ili wajue kama Halmashauri ya Kyela imelipwa ipasavyo. Mimi nikatafuta contacts zangu na kuwaunganisha na mhusika.
Baada ya siku kama tatu, jamaa yangu mwingine ambaye ni rafiki yake Dr. Mwakyembe akaanza kuniuliza juu ya mimi kuongea na hao madiwani. Akasema kuna wapambe wa Dr wameniona na habari imeenda kwake. Nikacheka tu, hata Dr. naamini aliwadharau tu. Wengine tumekuwa tukiambiwa tunataka kugombea toke 95, 2000, 2005 na sitashangaa tukitajwa 2010. Kumbe hao madiwani wawili ni watu wa mkuu wa mkoa, mimi hata sikujua ingawaje huyu niliyesoma naye niliwahi kusikia alimwunga mkono Mwakipesile mwaka 2005.
Mimi wanaoniuliza nawaambia wazi, siku ikifika nitasema mwenyewe, wala sitasingizia nimefuatwa na wazee au nini. Nikiamua kuingia kwenye siasa kila mtu atajua wala hakuna haja ya kuficha. Kwasasa muhimu ni kwamba tuna viongozi wacha watimize majukumu yao bila bugudha za majungu.
Huko mikoani kuna madudu mengi sana, ndio maana wakati mwingine mimi huwa nachukia juu ya jambo hili. Majungu ya kisiasa na ushirikina yanaua zile wilaya zetu.