Kikwete aamuru mitambo ya IPTL iwashwe mara moja!

Ina maana mapendekezo ya Zitto - kuwasha IPTL na kutaifisha Dowans - ndio silver bullet ya matatizo ya umeme Tanzania?

You say that. Nobody said that. Hakuna mwenye akili anayeweza kusema hivyo. Tunazungumzia kutatua tatizo la sasa wakati tunatekeleza hatua za kutatua tatizo la kudumu (kama watafanya....!)
 
JK mkuu, cha kufanya ni kuwaita Wartsila, Ericsson na GE hapo TZ very soon, kuwe na kikao na uwaambie TZ tunahitaji gas powered generators za 300MW kwenye fast track modality, watoe quotes na since hayo makampuni yote ni among the world best, mwenye quote ya bei ya chini ndie apewe hiyo tender ili say in 12 months, tuwe tumemaliza hii issue once and for all.

Mkiwasha IPTL week ijayo ukitokea uharibifu mwingine kwa juhudi za kina Rostam tutakuwa tumerudi palepale.

Hapa tunaweka plaster kwenye tatizo, KATA MZIZI WA FITINA JK watu tumove on na uwekezaji sio tunaact kama huu ni mwaka 1947.
 

Unapo mshangaa JK kwa kutoitisha IPTL kuwashwa mapema una maana gani kuhusu IPTL?

1. ni suluhisho bora

2. Isi suluhisho bora

3. Havina uhusiano wowote
 

Lakini JK amelaumiwa, na hapa hasitahili sifa yoyote. Imesemwa tayari kama Ngeleja ni bomu kwa nini alimchagua? anayesitahili kubeba lawama ya matatizo ya umeme ni yeye JK.
 
Solomon Vipi bana, kwani hujui hawa jamaa hawaoni mbali...zima moto...zima zima...wanapigania 140MW wakati watanzania 88% wako gizani, hili hawaongelei na wala hawalioni, hili ndilo kubwa zaidi.

Kwa hiyo hata alichosema Zitto pia ni zima moto?
 
Lakini JK amelaumiwa, na hapa hasitahili sifa yoyote. Imesemwa tayari kama Ngeleja ni bomu kwa nini alimchagua? anayesitahili kubeba lawama ya matatizo ya umeme ni yeye JK.

Hivi nini maana ya kuwa rais kuwa na wasaidizi????????

Maana kila kitu saa hivi ni JK!
 
Zitto aliongelea kwa solution ya haraka ya kuokoa Taifa na giza na hakusema ndiyo ufumbuzi wa kudumu .Zitto aliuliza kwa nini Nchi iko kwenye giza na mitambo ipo ?

Mkuu Lunyungu,

Kumbuka kuwa Zitto alisema almost the same thing a year ago (hata kabla ya emergence hii kuja). Ili suluhisho la haraka halina time limit?
 
inawezekana ngeleja ni bomu ndio maana kampeleka mtu wake wa karibu kuwa katibu mkuu hapo madini na nishati
 
Lakini bado inabidi tumuulize kwanini tumefikia hapa tulipo?
 
Unapo mshangaa JK kwa kutoitisha IPTL kuwashwa mapema una maana gani kuhusu IPTL?

1. ni suluhisho bora

2. Isi suluhisho bora

3. Havina uhusiano wowote

1, 2, 3 siyo sawa nitachagua number 4, ambayo nina uhakika wewe na sisi tunaijua.
 
Hivi nini maana ya kuwa rais kuwa na wasaidizi????????

Maana kila kitu saa hivi ni JK!

JK anastahili kubeba lawama kwa sababu ya kuangalia sura ya mtu katika uteuzi wake na si uwezo. Vinginevyo tuseme kuwa CCM hakuna anayefaa.
 

Baada ya kusema kuwa hali ya umeme ni kama vita (almost a year baada ya tatizo kuwekwa hadharani), sitakushangaa ukiandika hivi

Zitto said:
Sina swali tena.
 
Mimi nilikuwa wapi muda wote? Naomba urudie swali tafadhali.......

Mkuu nilishakukanya kwamba usipoteze muda na watu kama hao... Wataelewa mbele kwa mbele. Juzi walikuwa wanakupinga hapa leo aibu tupu.
 
Tusubiri utekelezaji wa ile amri/pendekezo lingine la Mh Zitto kuhusu Dowans. Maana yaonekana 'ndo wanazinduka ... waliishiwa ideas.
 
Mkuu nilishakukanya kwamba usipoteze muda na watu kama hao... Wataelewa mbele kwa mbele. Juzi walikuwa wanakupinga hapa leo aibu tupu.

Shapu,

aibu gani unayoiongelea? Eti kwa vile Kikwete amefuata ushauri wa Zitto basi hiyo tu inafanya tamko la zitto liwe mana toka mbinguni.

Kama hataki kupoteza muda na watu kama sisi, atapoteza muda na kina nani? wamiliki wa Dowans?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…