Kaomba kupumzika...kazi ya uDC ina mikiki mingi mno ikilinganishwa na afya yake kwa sasa
u-DC hauna mikiki yoyote, tumeiga mfumo ambao sasa unatughalimu. unajua ma DC waliwekwa ili kurahisisha ukusanyaji kodi ya kichwa baada ya kodi ile kufutwa siioni kazi yao. kwa sababu katika wilaya kuna Diwani(Meya) kuna mkurugenzi wa wilaya, kuna mbunge, kuna watendaji wa vijiji na mitaa kuna wajumbe wa nyumba kumi. Labda niambiwe ni kazi iliyowekwa maalumu kwa ajili ya wanajeshi wakistaafu maana wanastaafu wakiwa vijana sana. vinginevyo nahitaji ushawishi mkubwa ili niwaelewe hawa ma-DC
Nafasi nyingine inayonishangaza ni ya Wakuu wa mikoa pia nao kazi zao ni kama za ma-DC nao hawana kazi ,kazi yao ilikuwa ni ileile ya ukusanyaji kodi sijui kama kuna mtu anaijua kazi yao vizuri basi atujulishe