Kikwete ahaha urais 2010

Luteni,
Jaribu kutumia uwezo wako wa akili kupambanua mada ili uisaidie JF na nchi kwa ujumla. Ukianza kutumikia umbea na uzushi, utatupotezea muda wetu na ubora wa JF.

Ningekushauri ujadili mazito yanayoletwa humu JF kulingana na yaliyomo ndani yake. Kama unafikiri kuna watu wenye ID zaidi ya moja is immaterial kwa sababu huna uwezo wa kuwatambua zaidi ya kuzusha umbea. Kama wanazo, sio jambo baya as long as wanazitumia zote effectively.
 

Mkuu Waberoya
Wala usishituke na maneno hayo, ndio strategy ya chadema kujijenga, kwamba mtu yoyote anayepinga ama ni mnafiki ama ni fisadi. Wala usifikiri ni wanachama wachache ni stategy yao toka juu hadi chini.

Kumbuka Kobouru,Chacha,Zitto,Mzray nk, wamejaribu kutofautiana wakaitwa kila aina ya majina.
hiyo ndo sera yao ya kututoa ktk umasikini.
 
Kinyambis,
You are well reasoned. Huu ushauri tulishautoa siku nyingi kuwa kila mpinzani mwenye umaarufu na uwezo wa kuingia bungeni, ni vema akapigania ubunge badala ya uraisi, kwani nafasi ni mkubwa kushinda ubunge na kupigania mabadiliko kuliko uraisi.

Wakati ule tulipigwa sana mawe tuliokuwa na haya mawazo, lakini hatimaye kimya kimya naona wameyakubali.

Lakini bado nafikiri ni vema watafute mtu anayefaa kuwa mgombea uraisi ili apambane na JK. Lakini ni muhimu awe anaungwa mkono na vyama vyote vikuu vya upinzani hata kama akiwa ni wa mgombea toka CHADEMA, CUF, NCCR n.k.

Upset bado inawezekana kwani CCM chini ya JK ina mabaya mengi ambayo wananchi yamewaudhi sana na inaweza kupigwa mweleka kama kamapeni nzuri zitafanyika.
 

mie nafikiri mtu sahihi wa kupambana na JK ama awe Lowasa ama Magufuli.
 

Mkuu Lekanjobe,
Wa kulaumiwa ni JK na si mwingine. Uraisi TZ unategemea sana uongozi wa raisi mwenyewe na ndio maana kuna tofauti kubwa za utendaji kati ya serikali ya Mkapa na JK ingawa watumishi wengi ni walewale. JK sio kiongozi bali ni mpiga porojo na mbabaishaji na ndio maana mazuri karibu yote aliyoacha Mkapa hayakuendelea na tumerudi nyuma zaidi.

Ni rahisi kuyaona makosa ya mchezaji ilhali wewe ni mtazamaji, ukiingia kucheza wewe mwenyewe utashangaa pengine kuwa mchezaji mbaya zaidi kuliko aliyekuepukia nafasi hiyo. Kwani alipokuwa anatoa ahadi alisema atafanya kama Rais au kama JK?

Mkuu, tusimtetee JK kazi imemshinda. Hakuna mtu anayechaguliwa uraisi halafu akafanya kazi kama yeye binafsi. Nguvu anazopata ni kutokana na wadhifa wake wa uraisi na ndio hapo anapopata uwezo wa kutimiza ahadi zake. Kumbuka JK alikuwa waziri wa serikali mbili zilizopita kwa hiyo hakuna ambalo anaweza akasema hakulifahamu alipokuwa anatoa ahadi.
 
...Tanzania itaona mabadiliko pale tu katiba nzima ikiundwa upya na wajibu wa kila kiongozi na risk zake zikiainishwa bayana. Vinginevyo ni mtindo wa danganya toto milele hadi Yesu atakaporudi tena (soma KIAMA kwa wengine).

Hapa nakubaliana na wewe kabisa. Tunahitaji katiba mpya. Lakini sidhani kama hii itawezekana CCM wakiendelea kuwa na nguvu nyingi kiasi walicho nacho hivi sasa.


Mkuu Leka,
Nakubaliana na wewe kuwa kama hakuna mtu wa kujitolea mhanga, kipindi cha uraisi kitaendelea kubaki miaka 10 (unofficial).

Lakini naamini pia kuwa, hatujawahi kuwa na raisi asiyejua kazi kuliko JK. Mazingira ya kisiasa ni mazuri sana kwa mtu yeyote atakayejitokeza kishujaa na kubwatuka hadharani madhambi yote ya JK na wapambe wake na jinsi walivyoiharibu nchi. Akiweza kuwaelewesha wananchi ni kwa jinsi gani nchi itakavyoporomoka zaidi kama JK akiendelea kutawala, kuna uwezekano mkubwa sana wa kumbwaga JK. He is the weakest and probably the dirtiest president we had ever had, vying for reelection.
 
mie nafikiri mtu sahihi wa kupambana na JK ama awe Lowasa ama Magufuli.
Binafsi sidhani kama Magufuli atagombea na ingawa simjui vizuri, bado sijaona kitu cha maana alichokifanya kwenye miaka yake yote ya uwaziri.

Lowassa nafikiri atagombea kama tete a tete yake na JK itaendelea. Lakini sidhani kama atafika mbali ndani ya CCM. Maadui wake ni wengi mno ingawa ana uwezo mkubwa wa kuongoza ukilinganisha na JK.

Binafsi nisingependa kumuona Lowassa anywhere karibu na ikulu.
 
Kubwajinga,

Ninafurahi sana tunapoongea lugha moja lakini inakuwaje unasahau haya? Kuzungumza na wananchi
 

JK ana wasiwasi gani kama anajua ana rekodi nzuri mbona wenzake kina Mwinyi na Mkapa walikuwa wanajiamini hatukusikia vitu kama hivi mara Amani forum mara Saidia JK ashinde mara kuwanunua wapinzani Mrema na Cheyo type

kumweka Sitta kwenye mtandao maana yake ni kumtoa Lowassa na kumtoa Lowassa ni kupunguza kura maana mtandao wa Lowassa unajulikana ni mkubwa hata kama Lowassa atashiriki na Sitta basi ni kwa vile hana alternative
 

Mkuu,

Hujaona chochotea alichofanya magufuli?plz tell me you are joking!
 
Binafsi nisingependa kumuona Lowassa anywhere karibu na ikulu.

EL ni kiongozi mzuri is an infantrier soldier mfatiliaji tuliona juhudi zake ingawa zilikuwa za muda mfupi lakini at least ali dare alisimamia shule za kata usambazaji wa chakula wakati wa njaa pia usafiri dar aliwaita wawekezaji ofisini kwake kujieleza nk tatizo nidhamu bwana huwezi kuwa na jeshi lisilokuwa na nidhamu vitani askari asiyekuwa na nidhamu hupigwa risasi ya mgongoni na wenzake
 
Mkuu Kubwa, unachosema is 100% correct to the best of the reality. lakini ndugu yangu kama ulivyosema, atakayeweza kujitokeza kishujaa anaweza kumkalisha pembeni. Lakini je, tunaye mtu wa aina hiyo Tanzania ya leo? Watanzania waoga mno. Mtu akitokea CCM hata kuonyesha nia tu, tayari inakuwa shida kwake kwa kuandamwa na kisha wanashusha pumzi na kunyamaza. Inakuwa kama ni uhaini vile kutaka kuwa Rais wakati aliyepo hana jipya kutaka kumchagua tena. Akitokea vyama vya upinzani inakuwa ngumu sana sababu ya mtandao wao ulivyo mfinyu, wanajulikana zaidi mjini wapinzani na sio kijijini. Kama wapinzani wangeweza kuungana na kutoa best mmoja tu akapigiwa debe nchi nzima, najua CCM pasingetosha. Lakini kila mpinzani anadhania kupata uraisi ndio upinzani wenyewe.

Kama wapinzani wangeonyesha ushirikiano kweli wa kuweka mmoja mwenye nguvu katika kila jimbo la uchaguzi pia, wangeongezeka bungeni na Rais angelazimika kushika adabu katika maamuzi yake. Lakini sasa hivi Bunge linatawaliwa na CCM, wapinzani ni tone tu la rangi. Nafurahia sana kusikia kwamba wapinzani sasa hivi wanaelekeza nguvu zao majimboni kuliko ilivyokuwa, kwani vitu hovyohovyo vinaweza kuwa na wakati mgumu kupitishwa pale. Angalia ufungwaji wa Richmond ulivyofanyika, hata wabunge wenyewe hawajaridhika lakini wafanyeje CCM ni wengi na maamuzi yao kwa kura ndiyo final?

Watanzania kama tumerogwa vile, tunaacha mambo yaende yalivyo kwa kuogopa misukosuko, hatujazoea rabsha rabsha. Tunangojea kina Obama kutoka nowhere waitikise dunia, ipo siku itakuja tu. Mfumo wa uchaguzi wenyewe sasa hivi upo biased towards CCM chama tawala. HAta hao CCJ watawekewa vikwazo mpaka wakome ubishi. Umesikia Tendwa na mkakati wake wa kukishighulikia CCJ? Anaona shida kwamba hawa watu walifanya siasa miaka miwili kabla ya kusajili. Ubaya uko wapi? Mnapoanza kukusanyika kajadili namna ya kuunda chama na kupata ushauri hapa na pale si ni siasa hiyo? Kila chama kinapaswa kufanya hayo, mnaweza kupata ushauri kutoka mikoa yote kujua kama hamjakosea ndipo mnasajili ili iwe rasmi. Unapotangaza sasa, tayari wengine walishajua malengo yenu inakuwa rahisi kupata watu 200. Kibaya ni kipi hapo?

Maeneo yote nyeti wakuu wake lazima wawe chini ya uteule wa Mtawala - Msajili, mwenye kigoda cha uchaguzi, majaji, nk. Hawezi kuwaweka watu ambao anajua hawatampendelea. Hiyo ni ubinadamu wa kawaida. Katiba hawataki iandikwe upya kufanana na vyama vingi, bado ina mfumo uleule wa chama kimoja, wanaweka viraka kwa uangalifu sana wasije wakajiharibia. Hata wagombea wa kujitegemea hawataki kwa sababu hata wao kwa wao hawaaminiani, wanahofia wasije wakageukana.
 

Ni kweli kabisa,
Mkubwa mie hapa simwamini yoyote ktk hao akiwemo rais wa sasa kama watabaidirisha uchumi wetu ila-

Siasa za Tanzania na demokrasia ina-umwa ugonjwa wa utapia mlo,,hakuna changamoto yoyote, binafsi naamini kabisa Lowasa ama Magufuli wakijitosa ktk kinyang'anyiro cha 2010 kunaweza leta sura mpya kabisa ktk nyanja ya demokrasia na siasa nchini.

Hapa nikiwa naamana ya kwamba kwa kufanya hivyo ile tabia ya kupea vijiti inaweza toweka kabisa nafikiri hii ndo tunatakiwa kuitafuta kwanza.

Bado naamini tatizo la Tanzania sio kubwa sana na bado nafikiri tatizo lake ni lile la kupeana vijiti hili ndilo tatizo kuu.Na bado naamini ili tupige hatua kutoka tulipo lazima tuvuruge kwanza hii system ya kupeana vijiti, naaminii baada ya hapo tutatembea salama,unajuwa ktk biashara ukiogopa kuchukuwa risk hutofanya biashara kabisa.

Na bado sioni sababu kwanini Lowasa na Magufuli wanaogopa kugombea nafasi hiyo?
 
Mkuu,

Hujaona chochotea alichofanya magufuli?plz tell me you are joking!

Kubwajinga ni mwanamtandao huyo ... kazi yake ni kuua kila mtu ambaye anaweza kuleta upinzani kwa Kikwete. Soma post zake toka mwanzo, akiua ccm, basi anaua wale ambao wangeweza kuleta upinzani kwa Kikwete.

Wanamtandao ndio zao hizo ... waulize Salim na Sumaye watakuambia kilichowakuta.
 

ha ha ha ... hii fiesta ball ya wanachama wa chama cha mafisadi ambayo inaanza kwa waberoya kisha inapitia kwa mkamaP kabla ya kumalizikia kwa kubwajinga imeniacha mbavu zimevunjika zote!
 
ha ha ha ... hii fiesta ball ya wanachama wa chama cha mafisadi ambayo inaanza kwa waberoya kisha inapitia kwa mkamaP kabla ya kumalizikia kwa kubwajinga imeniacha mbavu zimevunjika zote!

Mwambie Mbowe agombee urais ili apate hata hiyo milion 50 ya mgombea wa urais. Maana akibwagwa ubunge ndo kaburi lake kabisa.Urais nachoweza sema kwa uhakika atapata milioni 50 na kura zisizozidi 5%.
 
Mwambie Mbowe agombee urais ili apate hata hiyo milion 50 ya mgombea wa urais. Maana akibwagwa ubunge ndo kaburi lake kabisa.Urais nachoweza sema kwa uhakika atapata milioni 50 na kura zisizozidi 5%.

Mie nilidhani milioni 50 ni moja ya nane ya pesa zilizotolewa na mafisadi papa RA na EL kwenye kampeni ya kumng'oa Mwakyembe kule Kyela ... au kuna unachotaka kueleza zaidi?
 
- Mkuu Mwafrika naona huku unamkoma nyani giladi tena kiroho mbaya sana! I am down!

REspect.

FMEs!
 
Mwambie Mbowe agombee urais ili apate hata hiyo milion 50 ya mgombea wa urais. Maana akibwagwa ubunge ndo kaburi lake kabisa.Urais nachoweza sema kwa uhakika atapata milioni 50 na kura zisizozidi 5%.

Mbowe akitaka kugombea hahitaji hata hizo milioni 50 zenu hazitoshi hata mafuta ya helkopta halafu yale mawazo ya pesa pesa mbele ndiyo yanayokimaliza chama chenu akili yote iko kwenye pesa tu mko tayari hata kuuza nchi midenda ya kina RA EL na wapambe wake wanafikiri pesa ni msingi wa maendeleo jamani imewaingia hata watetezi wao humu sema ukweli usipolipwa mwezi huu utaendelea kuwatetea tuambiane ukweli
 
- Mkuu Mwafrika naona huku unamkoma nyani giladi tena kiroho mbaya sana! I am down!

REspect.

FMEs!

Haa mkulu FMES ... mara moja moja inabidi vijana niwakumbushe nia na madhumuni ya kuingia kwenye hizi forums (toka miaka ile ya times) - ni kumkoma nyani giladi mchana kweupee bila kumwangalia usoni.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…