Hapa nakubaliana na wewe kabisa. Tunahitaji katiba mpya. Lakini sidhani kama hii itawezekana CCM wakiendelea kuwa na nguvu nyingi kiasi walicho nacho hivi sasa.
Mkuu Leka,
Nakubaliana na wewe kuwa kama hakuna mtu wa kujitolea mhanga, kipindi cha uraisi kitaendelea kubaki miaka 10 (unofficial).
Lakini naamini pia kuwa, hatujawahi kuwa na raisi asiyejua kazi kuliko JK. Mazingira ya kisiasa ni mazuri sana kwa mtu yeyote atakayejitokeza kishujaa na kubwatuka hadharani madhambi yote ya JK na wapambe wake na jinsi walivyoiharibu nchi. Akiweza kuwaelewesha wananchi ni kwa jinsi gani nchi itakavyoporomoka zaidi kama JK akiendelea kutawala, kuna uwezekano mkubwa sana wa kumbwaga JK. He is the weakest and probably the dirtiest president we had ever had, vying for reelection.
Mkuu Kubwa, unachosema is 100% correct to the best of the reality. lakini ndugu yangu kama ulivyosema, atakayeweza kujitokeza kishujaa anaweza kumkalisha pembeni. Lakini je, tunaye mtu wa aina hiyo Tanzania ya leo? Watanzania waoga mno. Mtu akitokea CCM hata kuonyesha nia tu, tayari inakuwa shida kwake kwa kuandamwa na kisha wanashusha pumzi na kunyamaza. Inakuwa kama ni uhaini vile kutaka kuwa Rais wakati aliyepo hana jipya kutaka kumchagua tena. Akitokea vyama vya upinzani inakuwa ngumu sana sababu ya mtandao wao ulivyo mfinyu, wanajulikana zaidi mjini wapinzani na sio kijijini. Kama wapinzani wangeweza kuungana na kutoa best mmoja tu akapigiwa debe nchi nzima, najua CCM pasingetosha. Lakini kila mpinzani anadhania kupata uraisi ndio upinzani wenyewe.
Kama wapinzani wangeonyesha ushirikiano kweli wa kuweka mmoja mwenye nguvu katika kila jimbo la uchaguzi pia, wangeongezeka bungeni na Rais angelazimika kushika adabu katika maamuzi yake. Lakini sasa hivi Bunge linatawaliwa na CCM, wapinzani ni tone tu la rangi. Nafurahia sana kusikia kwamba wapinzani sasa hivi wanaelekeza nguvu zao majimboni kuliko ilivyokuwa, kwani vitu hovyohovyo vinaweza kuwa na wakati mgumu kupitishwa pale. Angalia ufungwaji wa Richmond ulivyofanyika, hata wabunge wenyewe hawajaridhika lakini wafanyeje CCM ni wengi na maamuzi yao kwa kura ndiyo final?
Watanzania kama tumerogwa vile, tunaacha mambo yaende yalivyo kwa kuogopa misukosuko, hatujazoea rabsha rabsha. Tunangojea kina Obama kutoka nowhere waitikise dunia, ipo siku itakuja tu. Mfumo wa uchaguzi wenyewe sasa hivi upo biased towards CCM chama tawala. HAta hao CCJ watawekewa vikwazo mpaka wakome ubishi. Umesikia Tendwa na mkakati wake wa kukishighulikia CCJ? Anaona shida kwamba hawa watu walifanya siasa miaka miwili kabla ya kusajili. Ubaya uko wapi? Mnapoanza kukusanyika kajadili namna ya kuunda chama na kupata ushauri hapa na pale si ni siasa hiyo? Kila chama kinapaswa kufanya hayo, mnaweza kupata ushauri kutoka mikoa yote kujua kama hamjakosea ndipo mnasajili ili iwe rasmi. Unapotangaza sasa, tayari wengine walishajua malengo yenu inakuwa rahisi kupata watu 200. Kibaya ni kipi hapo?
Maeneo yote nyeti wakuu wake lazima wawe chini ya uteule wa Mtawala - Msajili, mwenye kigoda cha uchaguzi, majaji, nk. Hawezi kuwaweka watu ambao anajua hawatampendelea. Hiyo ni ubinadamu wa kawaida. Katiba hawataki iandikwe upya kufanana na vyama vingi, bado ina mfumo uleule wa chama kimoja, wanaweka viraka kwa uangalifu sana wasije wakajiharibia. Hata wagombea wa kujitegemea hawataki kwa sababu hata wao kwa wao hawaaminiani, wanahofia wasije wakageukana.