mrefu36
Member
- Aug 16, 2010
- 72
- 22
Mjini Mbozi tukio la mgombea ubunge kuzomewa lilimkumba Dk Lucas Siyame baada ya kuitwa jukwaani na Kikwete ili awasalimie wananchi baada ya kumaliza hotuba yake fupi kutokana na kuwa na mkutano mwingine kwenye mji mdogo wa Vwawa wilayani Mbozi ambao, hata hivyo, uliahirishwa hadi leo asubuhi.
"Sipo peke yangu, jamani nawaombea kura pia madiwani, na mbunge, alisema Kikwete lakini kauli hiyo ilipokewa na kelele za wananchi waliokuwa wakipiga kelele kusema maji, maji, maji, hatutamtaki huyo.
Wananchi hao walipiga mayowe hayo huku wakionyesha ishara ya vidole viwili ambayo ni alama ya Chadema, hali iliyomaanisha kuwa wanamuunga mkono mgombea wa chama hicho cha upinzani.
Upepo wa kisiasa kwenye mji huo haujaikalia vizuri CCM kutokana na hali ilivyojionyesha dhahiri kwenye mkutano huo. Wakati baadhi ya watu walionekana kumkubali Kikwete, wengine walikuwa wakipiga miluzi na baadhi kuonyesha ishara ya vidole viwili.