Kikwete alimtuma Membe kwa Mwl Nyerere, Sehemu ya nne (4)


Hivi JPM Olevel,Alevel,degree,masters,PHD alikua anachomoa kwa makarai tu.
Sababu anapendaga sana kuzungumzia mambo ya masomo yake.

majuzi wakati anamuonea yule mkurugenzi mmarekani kwenye hadhara nilimsikia anamuambia jamaa "UNAJUA NILICHUKUA HESABU"

Nikazidi kuamini kwamba historia ya masomo ya jamaa inashida. yaani anatishia watu kuchukua hesabu.
 
Simulizi nzuri, historia hudumu katika maandishi na si matamshi
 

Jiwe elimu yake ya kuunga unga mpaka kufikia PhD
 
Jiwe elimu yake ya kuunga unga mpaka kufikia PhD
Jiwe anamchukia sana Ali Mufuruki, walisoma wote Lake Secondary alafu Ali akatusua vibaya sana, huku JIWE akiambulia scores za kwenda vocational training.

Sasa badala hata akili zimjie kwamba kumbe kufaulu au kufail masomo hasa haya secondary sio issue jamaa bado anayang'ang'ania, yanamuumiza kwelikweli. Yaani huwa najiuliza haamini kama yeye ndio Rais au nini?

Juzi alikuwa zambia akajifanya kuchomoa kuongea kiingereza, tena akamtolea maneno ya shombo mkalimani anamforce kuzungumza kichewa eti ndio rugha yao wanayoielewa. atafsiri kutoka kiswahili kwenda kichewa.

Dakika mbili hazikupita yeye mwenyewe akachomekea neno la kiingereza kwenye hotuba yake, nikasema iiiishi.
 
Tunapata historia nzuri na adhimu,series ijayo ongeza na kipengele CH Boleni Ngete,jinsi alivyotekwa na kuachiwa,je watekaji walitaka nini kutoka kwake?! Kwa nini walimuachia na hakupotea kama kina Ben Saanane na Azory?!!
 
Mwingine atuletee historia ya mchattle aisee
Nakuja, ila yangu itakuwa ya kujumlisha jumlisha kupata jibu.
Na inaanzia alipogombea ubunge wa Biharamuro 1990 na kugaragazwa kama Samatta kakutana na John Cena.
Stay tuned
 
Mwandishi sio Bernard Membe, ila ni mtu ambaye anamfahamu Membe au walifanyakazi pamoja. Kwasababu angekuwa ni Membe ndio mwandishi basi hizi habari za Monduli ambazo ni kweli, angeziweka vizuri sana na pia kuna mambo ambayo mwandishi hayajui vizuri
Ila hii habari ya Monduli awali tuliletewa hapa JF tofauti.
Ilisemekana kuwa JK akiwa kamisaa wa siasa aliona ufisadi wa mkuu wa chuo kama sikosei Sayore kuhusu tenda ya kuilisha kambi (chuo) nyama na maziwa. Na Brigedia Sayore alikuwa anaogopwa sana. Akaandika barua kwa Amiri jeshi na mwenyekiti/Rais wa TANU.
Mwalimu alipoisoma akampa CDF na kumwambia mkamalize huko kwenu.
CDF akampa mkuu huyo wa chuo barua hiyo.
Jamaa akaisoma kisha akaitoa kopi za kutosha na kuita kikao cha menejimenti ya chuo kuanzia Adjutant hadi wakufunzi, akawauliza kuna tatizo lolote hapa Monduli? Wakajibu (akiwemo JK) hakuna. Baada ya kuuliza Mara kadhaa akagawa copies za barua ya JK nakusema nawapa nusu SAA muisome kisha nikirudi muliambie hii ni nini na akatoka. Kila MTU anamjua Sayore wakaona huo moto atakaorudi nao ni Shetani tuu anajua.
JK akajifanya anaenda toilet, na huko akageuka Kipchoge kuelekea Arusha to DSM na begi la nguo lilimfuata.
Sasa story hii ndio ilikuwa hapa JF na kujadiliwa sana, Leo tunaletewa tofauti. Tupewe ufafanuzi ukweli wa historia ya Monduli ni upi?
 
Membe tuelezee mi napenda stories kama hizi.ni nzuri na sina shida nazo.ILA URAIS SAHAU NDUGU YANGU.SAHAU KABISA MEMBE.HILO HALITATOKEA. ENDELEA KUTUPA STORIES NDUGU YETU MEMBE. MI NAJUA WEWE NI MEMBE NA UNA IDs nyingine 3 humu.
Chukua form wewe tukupigie kura
 
Fursa haichukuliwi bali inatumiwa, syo kesi twende
 

Mkuu kuna watu wamesoma wana madigrii lakini maksi zao za O-Level huwa zinawaumiza mpaka leo hii, huwa zinawakosesha amani.
 
Mzee Meko atakuwa anaufuatilia sana huu uzi, episode after another.

Membe anampa pressure isiyo kifani.
Katunga hadi movie ya kuombwa msamaha lakini Membe kachomoa!
 
I agree with you.

Japo natamani hivi ilivyo ndio iwe kweli sababu nataka sana Membe awe Juu.
 
Kuna mambo mengine ya jeshi huwa hayafai kuyaeleza kwa uwazi sana, ndio maana hata huyu mwandishi amehifadhi jina la huyo mkuu wa kambi. Lakini ukweli unabaki kuwa bila Bernard Membe kueleza kwenye ripoti yake ukweli wa hali halisi ulivyokuwa Bila kupendelea au kumuonea mtu ule ndio ulikuwa mwisho wa JK kisiasa. Lakini kwasababu Membe alifanya kazi yake in a very professional way mwalimu alikubaliana na ile report. Na aliwaita wote Mkuu wa kikosi na JK kila mmoja kwa wakati wake na kuwaeleza what transpired
 
Na baada ya JK kujua, kwasababu mwalimu aliweka wazi, kuwa ripoti ya Membe ndiyo ilimuokoa ilibidi amtafute na kumshukuru. Hata ungekuwa wewe au mimi you could have done the same
 

Vipi kuhusu JK alivyokuwa mwanafunzi pale Monduli alipokimbia kambi na kutembea mguu kwa mguu kutoka jeshini hadi arusha town baada ya kukosana na mkuu wa kambi. Hiki ndo kisa chenyewe au hiki ni kingine tofauti?
 
Nami naongezea tu
JK kumpa uwaziri Membe ilikuwa kulipa fadhila pia kumbeba aje kuwa Rais 2015 ilikuwa bado akilipa fadhila kwa Membe, kwa maana nyingine hii ni rushwa
 
Ukisoma hizi episode kuna mahala utaelewa na kujifunza kitu kihusiana na Mwalimu..

Inaonekana kabisa Mwalimu alijitengenezea mfumo wa kukuza vijana na kuandaa viongozi wa baadaye akijua historia, uzoefu wa kila mtu kutokea chini na hii ilimpa urahisi na umakini kwenye "what next"..

Kwa sasa ni vyema tukatengeneza mfumo wenye mafaili ya kila mtu unaolezea historia ili iwe rahisi kupata viongozi wazuri walioandaliwa na kuivishwa na tuachane kabisa na hii style ya kuajili kupitia UVCCM in critical positions na biashara ya kuokoteza watu na kuwapa majukumu mazito pasipo kuwa na uzoefu nao..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…