Kikwete aliongozwa na CHADEMA, Hayati Magufuli akaongozwa na Kigogo2014; Rais Samia ameanza kuongozwa na CHADEMA, ataweza kuondoka kwenye huu mtego?

Beatrice Kamugisha

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2019
Posts
762
Reaction score
6,984
Wakati wa JK mfumo uliona Rushwa ilivyokithiri ukaona namna Mali za umma zinavyoliwa na watu wachache . Walimwona JK alivyo mwanasiasa mahiri lakini ambaye siyo mwepesi wa kusoMa sana na kwake yeye wasaidizi wake wanaweza wakafanya Kila kitu. Watu walimwona alivyokuwa busy kuzunguka Duniani kutafuta fursa lakini pia kuitangaza Nchi. Watu wa mfumo wakabaini akiondoka anakaimisha ofisi na watu wanapitisha mambo Yao. Wakabaini pia baba kanituma ni wengi n wanadanganya wametumwa kumbe awajatumwa.Zikapigwa zakutosha nyingine kupitia masandarusi; tuliambiwa Bungeni.

Mfumo ukasema huyu mtu adhuiliki, lazima hata kama ataki kusikiliza mfumo unamshauri VIPI lakini uwepo wa wesstle blowers unaweza kumkumbusha na kumwambia anaibiwa. Taarifa zikavujishwa kwenda Kwa akina Zitto, Slaa,Mbowe, Tundu na webgine wengi. Hawa watu Kwa uzalendo mkubwa wakazichakata na kuzipenyeza Bungeni. Spika akashtuka akataka zifanyiwe kazi akiamini wapinzani wanaipaka matope Serikali, Spika akiwa anajiamini hakuna na may be baada ya kumuliza JK nakuambiwa hao ni wapinzani wanatafuta kick akateua kamati za kibunge.

Acha weweee. ...watu wakaenda kupekua majalada nakuibuka na mambo lukuki. Kwa kuwa Mzee wa Msoga hakuwa mtu wa kujitwisha shida za watu ziangaike naye akatoa go ahead spika apokea taarifa na bunge lishauri. Huko ndipo Tanzania ikafahamishwa namna fedha za epa na escrow zilivyoliwa na watu wachache. Waliokula wakapigwa jambajamba wakaona Hali mbaya wakamrudia JK tumekosa Sisi, Mzee wa watu akawasamehe na kujitokeza adharani na kutamka hizo zilizopigwa siyo gfedha za umma. Mission accomplished

Wakati anasema hivyo JPM kimoyomoyo akawa anasali kimoyomoyo akiumia namna watu wanavyokwapua fedha za umma. Akatamani apewe masaa awashuguulikie, mara paap ugomvi ukampa upenyo akapewa bendera....maamaaaaaaa..

Alipoingia ikulu akujipa muda wa kutafakari sana, akatamani yeye awe serikali,Rais,Bunge na Mqhakama nadhani siyo Kwa kupenda Bali alitambua katika mihimili na vyombo anavyosimama hakuna uadilifu na upotoshaji ni mwingi. Akaamua ashike sekta zote atoe maamuzi yeye bila kujali usalama wa maamuzi yake Kwa ustawi wa Taifa.

Hapo ndipo mfumo ukabaini pamoja na mazuri yake tote anatakiwa afungwe speed govonor , wakawaita wazee na kuwaelekeza wamwone Mzee wampunguze speed la sivyo atapeleka Nchi shimoni. JPM akausoma upepo akatamka maneno ambayo yaliwafedheesha wastaafu wote ;alisema " Wapo wastaafu Sijui wazee wana washwawashwa" . Maneno haya yakabebwa na akina Hapi, Makonda na a like wakayabebea bango wazee wakawa wakisema wanaambiwa waache kuwashwa. Nadhani wazee wakaamua kujikalia Kimya wasikose pensheni.

Mfumo nadhani ulipobaini ukipenyeza mambo Yao Kwa upinzani ayatasikika Kwa sababu Nape alishafunga matangazo ya Bunge na vyombo vya habari vipo GIZANI wakamzalisha KIGOGO2014 wa tweeter akawa amejichimbia mizizi kwenye familia ya JPM au Kigogo akawa Moja ya mtu wa karibu wa JPM. Kigogo akaanza kutoa taarifa za mambo ambayo JPM amefanya na anategemea kufanya na taarifa zile zikawa za kweli.

Uwekezaji mkubwa ukafanyika kudukua watu wake wa karibu matokeo yake wakabainika akina nape, Januari ,Mzee makamaba na akina Kinana lakini wao wakabainika wanamdis Mzee akashughulika nao lakini Kigogo akaendelea kutoa za ndani ambazo unaweza kusema zilitoka Kwa wapishi. Mzee akawa anakimbizana huku lakini maovu na njama zake zikawa zinavuja. Kigogo akaenda Hadi Mzee anaondoka Duniani.

Baadaya kuondoka Kigogo akatuambia ipo Vita ya madaraka inafukuta tukadhani uongo Hadi tuliona mama Samia anasafisha nyumba na baada yakumaliza tu kudeki nyumba nadhani akaondoa na Kigogo bila yeye kujua amemwondoa Kigogo. Historia itabaki kumkumbuka Kigogo na mfumo utabaki kupongezwa Kwa KAZI kubwa la sivyo situation ingekuwa mbaya zaidi.

Mama ameingia madarakani anaupiga mwingi lakini Sasa kosa alilofanya nikuruhusu mfumo umwaminishe kwamba wabaya wake ni Chadema. Akaanza nao kumbe masalia ya JPM yapo nyuma yake; ameenda na kesi y Mbowe sasa imefika wakati Kila mtu anajiuliza CCM inanufaikaje na kesi hii? Mkakati huu unalenga kumnufaisha Nani? Kivipi?

Nadhani Sasa mama anapaswa kutambua mfumo unavyojizungusha zungusha kwa nia njema au mbaya. Anapaswa kuufanyia surprise mfumo kama alivyomsambaratisha kigogo bila kufahamu kwamba amemsambaratisha na Sasa taarifa za ikulu zipo salama naatuoni zikivuja.

Yawezekani kuna Jambo analiona kama Mkuu wa nchi lakini alione Kwa angle zote asije akaliona hivi wakati limetegeshwa hivi. JPm aliaminishwa Kigogo ni watu Wapo upinzani na siyo Wana CCM lakini Leo angeamka akajua kwamba mbio za Kigogo zimeishia ukingoni angejutia alivyotumia nguvu kupambana na maadui nje kumbe watoa sirianaambatana nao akiwalipa vizuri.

Vita hizi dawa yake ni haki na chanzo Cha haki ni Katiba.
 
Usijidanganye hakuna kichotokea pasipo sababu huko juu wanajua mambo yao, mengine yanatokea kwasababu yanapaswa yatokee (yanapangwa).

Mengine yanatokea kwasababu ya matokeo fulani,Kuna mambo hata rais hapendi yatokee lkn hujikuta ktk option ya kutokuwa na uchaguzi afanye nini!.. hii ni kutokana na mapokeo ya kiti,unajua kuanzisha kitu na kurithi ni vitu viwili tofauti..?

Narudia na nitaendelea kurudia hakuna system ktk nchi inayotakiwa kuwa imara Kama jeshi/usalama wa taifa,pakiyumba hapa basi kila mahali kumeyumba hawa ndio wanaoweza hata kuonyesha njia papitwe wapi kiusalama zaidi,dira ya nchi ifatwe vipi,nani akae nani asikae,Uhuru wa serikali wa madaraka uende vipi,Hawa wanaweza mkingia kifua kiongozi au wakamtema!,masirahi ya taifa yapigwe au yasipigwe kwa hawa ndo yamelala. Hivyo vyombo vyengine ndo vinafuata na hao maamuzi yao utaona matokeo tu sio kelele kama vyombo vyengine.!

Naamini serikali mahili inaundwa na watu mahili na hao watu kuwapata sio mchezo wa kuigiza au kuwaachia tu kikundi cha watu fulani ndo wawateua viongozi wakuu ni mchakato haswa!.

Huwa sipendi ninaposikia pesa ndefu imepigwa halafu jeshi lipo tu!,huwa sipendi kusikia viongozi wanatamba nje na misingi yao utafikiri tumekosa elite wa elite ktk elite!.

Miradi mikubwa tunasikia inachezewa halafu tunavyombo vya ulinzi!,mi sidhani Kama ulinzi ni kulinda amani pekee naamini ulinzi ni pamoja na kulinda masirahi ya nchi pia.

Kwa hili andiko utaelewa tunakwama wapi na haya unayoyaona ndio matokeo ya kule tunapokwama!. Kuna vitu vya msingi vingekuwa vishapatikana zamani sana kama ndani ya elites kungekuwa na elites wa elites!. Lalamiko la katiba lingekuwa lishaisha, kelele za pesa kupigwa hovyo zamani sana,nidhamu ya hovyo makazini ingekuwa ndoto!,ingekuwa watu wanaishi kwa kufocus ktk malengo na sio kuwaza kutatua shidashida ambazo zingekuwa zishatatuliwa.

Anaewaza kwenda ofisini asiwaze barabarani nitakutana na mabonde ama trafiki aniombe rushwa bali atawaza kazi yangu naifanya kwa ubora upi.
 
Yanayotokea sasa CCM ilishayachungulia kimipango na mkakati 2015!

Ccm ni chama kikubwa!
 
Umesema vizuri sana; day one ya year one ukiwaza kufikiri uchaguzi unaokuja utajikuta unafanya mambo ya kiuchaguzi siyo mambo ya maendeleo ya nchi.

Tanzania mtu anayeweza kusema umeiba ni mwasiasa Tena mkubwa Kwa cheo na akiamka Asubuhi akasema ujaiba inakuwa ujaiba kweli, so tuna vyombo lakini vinasikiliza zaidi kuliko kusikilizwa
 
Imagine, kila siku tutakuwa tunajadili hivi hivi siku inapita tunakula tunarudi kujadili tunalalaπŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€
 
Mpaka masikio yafanyeje ndio anasikia?
 
Mfumo kigogo 2014 walimuua JPM. Sasa wapo na SSH. Ninaamini kuwa huyo wa mwisho anahusika katika assassins squad! au aliisaidia. Kigogo 2014 ni kundi kubwa la mchwa linalotaka system ya ujambazi liendelee na wao wafaidike. Haya hamtaamini leo lakini ukweli ni huo!
 
Yanayotokea sasa CCM ilishayachungulia kimipango na mkakati 2015!

Ccm ni chama kikubwa!

Ni kweli kabisa, ni chama kikubwa lakini sio chama bora. Bado ni chama analogia sana kwenye ulimwengu huu digital, ndio maana matumizi ya nguvu ni makubwa, hila, ushirikina na Majungu.
 
Kigogo ni taasisi?
 
.πŸ‡©πŸ‡ͺπŸ‡©πŸ‡ͺπŸ‡©πŸ‡ͺπŸ‡©πŸ‡ͺπŸ‡©πŸ‡ͺπŸ‡©πŸ‡ͺπŸ‡©πŸ‡ͺπŸ‡©πŸ‡ͺ
GERMANY BIDS FAREWELL TO ANGELA MERKEL_

With six minutes of warm applause, on the streets, balconies, windows, the whole Country applauded for 6 minutes - spectacular example of leadership and defense of humanity, chapeaux !

The Germans elected her to lead them, and she led 80 million Germans for 18 years with competence, skill, dedication and sincerity. She did not utter nonsense. She did not appear in the alleys of Berlin to be photographed. She was dubbed "The Lady of the World" and who was described as the equivalent of six million men.

During these eighteen years of her leadership of the authority in her Country, no transgressions were recorded against her. She did not assign any of her relatives to a government post. She did not claim that she was the maker of glories. She did not get millions in payment, nor did anyone cheer her performance, she did not receive charters and pledges, she did not fight those who preceded her.

Yesterday, Merkel left the party leadership position and handed it over to those after her, and Germany and it's German people are in the best condition ever.

The reaction of the Germans was unprecedented in the history of the Country. The entire population went out to their balconies of their houses and clapped for her spontaneously for 6 continuous minutes. A standing ovation nationwide.

Germany stood as one body bidding farewell to their leader, a chemical physicist who was not tempted by the fashion or the lights and did not buy real estate, cars, yachts and private planes, knowing that she is from former East Germany.

She left her post after leaving Germany at the top. She left and her relatives did not claim advantage. Eighteen years and she never changed her wardrobe. God be upon this silent leader.

At a press conference, a female Journalist asked Merkel : We notice that you're wearing the same suit, don’t you have any other? She replied: "I am a government employee and not a model"

At another press conference, they asked her : Do you have housemaids who clean your house, prepare your meals and so on? Her answer was: "No, I do not have servants and I do not need them. My husband and I do this work at home every day.

Then another journalist asked : Who is washing the clothes, you or your husband? Her answer: "I arrange the clothes, and my husband is the one who operates the washing machine, and it is usually at night, because electricity is available and there is no pressure on it, and the most important thing is to take into the account the possible inconvenience for the neighbours, thankfully the wall separating our apartment from the neighbours is thick. She said to them, "I expected you to ask me about the successes and failures in our work in the government??"

Mrs. Merkel lives in a normal apartment like any other citizen. She lived in this apartment before being elected Chancellor of Germany. She did not leave it and does not own a villa, servants, swimming pools or gardens.

Merkel, the now former Chancellor of Germany, the largest economy in Europe !!

WASWAHILI TUNAWEZA?
 
Una kazi nyingine ya kufanya zaidi ya kuandika mambo hapa JF
 
Kigogo ya tabata ya Chanika au Kigogo cha mwembe.aliyemfundisha chui kula watu ni mwanaadamu. Kusema kweli Kigogo sijamjua bado. Ila mama akaze kishida kweli kweli.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…