Kikwete alivyoondoka Monduli chuo cha Jeshi kwa misukosuko


Unachekesha mno halafu una hoja sana. hufai!
 
Kwa nini hakumjulisha bosi wake Meja Jenerali Natepe? Kwa madai yako kuwa Msuguri pia alihusika mbona hakumshitaki naye kwa Nyerere?
.

Unachoshangaza zaidi ni kwamba, ukipeleka tuhuma za uhalifu kwa IGP anatakiwa kukurudisha kuanzia ngazi za chini ndio protocol au itifaki sio kweli. Mimi ninavyojua IGP atapokea na kuagiza ngazi ya chini kumpa taarifa sahihi juu ya jambo hilo na mara nyingine sio lazima kuwaeleza ngazi za chini chanzo cha taarifa yake ili kumlinda mtoa taarifa. Kwa hiyo, kwa mtoa taarifa yeyote kuruka ngazi za uongozi kunategemea sana jinsi yeye Kikwete alivyokuwa anamwamini Natepe na Msuguri katika suala hilo.
 
Kumbe JK wetu alikuwa MJAMAA kiasi hiki! Nini kilimbadili akawa hivi alivyo sasa?
 
Regardless of there is proof on not but that is how JK behave!! ni m2 wa visasi sana na wivu wa kutosha!! its very disgusting to have a president like this!!!

I see, kuna watu wakali duniani!
 

...kumbe umbea kaanza muda!
 
Nafikiri ni bora tumpindue JK tumuweke matungusha maana kibinadamu yeye hana visasi wala chuki.
 
Hoja yangu hapa ni kuwa......Kwa mfano hata hivi sasa namba ya simu ya Rais kikwete iko wazi kwa wananchi wote na watumishi wote wa umma na serikali kama watafikia kutaka kumpa taarifa yeyote. Leo tukiona Rais kikwete anapokea taarifa isionekane kama kuna mtu hakufuata itifaki au kamshitaki mwingine bali ni jambo la kawaida katika utendaji kazi wenye lengo la kupunguza urasimu kwa kupunguza kufuaata chain of command kwa kila jambo. Hoja hapo isiwe kwa nini kikwete alimpatia nyerere taarifa hiyo bali ukweli wa taarifa hiyo ndio jambo la msingi.
 
Kwa nini hakumjulisha bosi wake Meja Jenerali Natepe? Kwa madai yako kuwa Msuguri pia alihusika mbona hakumshitaki naye kwa Nyerere?

Hoja yangu hapa ni kuwa......Kwa mfano hata hivi sasa namba ya simu ya Rais kikwete iko wazi kwa wananchi wote na watumishi wote wa umma na serikali kama watafikia kutaka kumpa taarifa yeyote. Leo tukiona Rais kikwete anapokea taarifa isionekane kama kuna mtu hakufuata itifaki au kamshitaki mwingine bali ni jambo la kawaida katika utendaji kazi wenye lengo la kupunguza urasimu kwa kupunguza kufuaata chain of command kwa kila jambo. Hoja hapo isiwe kwa nini kikwete alimpatia nyerere taarifa hiyo bali ukweli wa taarifa hiyo ndio jambo la msingi.
 

Unachoshangaza wewe ni kutoelewa kuwa JK alikuwa mtumishi wa CCM wakati huo na sio Jeshi pamoja na kuwa na cheo cha kijeshi.Yeye pengine alimwandikia Nyerere kama Mwenyekiti na sio Rais,naye akamtupia Musuguri kama mwenyekiti wa mkoa wa 'Majeshi' na si kama CDF?(Wewe umechanganya na IGP). CCM hata leo mwanachama wa kawaida hawezi kulianzisha jambo ataambiwa pitia kwenye vikao kwanza. Sasa kipindi hicho cha mid 1980s kulikuwaje? Labda ulikuwa hujazaliwa au hujakuwa. Jikumbushe Kolimba ndugu yangu...ndiyo CCM hiyo!
 
.

Soma vizuri taarifa ya kwanza 'post' iliyoleta mjadala huu hapa inasema wakati huo Msuguri alikuwa mkuu wa majeshi( CDF). Ni yupi mkweli wewe au aliyeleta thread hapa. Wewe unaonekana hata nyumbani kwako ni mrasimu, mtoto akileta mashitaka kwako utamrusha kupeleka kwanza kwa kaka yake, kisha kwa mama yake ndipo akuletee wewe, taarifa za nchi kupinduliwa utaendelea kufuata protocal 'chain of commnd'. Rudi tena kwenye somo la management.....Ndugu acha kukariri mambo ya itifaki. kama umekuja hapa kututoa nje ya mada basi kazi unayo.
 
.

Soma vizuri taarifa ya post iliyoleta mjadala huu inasema wakati huo Msuguri alikuwa mkuu wa majeshi( CDF). Ni yupi mkweli wewe au aliyeleta thread hapa.

Sasa mimi kwani nimekataa kuwa Musuguri hakuwa CDF au wewe hujui historia. Chini ya chama kimoja majeshi yote yalichukuliwa kama 'mkoa' wa 21 wa CCM na kuwa na uongozi wake kama mikoa mingine CDF alikuwa Mwenyekiti wa mkoa na Natepe alikuwa katibu wa mkoa....na nilikuwepo sijasimuliwa
 
Mkwere ni mzee wa fitina kweli kweli, na Rizwani amerithi fitina za babake, kumbuka yaliyomkuta Masauni, ama kweli like father like son.

MIMI NAKUMBUKA YALIYOMKUTA KIFUKWE.......ETI WATU WANAOSHINDA BAKURUTU HAWANA NAFASI YANGA....PIA NAKUMBUKA SANA UFIRAUNI ALIOUFANYA BIG-BOSS KWA KUDANGANYA KUWA BASHE SI RAIA ili apate tu kumng'oa kwenye kura za maoni.
 
Ungeniaminisha haya majungu 2005, leo ni kupoteza mda bila tija.Wala sitaki kuamini maana nikiamini itachukua memory ktk nvram ya kichwa yangu bure.

Mkuu unaonyesha kichwa yako inamemory ndogo sana mpaka unakwenda kwa budget.
Naweza amini story kwa kuwa kuna mifano mingi ya Mkwere ambayo inaonyesha jamaa hakuanza fitna leo wala jana.
Yupo wapi Steven Mashishanga nenda kamuone morogoro mzee alivyochoka kwa kumsupport Sumaye wapi Philip Mangula katibu mkuu CCm kipindi cha mkapa hakumsupport JK sasa anaendesha baloon lililochoka Iringa, na wengi wa wanazuoni wanasema katika kosa alilofanya Mkwere CCM ni kumpiga chini Mangula mtu aliyeweza kudumisha nidhamu chamani.

Fuatilia stori ya Professa Mahalu na kesi yake ya ubadhirifu wa pesa kule ubalozini Italia na safari ya Kikwete Italy pindi Mahalu akiwa balozi na baada ya kikwete kurudi kesi ikashonwa ili kumkomoa Mahalu. so binafsi naweza amini kwani inaendana na visasi na fitna nyingi, ikumbukwe Kikwete alikuwa mkufunzi so maya be alidhani anaweza pandishwa cheo but hakufuata Military Chain of Command
 
Kwani yeye JK alijaribu kulima huo mchicha na kuiuzia kambi na akazuiwa? Au ndio uvivu wenyewe wa kikwere,jembe halishikiki?

Kwi kwi kwi. Duh! Sasa na yeye angelima na kuliuzia jeshi matembele si angekuwa anashindana na wakubwa wake jeshini? Mgongano wa kimaslahi.


Ndugu mtoa hoja,
Kama umesoma vema hoja za hapa, kuna watetezi wa JK na wale wanaounga mkono madongo kwa JK kwa ushahidi wa kimazingira. Please read carefully kabla hujatoa hitimisho la namna hiyo!
Mie sitetei ubaya, ila ukitaka kujua JK ni mtu wa namna gani, jaribu kifikiri kwa akili ya kawaida kabisa (ukichanganya na ya wenzako) kile alichokishabikia kuhusu uraia wa Hussein Bashe. Kama baba mwenye nyumba (Mwenyekiti wa Chama) hakutakiwa kumhukumu Bashe bila kungoja ushahidi wa kitaalamu kutoka kwa Idara ya Uhamiaji kuhusu uraia wa Bashe. Hata kama thread hiini ya uongo kuhusu JK, lakini ukiangalia namna alivyolishughulikia auala la Bashe basi iunaweza kuhitimisha kwamba majungu ni tabia yake.
Kama ushahidi huu wa kimazingira hautoshi, basi tuanze kujadili suala la Francis Kifukwe wa Yanga na majungu yaliyomzunguka.
 

JF Ni burdani kwelikweli.

Ina maana kama wasingekuwepo watu wanaofitiniwa, walala hoi tungekuwa na mzigo mzito wa kuwabeba watu ili waendelee kuishi maisha laini.

Hapo kwenye bold natamani kama idadi ya wafitiniwa ingeongezeka maana kwa sasa hivi watu wengi mno wanaishi na kuvuna pale ambapo hawastahili, wanabebwa kwa vile wako kwenye vitabu vizuri vya wenye mamlaka.
 
Heshima kwenu wanajamvi,

Kwanza naomba nimpongeze mleta thread Mzizi wa Mbuyu.

Kuna baadhi ya matukio yanayoondoa uwezekano wa habari yenyewe kuwa kweli au labda muanzisha thread kashindwa kuniaminisha kutokana na mtiririko wa hoja na matukio.

[1] Lt Gen Gideon Sayore kuuza bidhaa alizozalisha mwenyewe kwenye chuo anachokiongoza ni ukiukwaji mkubwa wa taratibu na kanuni za manunuzi ambazo zilikuwepo wakati huo.Ebu fikiria mkuu wa chuo analeta chuoni maziwa yaliyotiwa maji afisa anayepokea ana cheo cha Captain ataweza kuhoji ubora wa maziwa ya mkuu wake wa kazi mwenye cheo cha Brigadia ?.

[2] Major Kikwete kuandika barua kwa Amiri jeshi mkuu ni utovu wa nidhamu wa hali ya juu.Kwanini hakuipeleka barua kwa mkuu wa utawala jeshini ?,au kwa mkuu wa majeshi ?.Alipaswa kufahamu kwamba Rais ambaye pia ni amiri jeshi mkuu hakupaswa kupelekewa issues ndogo kiasi hicho.

[3] Ni makosa makubwa mwanajeshi kutoroka jeshi.Sipendi kuamini Kikwete aliondoka Monduli kwa staili ya mleta mada anavyotaka kutuaminisha.Yawezekana kweli ulikuwepo mtafaruku wa kuchongeana lakini akili yangu inaniambia jambo hilo lilishughulikiwa kivingine kabisa na pengine ndiyo maana Kikwete aliteremshwa cheo hadi ukatibu wa wilaya [graduate wa wakati wake halikuwa jambo dogo].

[4] Mwl Nyerere kama ni kweli aliandikiwa barua na Major Kikwete akaamua kuiteremsha kwa mkuu wa majeshi General Musuguru pengine hakutaka ishughulikiwe namna ilivyoshughulikiwa,yamkini alitaka Gen Musuguru alichunguze suala lenyewe ili kubaini ukweli wenyewe.Gen Musuguru alikuwa na uwanja mkubwa wa kumshulikia mkosaji lakini kwa mshangao aliamua kumpa barua mkosaji badala ya kumchunguza mtuhumiwa.Sioni kosa la Mwl Nyerere alieamua kufuata itifaki ya kijeshi.
 

Mzee Edgar Maokola-Majogo...kama sio kuwa karibu sana na Mkapa naye angeipata fresh...yeye ndie aliyekabidhiwa JK baada ya kutoka Monduli kule Lindi...akampeleka Nachingwea (Farm 17 kwa mnaokumbuka JKT) badala ya kukaa town...alimchukia vilivyo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…