Kikwete alivyoondoka Monduli chuo cha Jeshi kwa misukosuko

Jakaya Ana Historia ya kusisimua kuliko Mwanasiasa yoyote hapa Nchini!

Mabonde na Milima yake ya Kisiasa akiamua kuandika bila ya kuficha kitu huenda Kitabu chake kitakuwa reference Muhimu kwa Siasa za ukanda wetu lakin Tatizo la Yule Mkwere ni Mzuri sana wa kuzungumza sio kuandika [emoji12][emoji12]
 
Mkwere alichukia Maofisa Cadet kufanyishwa kazi za kusafisha mabanda ya kuku na nguruwe, wengine wakiwa waislam.
JK kwa fitina noma!!
 
Mkuu upo?
Habari ATown.
Manyara ni poa.
 
That is where the difference is...aandike tena aandike ukweli mtupu ili vizazi vyetu vijifunze. Wanaoandika ni wachache sana kama Yule kijana anayeandika harakati za wanaofukuzwa chuo kwa utukutu
 
Penye riziki hapakosi fitina. Fitina ni moja ya mbinu za maisha. Ila usizidishe.
 
Very interesting kwa kweli!
 
Kama umezaliwa miaka ya 90 utajuaje unaona miaka ya 70 na 80 kama zamani sana, kopi zilikuwa zinatolewa tangu enzi za uhuru tulikuwa tunatumia carbon paper najua huzijui, nyie watoto wa enzi za photocopy na scanner.
Hawa vijana hata ukiwaambia enzi hzo sisi tunafanya mitihani inaandikwa ubaoni na chaki na kama ubao mdogo mwalimu anasubiri mmalize anafuta tena na tena au ukikuta mwl mwandiko wake wa kitaalamu anabananisha mtihani wote ubaoni. Sidhani kama wataamini
 
Naona mambo ya siasa tushazungumza sana.

Ngoja niingize human touch, light touch story. Memoirs of Al-Watan.

Hii story ilivyomtaja General Sayore imenikumbusha Nancy Sayore enzi za ujana wangu.

Katika pitapita zangu nikawa nakatiza Namanga,mara nikapita Kimicho, watoto wa Oysterbay wanakutana wanakula Ice Cream na mapochopocho, mimi nakatiza tu kuangalia vitu madukani.

Mara namuona Nancy anatoka Kimicho. Wakati huo ndo scandal yao ya email na Heri "DJ Red" Bomani ndo kwanza imetokea. Vijana waliokuwa wanafuatilia mambo ya Dar miakaya mwisho ya tisini watakumbuka.

Mimi Nancy alikuwa kama kichaa wangu kwa sababu kuna mshkaji alipumzika. Ndipo nilipojua kwamba yule mtoto kwa nje anaonekana mpole lakini kichaa kama baba yake. Mimi nilikuwa jioni kisomo flani siku hizo nashika time zangu kwa hiyo sikuwa na mazoea naye sana, ila siku hiyo nilipomuona nikawa namsalimia "Mambo vipi Nancy?" Basi namuona mtoto wa kike anajiumauma, akasema "Poa tu, vipi wewe?". Nikamwambia poa tu.

Yeye anajua kwamba mimi najua scandal yake. Na mimi najua yeye anajua. Ila ikawa kama kuna an wakward moment.

Basi nikaamua kumpoza. Nikamwambia Nancy najua uko katika wakati mgumu sasa, ila wewe usijali sana watu wanavyosema, wewe focus kwenye mambo yako tu, tunaokujali na kukujua hatuwezi kupoteza urafiki wako kwa sababu ya wabongo kukuvunjia faragha yako.

Akafurahi sana akasema "You are so kind, that is the nicest thing I have heard". Akacheka sana.

Na mimi nikafurahi kumtuliza roho baada ya kuona alivyofadhaika.

Basi nikwa namuaga nishike hamsini zangu.

Na yeye akaniaga.

Kuangalia pembeni nikaona Nissan Patrol. Limefungwa vioo.

Halafu ndani kakaa General Sayore kumbe mda wote namchombeza Nancy mshua ananiangalia tu.

Nikasema du, sasa pale ningekuwa na tabia za maneno mbovumbovu kumsema vibaya binti huku sijajua Mzee Mzima ananiangalia sijui ingekuwaje.

Nikajifunza kwamba kuwa na kauli njema ni jambo zuri sana.
 
Na ile ya waitara?aligoma kwenda kumpigia saluti kikwete.
 
Kumbe maneno yote kuna nukta muhimu ya UDINI ndani yake ee... Haya endeleeni lakini kumbukeni mtavuna mlichopanda.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…