Kikwete alivyoondoka Monduli chuo cha Jeshi kwa misukosuko

Huwezi kuwa mkuu wa chuo kisha uchukue tenda ya kukiuzia chuo ni ufisadi.
Nyerere aliogopa wajeshi maana walishajaribu kumpiga chini zaidi ya maramoja kipindi mambo yalipozidi kuwa hovyo nchini ndo maana kuna kipindi alikua anawekaweka watu kizuizini.enzi hizo jk ndo vijana waliokuwa wajamaa halisi asingefumbia macho ufisadi huo.leo humu ufisadi huo wa sayore mwausifu na kuupinga wa dowans ni yaleyale sayore alijipa mwenyewe kandalasi bora product zake angetafutia soko pengine
 

Hawa jamaa walikuwa noma..! Sayore nae alipokuwa Chief of Staff nasikia kuna jamaa mmoja toka Zenj alikuwa mchawi kishenzi na anatumia vitisho vya uchawi kulazimisha kupandishwa vyeo. Sasa Sayore habari ikamfikia akaitisha jamaa aitwe aje Dar ofisini kwake ASAP. Jamaa alipoingia ofisini akakuta Sayore amesimama kashika kifimbo chake mkononi, ikabidi nae abaki amesimama. Sayore akavua kofia akaweka mezani, jamaa nae ikabidi afanye hivyo hivyo........! Then Sayore akamuuliza wewe ni fulani, jamaa akajibu ndio afande. Sayore akawa anapiga piga ile fimbo mkononi huku anamzunguka yule jamaa na kumwangalia. Then Sayore akamuuliza nasikia wewe ni mchawi sana, jamaa akajibu ndio afande........basi Sayore akampa fimbo ya kichwa. Akamuuliza tena nasikia wewe ni mchawi sana, jamaa akajibu ndio afande.......akapewa zingine mfululizo za kichwa. Sayore akamuuliza unaweza kuloga jeshi zima weye, jamaa akajibu hapana afande.....basi akaamuru jamaa arudishwe Zenj na achukuliwe hatua zaidi za kinidhamu
 
It's a true story!!
Na tangu JK amekuwa Rais, amekuwa akimuomba sana Mzee Sayore awe Balozi wetu nje, lakini Sayore amekuwa akimkatalia kwa kusema "siwezi kuwa nafanya kazi na kuripoti kwa watoto wasioijua nchi"!

Ni kweli, hii aliisema mwenyewe JK kwenye hotuba zake kwamba kuna mtu alimkatalia uteuzi wake kwamba hawezi kufanya kazi chini yake. Hakumtaja mzee Sayore lakini.
 
Maweeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee, tehtehteheteghetegheteheteeee yoooooooooooo chonka inyweeeeee yoyoyo mwanyita, i mean mmeniuaaaaaaaaaaaaaaa loh hii kali,
 

Kama kuna sababu zilizomfanya Kikwete kuamini kwamba level za chini Jeshini haziwezi kumuwajibisha Sayore, alikuwa justified kwenda kwa Amiri Jeshi Mkuu.

Huwezi kusema corruption jeshini, tena inayoweza kuleta mgawanyiko kati ya maafisa wa jeshi katika chuo kikubwa cha jeshi, ni kitu trivial.

Kikwete was right, and he can even argue that incidents like this proved really discouraging to his reforming zeal. Even if some Machiavellian intrigues were involved.
 

Kula tano.

Hebu tuache double standards hapa. Huwezi kumshutumu Rostam halafu ukamshabikia Sayore, wote mafisadi tu.
 
General Musuguri alikuwa anajua kusoma japokuwa alikuwa naongea lafudhi ya Kimsoma!
 
Kitu ambacho wachangiaji wengi wamekisahau ni kwamba wakati wa mfumo wa chama kimoja kuna wanajeshi walikuwa jeshini kwa ajili ya kulinda maslahi ya chama. Na hawa wengi waliingia toka kwenye uongozi wa chama baada ya jaribio la kuipindua serikali ya Nyerere lililofanywa na jeshi. Kikwete alikuwa ni miongoni mwa wanajeshi wanaolinda maslahi ya Chama.

Kikwete anaweza kumuandikia Nyerere kama Amiri jeshi mkuu, Rais wa nchi au mwenyekiti wa chama. Kama kweli barua hiyo ipo, ingewekwa hapa ionekane Nyerere aliandikiwa kwa nafasi ipi na kada huyo mwanajeshi? Otherwise uchambuzi hauwezi kuwa kamilifu.

Hata hivyo, maelezo aliyotoa mtoa mada yanaonyesha udhaifu mkubwa wa Nyerere. Nilitegemea Nyerere kama mwalimu ategemee kuwa vijana wake (kina Kikwete) hawawezi kuwa perfect na anapoona wanakosea afanye jitihada za kuwafundisha. Katika habari hii haionekani kama Nyerere kama mwenyekiti wa chama alifanya jitihada zozote za kumfundisha kada wake aliyemtuma jeshini kufundisha wanajeshi siasa.

Mtoa mada pia anamdhalilisha Rais Mkapa kwa kuonyesha kuwa Kikwete ni mdini na alikuwa mdini tangu enzi hizo. Kwa kusema hivyo anafanya watanzania wajiulize ilikuwaje Rais Mkapa ashindwe kujua kuwa Kikwete ni mdini hata akamuachia apewe fursa ya kugombea urais kwa tiketi ya CCM. Tukumbuke kuwa majina ya wagombea urais katika kura za maoni CCM mwaka 2005 yalikuwa 10. Tulitegemea Mkapa kama mwenyeti wa chama na Rais ahakikishe jina la mdini Kikwete lisipitishwe hata hatua ya awali.
 
Shida ya Mkapa ni kwamba hakuweza kufanya uamuzi wa busara dhidi ya Kikwete kwa sababu alishakuwa "compromised." Ufisadi kitu kibaya sana.
 
JK ni mtu wa visasi kwa hiyo hili halinishangazi hata kidogo....................................na JK humkuza sana Kawawa kwa kumbeba bila ya kujua hata kawawa alikuwa kwenye mbeleko za Nyerere.....................................

Una uhakika Kawawa alikuwa kwenye mbeleko za Nyerere ...... nani aliyekuwa mkuu wa vyama vya wafanyakazi?
 
kIPINDI HICHO KULIKUWA NA FOTOKOPI MASHINE KWELI?
Zilikuwepo. Maana zilikuwepo nchini tokea miaka ya mwanzo kabisa ya sabini kabla Kikwete hajaingia Jeshi. Kwa vile kuna uwezekano zilikuwepo CTU (Chuo cha Taifa cha Uongozi) au NLA (National Leadership Academy) kama ilivyokuwa ikijulikana wakati huo. Ingawa sina uhakika na stori hii.
 
Kama kuna sababu zilizomfanya Kikwete kuamini kwamba level za chini Jeshini haziwezi kumuwajibisha Sayore, alikuwa justified kwenda kwa Amiri Jeshi Mkuu.

nope hakuna kitu kama hicho mkuu, jeshi siyo kama kampuni ambapo ukiona meneja wako hakusikiliza unaweza kwenda hata kwa CEO. Jeshi linaongozwa kwa chain of command na hadi hivi sasa hakuna mahali popote ambapo unaweza kutafuta ambapo panasema JK aliamini kuwa "level za chini haziwezi kumwajibisha Sayore". Hakuna - labda kama una infer tu kuwa kwa vile kaenda kwa Amiri jeshi mkuu.. tukikubali hivyo, Amiri Jeshi Mkuu attakuwa na kazi nyingi kweli kwani ukiondoa JWTZ kuna Polisi, Magereza, JKT na kila afisa ambaye hatoridhika na his immediate commanding officer basi akimbilie Ikulu. Hii ni hatari for unity and discipline ya jeshi.

Hoja ya Sayore kuwa fisadi inaweza kukubalika kabisa lakini kumlaumu Nyerere.. thats extremely overreaching..
 

Duh.. sasa historia mnaiandika upya; hivi mnajua ni lini siasa ilianza kuingizwa jeshini? Na kama unazungumzia Army Mutiny ya 1964 haikuwa jaribio la kumpindua Nyerere!

Kikwete anaweza kumuandikia Nyerere kama Amiri jeshi mkuu, Rais wa nchi au mwenyekiti wa chama. Kama kweli barua hiyo ipo, ingewekwa hapa ionekane Nyerere aliandikiwa kwa nafasi ipi na kada huyo mwanajeshi? Otherwise uchambuzi hauwezi kuwa kamilifu.

Mtu yeyote anaweza kumuandikia Rais barua yoyote, hata mtu wa kijijini akitaka. Lakini linapokuja suala lenye kuhusisha taratibu za kijeshi na mnyororo wa madaraka ni jambo linalohitaji upekee wa aina yake wa kufanya mtu aruke maafisa wake wote na kwenda kwa amiri jeshi. Kwanza, kutokana suala lenyewe kuwa ni la kisiasa, CCM ilikuwa na kamati za usalama za chama na kulikuwa na utaratibu wa kushughulikia malalamiko kabla ya kufika ngazi za juu. Hadi hivi sasa hakuna mtu aliyetuonesha (kama story yenyewe ni ya kweli) kuwa JK alijaribu kutumia njia za kawaida kupeleka malalamiko yake na hakusikilizwa.


Aah wapi.. Nyerere angesimamia vijana wangapi kila ambapo hawafundushiki. Maana tukikubali hilo itabidi tumlaumu Kikwete kwa kila uzembe unaofanywa na watu walio chini yake! huu si uongozi. Nyerere anaonekana makini kabisa kwa kurudisha suala hili kwa vyombvo husika kwani angetengeneza mazoea mabaya sana; kuwa kila mtu akigongana na afisa wa juu yake anakimbilia Ikulu. Nyerere aliweka standard, siku hizi hiyo standard haipo kabisa. Kanuni hii kwa wanaomfahamu Nyerere wanajua kabisa aliitumia mara nyingi sana. Hakupenda kile kinachoitwa "majungu"..
 
[

kumbe jamaa huyu alianza unafiki longtime, ndo maana hawezi kuongoza!!!!!!!!!!!!!!!
 

Kama ni kweli, je ni halali kwa mkuu huyo wa majeshi kujipa tenda kuuza hapo hapo chuoni? kwanza yalikuwa kinyume na AZIMIO LA ARUSHA.Kakitabu alikokuwa anatembea nako mwalimi kama ka kitabu ka muongozo wa nchi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…