Wakuu, Inawezekana inabidi tuchambue nguvu alizonazo JK katika nafasi yake ya Uenyekiti wa AU ili tujue kama kwelia ana nguvu za kutosha kufanya maamuzi yake binafsi kama ambavyo tunataka afanye, mathalan, kumshutumu Bob nk.
Kwa wale mliobobea juu ya ufanyaji kazi wa taasisi kama AU, kabla ya JK kuukandia uchanguzi wa Zim, maana ndiyo lingekuwa tamko rasmi la AU, yenye member 53 wenye mtazamo tofauti juu ya suala hili, angefanyaje?
Nini nguvu za Commission ya AU? Je, kuupinga tu (labda kwa maneno matupu) uchaguzi ule kungesaidia nini iwapo 53 members hawako kwenye uamuzi wa namna hiyo? Je JK angekuwa anawakilisha Tanzania pale alipotamka hivyo, au anawakilisha AU?
Sina hakika nini hasa kinatokea, lakini maswali haya yanaweza kutusaidia kutoa strong arguments za what should have been said or not said by JK in that regard.
Mimi naona maneno yake yako very precarious, obstensibly knowing that the divided continent and the world are closely watching his steps. Karibuni.