Huo utakuwa ni upumbavu na si ujinga. Kwani watakuwa wanajikomba tu wakidhani atawafaa huko mbeleni. Je, ni nani asiyejua jinsi wengi wa wafanyakazi wa sekta ya umma jinsi wanavyopata SHIDA na MATESO nchi hii? Hivi kweli mshahara wa shs 260,000= alizoongeza kinyemela ndo ziwafanye sasa wampe kura?
Wampe wasimpe ukweli utabaki kama hivi:
- Alisema hazitaki kura zao. Ushahidi tunao kwenye DVD na video camera majumbani mwetu.
- Jaribuni kumpa halafu muone inflation na devaluation zitakavyokuwa kwa kipindi cha 2010 - 2015.
- Matatizo yatakayo kuja baada ya hapo hayatachagua wala kuangalia wewe ni wa-Chama gani.
- Wakupongezwa ni Bwana Mgaya na Dr. Slaa, kwani ndo waliomtia kiwewe JK hadi akaongeza mshahara kinyemela na kuanza kuropoka ovyo eti hakusema..."HAZITAKI KURA ZA WAFANYAKAZI"
- JK, ni mnafiki alidai haongezi mshahara hata wakigoma miaka 8. Je, nini kimemfanya aongeze hela kimya kimya? ni nini hicho?