Elections 2010 Kikwete anatuchezea akili...

Elections 2010 Kikwete anatuchezea akili...

Kiranja Mkuu

JF-Expert Member
Joined
Feb 18, 2010
Posts
4,219
Reaction score
4,608
Kitendo cha yeye kusema kuwa hakuzikataa kura za wafanyakazi ni sawa na kutuona tusio na ufahamu.
Hotuba yake aliyoitoa akihutubia wazee wa CCM wa DSM tunayo.

HATUDANGANYIKI NG'O!!!!
 
WAMESEMAA HAWADANGANYIKI, na ndio maana kila anapokwenda anawaomba radhi watumishi hao kimtindo, hawadanganyiki.
 
Wafanyakazi sehemu nyingi wameapa watampa JK kura, wengine wanadai ni wana CCM lakini JK hawatampa kwa kudharau kura zao.
 
tukutane 03/11/2010 utakanyokuwa unahema mpaka kichwa kinataka kupasuka utakaposikia SLAA CHALIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIII

Kwa tume ya uchaguzi tuliyonayo hilo halishindikani I agree with you 150%
 
Tatizo wafanyakazi wengi hawana ufahamu wa elimu ya uraia. Wengi wao wakienda kwenye kampeni za CCM na kusikiliza TOT wanachanganyikiwa. Ebu jiulize uke umati wa Jangwani ulitoka wapi kama sio wafayakazi. Siamini kabisa tabaka la wafanyakazi. Hawana msimamo. Afadhali machinga na madreva na kondakta wa daladala. Hawa wakishikilia jambo wana msimamo lakini wafanyakazi wanayumbishwa sana. Kwanza ndio watatumiwa kuiba kura kwa ajili ya CCM.
 
anaomba radhi na kura wanampa

wangekuwa wanampa angekuwa anaweweseka kama jana ..eti ooooh sikusema hivi..kama yeye kidume aseme ndiyo sizitaki kura zenu..
 
Wafanyakazi sehemu nyingi wameapa watampa JK kura, wengine wanadai ni wana CCM lakini JK hawatampa kwa kudharau kura zao.

Huo utakuwa ni upumbavu na si ujinga. Kwani watakuwa wanajikomba tu wakidhani atawafaa huko mbeleni. Je, ni nani asiyejua jinsi wengi wa wafanyakazi wa sekta ya umma jinsi wanavyopata SHIDA na MATESO nchi hii? Hivi kweli mshahara wa shs 260,000= alizoongeza kinyemela ndo ziwafanye sasa wampe kura?

Wampe wasimpe ukweli utabaki kama hivi:
  • Alisema hazitaki kura zao. Ushahidi tunao kwenye DVD na video camera majumbani mwetu.
  • Jaribuni kumpa halafu muone inflation na devaluation zitakavyokuwa kwa kipindi cha 2010 - 2015.
  • Matatizo yatakayo kuja baada ya hapo hayatachagua wala kuangalia wewe ni wa-Chama gani.
  • Wakupongezwa ni Bwana Mgaya na Dr. Slaa, kwani ndo waliomtia kiwewe JK hadi akaongeza mshahara kinyemela na kuanza kuropoka ovyo eti hakusema..."HAZITAKI KURA ZA WAFANYAKAZI"
  • JK, ni mnafiki alidai haongezi mshahara hata wakigoma miaka 8. Je, nini kimemfanya aongeze hela kimya kimya? ni nini hicho?
 
Mkuu heko, nimeupenda mchango! watu ni wepesi kusahau kuwa hawa jamaa wanataka kura ili waendelee kunyonya watu.
Ukweli ni kwamba CCM hawana ubunifu wa kututoa hapa tulipo kwenda sehemu ambayo tutawakumbuka milele. Inshu kama ya kutaka kuacha kutegemea misaada kwenye bajeti, kuacha kuachia soko holela, mfuko wa bei, huduma za jamii (bara bara, elimu, hospitali, maji, umeme nk) ni vitu ambavyo vinatakiwa viwekwe katika mazingira ya ICU ya ikulu ili vifuatiliwe haraka na kuboreshwa ndani ya miaka mitano. Mambo haya yanawezekana kama tutaweza kuchukua shilingi kwa kila mfanyabiashara, muingiza bidhaa nchini toka nje ya nchi, tutatengeneza business centre kama Machinga Complex za kutosha kila mkoa.

Mambo ni mengi. lakini kama viongozi wetu watawajibisha watu, watu wataacha kukimbilia kuwa viongozi bali kufanya kazi za kawaida. Lakini saizi ni kinyume, kila mtu anataka kuwa kiongozi, wanabaki kupiga soga bila kufanya kazi, wanategemea misheni town, ndo kuhujumu nchi hivyo.
 
kama hazihitaji...tatizo lake nini...tutampgia mwingine unless asimame na ku-negate maneno yake ya Dar
 
Huo utakuwa ni upumbavu na si ujinga. Kwani watakuwa wanajikomba tu wakidhani atawafaa huko mbeleni. Je, ni nani asiyejua jinsi wengi wa wafanyakazi wa sekta ya umma jinsi wanavyopata SHIDA na MATESO nchi hii? Hivi kweli mshahara wa shs 260,000= alizoongeza kinyemela ndo ziwafanye sasa wampe kura?

Wampe wasimpe ukweli utabaki kama hivi:
  • Alisema hazitaki kura zao. Ushahidi tunao kwenye DVD na video camera majumbani mwetu.
  • Jaribuni kumpa halafu muone inflation na devaluation zitakavyokuwa kwa kipindi cha 2010 - 2015.
  • Matatizo yatakayo kuja baada ya hapo hayatachagua wala kuangalia wewe ni wa-Chama gani.
  • Wakupongezwa ni Bwana Mgaya na Dr. Slaa, kwani ndo waliomtia kiwewe JK hadi akaongeza mshahara kinyemela na kuanza kuropoka ovyo eti hakusema..."HAZITAKI KURA ZA WAFANYAKAZI"
  • JK, ni mnafiki alidai haongezi mshahara hata wakigoma miaka 8. Je, nini kimemfanya aongeze hela kimya kimya? ni nini hicho?
Kwa taarifa yako TRA wanasema kwamba hawatambui hicho kima cha chini cha msahara wa Tshs 260,000/= bali Tshs 135,000/=. Hivyo wafanyakazi wameuziwa mbuzi kwenye gunia.
 
J.K aendeleza usanii kwa wafanyakazi
Kwa taarifa yako TRA wanasema kwamba hawatambui hicho kima cha chini cha msahara wa Tshs 260,000/= bali Tshs 135,000/=. Hivyo wafanyakazi wameuziwa mbuzi kwenye gunia.
 
we sie mfanyakazi bana.! we mtu wa bizness waache wafanyakazi waongee wakate kiu yao kwani tatizo li wapi subirini wakati ufike kura zipigwe matokeo yatolewe ndipo mtajua nani ni nani ,kipindi cha kampeni watu mnachanganyikiwa kabisa.!
tulizeni mizuka fanyeni maisha taratibu.
 
tukutane 03/11/2010 utakanyokuwa unahema mpaka kichwa kinataka kupasuka utakaposikia SLAA CHALIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIII

Sasa wewe Jeykey nakuona mtu wa ajabu kabisa! Mara nyingi nikisoma kwenye mabandiko yako, huna hoja bali unaonesha ushabiki wako wa kimdundiko (a blind supporter). Naomba nikujuvye jambo muhimu; sasa hivi tupo kwenye campaign za uchaguzi. Mgombea unaye mshabikia unaweza kumharibia development ya campaigns zake kwa kuleta hisia kuwa anategemea ushindi wa kuiba kura! Kwa vile kura hazijapigwa wewe utasemaje kuwa tarehe 31 Oct watu watamwona akirudi magogoni ! Kwa procedure gani? Kama ni ushindi wa kura subiri watu watose kura zao kwenye ballot box na matokeo yabandikwe ndio useme hilo la kwako.
Ndugu yangu usidhani mambo ya uchaguzi ni mchezo wa karata tatu..sio ... and anything against your belief can happen na ukajikuta badala ya kukaa kwenye laptop yako na kubwatuka bwatuka ukawa huna hiyo fursa tena na katika mazingira tatanishi kiasi usijuwe laptop yako iko wapi na wewe mwenyewe upo wapi.
Mimi huenda ni mshabiki wa Dr Kikwete kuliko wewe, lakini siwezi ku-behave kijinga kama unavyofanya. Vilevile, kwasasa siamini kama ushindi wa Dr Kikwete utakuwa rahisi na au wa kishindo kama ilivyokuwa 2005, hii ni kwasababu mambo mengi yamebadilika. Lakini pia ninazo sababu zangu kadhaa (kama una akili ya kuzielewa) naziweka hapa:
Assume wagombea wawili ndio wanachuana kwa karibu (kila mtu atapoteza kura kwenda kwa wagombea wengine):
(1) Dr Slaa ameonesha uwezo mkubwa sana wa kujenga hoja kuliko Dr Kikwete (hili lipo wazi na sitajibu mabishano)
(2) Dr Slaa ameshakuwa maarufu karibu nchi nzima wanamfaham kwasababu ya ujasiri wa kutaja majina ya mafisadi na ameweza kuzunguka nchi nzima kupitia operation Sangara akieleza mambo yote kwa hoja zilizopevushwa kwa nguvu ya hoja ambazo kimsingi zimepokelewa na wananchi wengi popote alipopita (Hivyo Dr Slaa ataweza kuhimilishi kishindo cha umaarufu wa Dr Kikwete ambaye kwasasa bado ni raisi wangu)
(3) Dr Slaa ameonesha kuwa na uchungu wa nchi yake ambayo inafujwa waziwazi na kila mtu hata mpambe wa Dr Kikwete (kama mimi na wewe) hatuna pa kufischa nyuso zetu mbele ya ukweli huo. Kwa upande wa Dr Kikwete imekuwa vigumu kulithibitisha kama ana uchungu na nchi hii kutokana na kushindwa kuchukua hatua dhidi kashfa za wizi mkubwa ulioumiza na unaendelea kuumiza uchumi wa taifa letu masikini. Mfano mdogo tu ni mkataba wenye maumivu makali wa Richmond iliyokuwa inalipwa milioni 152 kila siku!!!!!! Hili hata mkulima wa kule Mbozi ndanindani hawezi kukubali.
(4) PhD ya Slaa ni genuine na inafanya kazi zaidi kuliko ya Kikwete ambayo ni honorary doctorate tu (na hii ndio msingi wa tofauti zao katika kujenga hoja)
(5) Campaign za mwaka huu zinamwelekeo wa kutaka ku-test statistics za communities kama dini na civil workers (there is a big potential for tug of war among the groups and can lead to civil riots or commotion)
(6) Hali ya afya ya Dr Kikwete ni dhahiri kuwa si njema na wala si kitendo cha kuanguka tu bali ni kitendo cha kurudiarudia kuanguka ndio kinaleta uthibitisho huo. Rais ni mgonjwa na ni vigumu kumtetea katika hali ya namna hiyo.
(7) Kuna kashfa zinazoizunguka serikali ya raisi Kikwete, zinatisha, zinatia hasira na hamasa ya kutaka mabadiliko ya uongozi wa kitaifa. Hili limeanza kushika moto na msisimuko mkubwa kwa jamii zote na makundi yote hapa nchini.
(8) Uongozi wa chama unaonekana kuzua maswali bila majibu sahihi. Ndani ya chama tawala kuna mfarakano mkubwa ambao haujawahi kutokea tangu chama hicho kiundwe. Makada wakubwa wanaondoka na kukihama chama chao. Chama kimejaa wafanyabiashara na watu wenye uraia na uzalendo wenye maswali. Kwa hakika hata chama hakina reflection ya Chama cha Nyerere tena. Watu ambao wanatuhuma ya ufisadi ndio watu wenye nguvu za maamuzi katika chama na wanaendesha mkakati wa kuondoa yeyote anayejifanya mpiganaji dhidi ya ufisadi Tanzania. Haya yote yanakirihisha nyoyo za watu wengi sana kutoka katika jamii zao na taifa kwa ujumla.

Kwa hali hiyo Dr Slaa ana hoja nyingi sana atakazoweza kuzuka nazo na kuziuza zikauzika mbele ya masikio ya wasikilizaji wake wote wakiwemo waislam, wakristo, wasomi, wakulima, maskini na baadhi ya matajiri, vijana kwa wazee, wanawake na wanaume... na kadhalika.

Kutokana na ukweli huo, watu wenye busara tunahitaji kuwa waangalifu katika kauli zetu kwa faida ya wale tunaowashabikia na pia kwa taifa letu. Wengine hatuna sehemu za kukimbilia kunusuru maisha yetu kama mambo yakiharibika. Kama huwezi kuona hiyo hatari basi labda wewe unayo sehemu nyengine ya kukimbilia kunusuru maisha yako kama hutakuwa umedunguliwa kabisa....

Tafadhali uwe mstaarabu, na ustaarabu unalipa. Kama unaamini Kikwete atashinda weka hilo moyoni mwako kwasababu kuna wanaoamini Slaa atashinda na sasa kila mtu akianza kutoa hizo hisia zake si tutaanzia hapa kutofautiana. Na tukirudi nyumbani kila mtu ataanza kunoa panga kujiandaa kwa makabiliano? Tuwe waangalifu kwa kauli zetu ili mchakato huu wa uchaguzi upite kwa amani. Mungu ibaeiki Tanzania. Napendekeza....
Sungura
 
Tatizo wafanyakazi wengi hawana ufahamu wa elimu ya uraia. Wengi wao wakienda kwenye kampeni za CCM na kusikiliza TOT wanachanganyikiwa. Ebu jiulize uke umati wa Jangwani ulitoka wapi kama sio wafayakazi. Siamini kabisa tabaka la wafanyakazi. Hawana msimamo. Afadhali machinga na madreva na kondakta wa daladala. Hawa wakishikilia jambo wana msimamo lakini wafanyakazi wanayumbishwa sana. Kwanza ndio watatumiwa kuiba kura kwa ajili ya CCM.

We acha ujinga wewe, ulifikiri wafanyakazi wa karne hii ndio wale wa karne za mwl, we hata husomi mambo ya wakati, hivi mfanyakazi mwenye akili wanaweza kukaa pale jangwani wakachomwe na jua kumsikiliza mtu kama JK, ule umati ulikuwa umejaa jobless kama kawa, na yule bibi nae ni mfanyakazi na wale watoto na wapiga debe na mama ntilie ni wafanayakazi? Acha unani hii wako wewe mwaka huu utajua kwamba wafanyakazi ni wa kina nani.
 
Back
Top Bottom