Kikwete anawakwepa watanzania wa USA - tena!


Ama kweli kuna watu ambao bado wanaota ndoto za mchana. Hivi mtoto wa mkulima unadhani hicho kilimo chako cha jembe la mkono ambacho ndicho kinatumiwa na wakulima waliowengi hapa Tanzania ndio kitatukomboa na kutufanya tuendelee?? Kati yako wewe na MWK nani ana mawazo ya kusadikika??

Hebu jiulize kwanza JK kaenda USA kufanya nini? Huo mualiko alioenda kuutoa huko ni kwaajili ya watu gani?? wakulima au wafanyabiashara??

JK ni Rais wa waTZ wote kwa hiyo waTZ walioko USA wana haki sawa ya kuonana nae kama ulivyokuwa nayo we mkulima.
 
Wabongo wa US muunde tawi la CCM huko kama walivyofanya wenzenu wa UK ndo mkuu wa kaya atakuwa tayari kuongea nanyi.Halafu upinzani wenu kwa serekali ya JK unaonekana wazi hapa, nadhani hata kama hasomi hapa taarifa zitakua zinamfikia.
 
ina maana rais ni wa wana CCM tu?

He hasnt got the bottle to face you guys, anajua mtamgrill kwelikweli....Msije mpa depression buree.Mngekua wanaCCM- ingekua ni mwendo "kidumu chama cha mapinduzi" na "CCM hoyee" huku akimwagiwa misifa kibao na angerudi bichwa limvimba kichizi.
 
Eti watu wa-behave kama maadili ya kiafrika yanavyosema, hebu tutolee upumbavu wako hapa na hayo maadili yako ya kiafrika. Wangekua wanafuata maadili ya kiafrika wasingekuwa wanaiba rasilimali kwa kasi kama hii. Wangekuwa wanafuata maadili ya kiafrika wasingekuwa wanawasaidia hawa wazungu wa makampuni mbalimbali ya madini watuibie, wangekuwa wanafuata maadili ya kiafrika wasingelindana kwenye kula rushwa. Kama maadili ya kiafrika ni kusema ndio kila kitu ambacho mkubwa wako anasema na huku akijua hakutendei haki basi hayo maadili yenu ya KIAFRIKA NI YA KIPUMBAVU na sitokubali kuyafuata.
 

Mkuu Geeque,

Yaani tumwambie Invisible kuwe na kuweka thanks 100 maana hapa ningebonyeza mpaka zifike.

Umeongea yote zaidi hata ya yale ambayo ningeweza kuandika. Hakuna cha kuongezea hapo mkuu.
 
Anasubiri muunde 'Jumuia' kwanza ndio akutane nanyi. Hamuoni wenzenu wa Uingereza mambo yanavyowanyookea?

Hakuna kunyooka kitu. Jiulize kwa nini wanapenda sana kupita London? Ukilijua hilo utaona jinsi pesa ya walipa kodi inavyoteketezwa kwa kupitia ofisi hii, na ipo siku tutaweka shinikizo kwa serikali ya UK kufunga account za wezi wote kutoka Tanzania. Mugabe hadi sasa analialia kama tumbili maana kilichompiga usoni alikuwa hakifahamu sasa tunaye huyu JK ambaye anafikiri sisi wote ni mataahira.
 
Nina wasiwasi kama "mtoto wa mkulima" ni mtoto wa mkulima kikweli, labda mtoto wa kigogo akijifaragua kama mtoto wa mkulima au ana makovu ya kisaikolojia na safari.Mtoto wa mkulima wa kawaida Tanzania hata mtandao anausikia kwenye bomba, anataka kutuzuga nini?

Ingawa binafsi kama nilivyowahi kusema hapo nyuma sihudhurii vikao vya rais anapokuja huku (labda kujumuika na watanzania tu, sitegemei chochote cha kujenga) naamini Watanzania popote walipo wana haki ya kukutana na viongozi wao.

Hayo maneno ya mtoto wa mkulima yanaonyesha kukurupuka.

1.Nakubaliana na wewe, ingawa kwa sababu tofauti.Ni kupoteza muda kwa sababu maswali muhimu yanajibiwa kwa propaganda na "responses" badala ya kufanyiwa kazi.

2.Dead wrong, kuna watu huko bado wanafikiri Nyerere ndiye rais.Kama nilivyosema, labda wewe ni mkulima special kwenye shamba lake la minanasi au upo kwenye "ukulima wa vigogo" ndiyo maana una special access.

3.Sio lazima kurudi nyumbani ili mtu ashiriki katika mchakato wa siasa na uchumi.Kuhusu fedha kutokuwa na impact hapa unajionyesha ukosefu wako wa habari, remittance za Watanzania zinaleta fedha nyingi za kigeni kuliko dhahabu, kwa mujibu wa ofisi ya makamu wa rais 8% ya familia za Tanzania zinategemea remittance *. By October 2007 Unajua kwamba 2.4% ya GDP au $ 313m zilitokana na remittance (International Fund for Agricultural development)**

Tafadhali lete masuala yenye kina, sio vitu visivyoeleweka.

Sources

* http://www.sendmoneyhome.org/uploads/2007/04/uk-press-release-07a-updated.doc

** http://www.ifad.org/events/remittances/maps/africa.htm
2007 International Forum on Remittances at the IDB Conference Center in Washington DC, on 18-19 October 2007.

*** http://www.iht.com/articles/ap/2006/10/26/business/AF_FEA_FIN_Tanzania_Mining.php

http://www.livelihoods.org/hot_topics/docs/RemitTanzania.pdf
 
Napenda pale isssues zinapojibiwa kwa nguvu ya hoja na siyo hoja za nguvu. Thanks Pundit for useful resources
 
Mkuu Geeque,

Yaani tumwambie Invisible kuwe na kuweka thanks 100 maana hapa ningebonyeza mpaka zifike.

Umeongea yote zaidi hata ya yale ambayo ningeweza kuandika. Hakuna cha kuongezea hapo mkuu.

Ahsante sana Mazee, unajua wakati mwingine inashangaza pale baadhi ya watu wanapokuja na ngonjera ndefu za kunyamazisha watu kwa kutumia vigezo ambavyo havina kichwa wala mguu.
 
Hii habari ya zamani lakini nimeona niweke hapa...alafu hili la kukwepa ni kuwa Rais ndio anapanga kuonana na Wananchi au wawakilishi wetu kwenye nchi husika ndio wanatakiwa kufanya hivyo? Sometimes wengine tunaolalamika kuwa kakwepa kuonana na Watanzania tunakaa sijui California,Minnesota au Texas sidhani kama tunategemea afunge safari kuzunguka US nzima kuonana na Bongonians. Muungwana anageuza jumapili so kuna leo na kesho nadhani anaweza kupata nafasi.


Source hii hapa
 
Hii article ya kipambe kaandika nani? Isije kuwa ndiyo mtandao unafagilia.
 
Jamani acheni kulalamika!
Mungwana hakwenda pale for his people's interest! Ameenda for his own interest.
Kaalikwa na mabesti wake na matapeli wa kimataifa akina Andrew Young na Paul Tudor Jones! Wamempa tuzo na kumwagia sifa. sasa aonane na wabongo kwa nini, ili wampe mfadhaiko wa akili? No way, Mwafrika wa kike, wewe ndiyo ulimwambia mungwana abembee! sasa utaona anavyojua kubembea!
This is our president! Tungojee hiyo 2010!
 

Ina maana hao jamaa ndiyo wamelipa gharama zote i.e. usafiri, malazi pale Four Seasons, per-diem za ujumbe wake ??!!
 
Susuviri,
I couldnt have said it better. Niliachwa mdomo wazi kwenye ile tafrija ya jana usiku pale Andrew Young alipomwintroduce Kikwete kama kiongozi aliyekuwa "groomed" na Julius Nyerere. Sioni lolote ndani ya uongozi wake linalofanana na Julius Nyerere. Lakini baada ya kusoma bandiko la Kichuguu kuhusu Andrew Young, sishangai tena. Hawa wapo hapa kwa maslahi yao wenyewe na kampuni zao. Kampuni ya Andrew Young, Goodworks International, imeshalalamikiwa Nigeria. Huko Tanzania wameshanunua Hotel Mount Meru. Mwakilishi wake pale Dar-es-Salaam alipokelewa kiserikali na rais akiagiza apewe usafiri wa kiserikali. Ila naunga mkono wazo la Sullivan Summit kufanyika Arusha. Hii pia itasaidia kuiweka Tanzania kwenye ramani na kutuongezea utalii. Katika tafrija za jana walikuwepo Boys 2 Men original. walitumbuiza kwa nyimbo zao tamu kukiwemo na ule "End of the Road." Chris Tucker did not disappoint either. Mwawado, sikukuona, ingawa hata kama tulionana singeweza kukufahamu. And so Icadon. There was no press room.
 

Jasusi,

Karibu sana, ulipotelea wapi?
 

Nitakwambia zaidi kwenye pm, meza ya press sikuiona vile vile.Alafu ni watu wangapi walinunua hizo DNA test kits?

Mwaka 2005 katika pita pita yangu nilijikuta pale Georgia State University Andrew Young School of Policy Studies, baada ya semina ile akawa anazungumzia kuhusu uchaguzi wa Tanzania na alimzungumzia Rais Kikwete kiundani(inaonekana wanajuana sana)


Andrew Young
 
Jasusi, habari za kufanyika mkutano huu Arusha mwakani zilikuwa tayari kwenye habari six months ago. Je ilikuwa ni lazima Rais ndiyo aje kutangaza hilo? Halafu hiyo tuzo ina prestige gani ya kumfanya mtu akurupuke kwenda kuifuata? Kwanini wasiamue kusubiri na kumpatia watakapokuja mwakani? Nadhani najua jibu la hilo swali la mwisho... they are helping him out kwa Watanzania!!!
 

Kwi, kwi, kwi,
 
Tatizo watu wameweka maadili ya kiafrika mbele" Heshima ya mshumaa" kuliko interest ya taifa .
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…