One need not look far, as if to provide a natural retort to Kikwete here is an article from today's IPPMedia.
So much for security
http://www.ippmedia.com/cgi-bin/ipp/print.pl?id=111469
Majambazi Dar yakomba Mil.5
31 Mar 2008
By Mwandishi wetu, Jijini
Kundi la majambazi waliokuwa na silaha limevamia bar moja iiliyopo katika maeneo ya Sinza Jijini na kurusha risasi kadhaa kabla ya kufanikiwa kupora pesa kiasi cha shilingi Milioni 5 na mali nyingine kadhaa za wateja kabla ya kuingia mitini.
Aidha, majambazi hao wamefanikiwa vilevile kupora mali kadhaa za wateja waliokuwa wakijichana kwa vinywaji na makulaji ya kila aina na hivyo kuwapa hasara kubwa.
Taarifa za mashuhuda wa tukio hilo la kuogofya zinaitaja sehemu iliyokumbwa na balaa hilo kuwa ni ile iitwayo Corner Bar.
Wanasimulia mashuhuda kuwa tukio hilo limetokea mishale ya saa 4:00 asubuhi wakati majambazi hayo ambayo baadhi yalikuwa yamevalia kwa staili ya kanzu na barghashia yalipotua na kuanza kupora mapesa.
``Walikuwa zaidi ya majambazi wanne... baadhi walivalia kama maustaadhi,`` akasema shuhuda huyo.
Akisimulia zaidi tukio hilo, mteja mmoja aliyekuwa ndani ya bar hiyo amesema majambazi hayo yalipojitoma ndani ya bar, yalikwenda moja kwa moja kaunta na kumsukasuka mtu anayeelezewa kuwa ndiye mmiliki wa bar hiyo, aliyekuwa akinywa mtoli.
Akasema baada ya kumkamata, yakawa yakimuamuru atoe pesa.
Akasema mmiliki huyo akawa akikataa kwa maelezo kuwa hakuwa na pesa.
Akasema baada ya majambazi kuona yanabishiwa, mmoja wao akachomoa bastola na kufyatua risasi kadhaa hewani huku mwingine akitembeza kipigo.
Kwa mujibu wa shuhuda huyo, baada ya mwenye bar kuona hali inazidi kuwa ngumu, akaamua kuwaongoza hadi kaunta ambako walijizolea fedha zote zilizokuwepo, ambazo zinatajwa kuwa ni zaidi ya shilingi milioni tano.
Kwa mujibu wa shuhuda huyo, baada ya majambazi hayo kuhakikisha kuwa yamekomba fedha zote zilizokuwepo kaunta, yakawageukia wateja wachache waliokuwepo asubuhi hiyo na kuwapora mali zao ikiwa ni pamoja na simu za mkononi.
Akasema baada ya uporaji huo, majambazi hayo yakafanikiwa kutokomea kiulaini bila kuwepo kwa kelelele ya aina yoyote mahali hapo.
Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni, Jamal Rwambow amethibitisha kutokea kwa tukio hilo.
Kamanda amesema kuwa polisi wamekuwa wakifuatilia tukio hilo kwa karibu na hadi sasa, juhudi za kuwatia mbaroni watuhumiwa hao zinaendelea.
``Tuko kwenye hatua nzuri za kuwatia mbaroni watuhumiwa, ``akasema Kamanda Rwambow.