Kikwete aombe msamaha au atolee maelezo maneno haya


Hizi argunment za vijiweni na ushabiki wa vyama...I won't waste my energy and time
 
With the daily headlines za majambazi wameiba hiki kule, wameua wangapi pale hata hiyo traditional security kutoka violence iko questionable.
 
Hizi argunment za vijiweni na ushabiki wa vyama...I won't waste my energy and time

Nani anahitaji arguments zako na energy zako hapa! umekuja mwenyewe JF na utaondoka mwenyewe taratibu na wala sio kuja kutoa vitisho as if wewe ndio mwenye internet zote duniani.

Grrrrrrrrrrr
 
Nimefurahishwa na mtiririko wa mjadala wa kumtaka Kikwete aombe radhi kwa kauli yake kwamba CCM ni chama pekee kinachoweza kutunza amani.

Mimi binafsi sihitaji kuwa makini katika kunukuu alichokisema JK. ninachohitaji ni kupata mahali pa kuwakumbusha wanachama wa JF kuwa kuropoka ni silika ya CCM na ya kuwa hakuna siku watajutia kutoa kauli ya kuwakwaza wananchi.

Wanachama na viongozi wa CCM kwa ujumla wao wanaamini kabisa kuwa hata kwenye kuongoza hakuna chama kinachoweza kuingia ikulu, hata kama kikipewa ridhaa hiyo na wananchi. Huu ni upofu wa kawaida kabisa katika siasa.

Kauli ya JK ni utambulisho tu kuwa anakiongoza chama cha watu wasiojua chochote kuhusu vipaji vilivyoko nje ya chama chao na ya kuwa imani yao imefunikwa kwenye Zidumu Fikra za Mtu Mmoja tu.
 
Ukiwa na akili za matope unaweza ukakubali kwamba ccm imeleta amani,lakini kwa mwenye akili timamu amani haipo.Au watu hawajui maana ya amani?Amani TZ haipo ila ni woga umewajaa watz.Tunayofanyiwa na viongozi wetu halafu tuseme tunayo amani then tutakua ni vipofu.

Tuogope moto wa jehanam jamani au wenzetu hamuamini kama Mungu yupo.Amani ya watanzania iko wapi,maovu mangapi wananchi wanafanyiwa.
 
One need not look far, as if to provide a natural retort to Kikwete here is an article from today's IPPMedia.

So much for security

http://www.ippmedia.com/cgi-bin/ipp/print.pl?id=111469

Majambazi Dar yakomba Mil.5

31 Mar 2008
By Mwandishi wetu, Jijini

Kundi la majambazi waliokuwa na silaha limevamia bar moja iiliyopo katika maeneo ya Sinza Jijini na kurusha risasi kadhaa kabla ya kufanikiwa kupora pesa kiasi cha shilingi Milioni 5 na mali nyingine kadhaa za wateja kabla ya kuingia mitini.

Aidha, majambazi hao wamefanikiwa vilevile kupora mali kadhaa za wateja waliokuwa wakijichana kwa vinywaji na makulaji ya kila aina na hivyo kuwapa hasara kubwa.

Taarifa za mashuhuda wa tukio hilo la kuogofya zinaitaja sehemu iliyokumbwa na balaa hilo kuwa ni ile iitwayo Corner Bar.

Wanasimulia mashuhuda kuwa tukio hilo limetokea mishale ya saa 4:00 asubuhi wakati majambazi hayo ambayo baadhi yalikuwa yamevalia kwa staili ya kanzu na barghashia yalipotua na kuanza kupora mapesa.

``Walikuwa zaidi ya majambazi wanne... baadhi walivalia kama maustaadhi,`` akasema shuhuda huyo.

Akisimulia zaidi tukio hilo, mteja mmoja aliyekuwa ndani ya bar hiyo amesema majambazi hayo yalipojitoma ndani ya bar, yalikwenda moja kwa moja kaunta na kumsukasuka mtu anayeelezewa kuwa ndiye mmiliki wa bar hiyo, aliyekuwa akinywa mtoli.

Akasema baada ya kumkamata, yakawa yakimuamuru atoe pesa.
Akasema mmiliki huyo akawa akikataa kwa maelezo kuwa hakuwa na pesa.

Akasema baada ya majambazi kuona yanabishiwa, mmoja wao akachomoa bastola na kufyatua risasi kadhaa hewani huku mwingine akitembeza kipigo.

Kwa mujibu wa shuhuda huyo, baada ya mwenye bar kuona hali inazidi kuwa ngumu, akaamua kuwaongoza hadi kaunta ambako walijizolea fedha zote zilizokuwepo, ambazo zinatajwa kuwa ni zaidi ya shilingi milioni tano.

Kwa mujibu wa shuhuda huyo, baada ya majambazi hayo kuhakikisha kuwa yamekomba fedha zote zilizokuwepo kaunta, yakawageukia wateja wachache waliokuwepo asubuhi hiyo na kuwapora mali zao ikiwa ni pamoja na simu za mkononi.

Akasema baada ya uporaji huo, majambazi hayo yakafanikiwa kutokomea kiulaini bila kuwepo kwa kelelele ya aina yoyote mahali hapo.

Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni, Jamal Rwambow amethibitisha kutokea kwa tukio hilo.

Kamanda amesema kuwa polisi wamekuwa wakifuatilia tukio hilo kwa karibu na hadi sasa, juhudi za kuwatia mbaroni watuhumiwa hao zinaendelea.

``Tuko kwenye hatua nzuri za kuwatia mbaroni watuhumiwa, ``akasema Kamanda Rwambow.
 

Dada Mwafrika wa Kike,

Kwa upana wa tafsiri ya neno "amani" kama unavyouweka kwenye wasilisho lako la sasa, hakika ni vigumu kuamua kama yeyote amewahi kuleta amani Tanzania. Lakini kama vigezo vyako siyo "all inclusive", yaani siyo lazima viwepo vyote ili tungo hiyo iwe kweli, basi ni wengi sana (including CCM) wanaoweza kudai kuwa wamechangia amani ya nchi, na hiyo inazidi kuifanya kauli ya JK kuwa sahihi. Na binafsi ningemshutumu sana JK kama angesema kuwa ni CCM pekee inayoleta amani Tanzania. Watu wa dini wanaofundisha maadili mema, nadhani wanachangia sana kwenye amani hasa wanapotufundisha kuhusu dhana ya "dhambi", ambayo ni pana kuliko "jinai", maana jinai huthibitishwa kwa ushahidi (mahakamani), lakini dhambi haihitaji ushahidi, ni Mungu ndiye anayeona na kuamua hata kama hakuna ushahidi wa binadamu!

Matumizi mabaya ya neno "amani" kwa hakika yanapaswa kukemewa kwa nguvu zote. Tumeona watu wakichagua mifano mibaya ya ukosefu wa amani kama vita za Somalia na Rwanda na kuyaonesha katika luninga na video ili kutishia watu na kuwafanya wachukie ama kuogopa kuchagua upinzani. Hii ni aina mojawapo ya extremism, ni ma-extremist wa CCM walitumia athari za extremists wa ukabila kuwatishia moderates, na hivyo kuwafanya hawa moderates wawachague extremists, sio kwa kuwapenda, bali kwa kuogopa aina nyingine ya extremism. Ni mbaya sana hii, na inanisikitisha sana kuwa CCM hawakupinga wala kukemea hii tabia (na inaniwia vigumu kuamua kama walinyamaza kutokana na ignorance ama ndio uliokuwa mkakati wao?). Haya yametokea pia huku Ulaya, kuna mbunge mholanzi ametoa sinema inaitwa FITNA yenye mapicha ya kutisha kutoka mitandao ya extremists wa kiislamu, na anajaribu kuwatisha raia wengine wa Ulaya kuwa hicho kinachoonekana katika movie hiyo ndicho waislamu watakachoendelea kuifanyia Ulaya! Tafsiri yangu ni ileile kuwa huyu mzungu ni extremist, anapinga uhamiaji, hivyo anatumia athari za extremists wa kidini kuunga mkono ideals zake za extremism, kuvuta wale walio moderates waingie upande wake, na anaamini moderates ni rahisi kutishika. Bahati nzuri huyu wadachi wenyewe wamempinga sana, na hiyo film imepigwa vita Ulaya yote, hata Ban Ki Moon kaikemea.

Narudi kwenye mjadala wa kauli ya Kikwete. Yaliyomo kwenye wasilisho lako nililonukuu hapo juu ni sahihi kimsingi, lakini hayakanushi usahihi wa kauli ya JK. Yaani haya uliyosema ni kweli, na hayo aliyosema JK pia ni kweli, hasa kwa mtazamo wa tafsiri pana ya neno "amani". Kazi yetu ni kumshawishi yeye JK na wenzie kuwa haya pia ni ya kweli na ya muhimu sana, ayachukue ayafanyie kazi, na kama hawezi au hataki, basi yako mioyoni mwa wapiga kura wake na wanaweza kuyatumia dhidi yake wakati utakapowadia.
 

YOTE ULIYO YASEMA NDUGU MASAKA NI YA KWELI.
 
Mwafrika wa kike acha mambo ya wivu.Umekosa hoja sana unaleta vioja.Mhe Jakaya Mrisho kikwete alikuw akatika Vikao vya Chama chake.hivyo kusema maneno hayo ni sawa kabisa.wewe ulitaka akawaambe CHADEMA maneno hayo?
ON THIS SIDE MY PRESIDENT WAS RIGHT 100%.Mie naona sasa tuanze kujadili matatizo waliyonayo watanzania ili serikali ianze kuyafanyia kazi kuliko kila siku kuponda viongozi wa o binafsi bila ya kujadili matatizo muhimu ya watanzania.na naamini ndio lengo la vyama vyote vya kisiasa!
 
kuna falsafa moja inasema "amani haiji pasipo na haki"...sasa huyo anayetetea kauli ya kikwete aende akamkumbushe kuwa tanzania hakuna haki, hivyo hakuna amani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…