Elections 2010 Kikwete awateua Meghji na Nahodha ubunge

Elections 2010 Kikwete awateua Meghji na Nahodha ubunge

Tangu lini mkwere akawa siriaz!!! Tumeamua kulikoroga basi tulinywe. Serekale itaendelea kuwa ya kishikaji!!!! Hata kama watu wataendelea kuichukia CCM. Washkaji lazima wawepo kwenye temu: Akina Masha, Kamala, Buriani na vigogo wengine mtawasikia!!!! Malalamiko yenu yeye hayamuhusu!!!Watajijua watakaokuwa CCM wakati huo.
 
tuache udini wana jf au la sivyo tutashindwa kujadili mambo muhimu ya kuendeleza taifa letu. Je unamjua salim ahmed salim ni mwislam lakini cv yake inatufurahisha wote an dunia yote pamoja na kuwa wao wanzanzibar hawamtaki. Tusichokitaka hapa ni kuteua mradi kuteua watu ambo ni nonperformers kama huyo prof kafanya nini? Tupe cv yake basi. Shida kubwa kwa jk ni kuteua ndugu zake kulipa fadhila hii ndiyo hatuitaki kabisaaaaa.




labda mkulu kipindi kile alipangiwa kazi na mwalimu zanzibar huyu prof alimkaribisha kwa muda?
 
William, nimekusoma. Lakini naomba uwe mkweli katika mjadala. Sio kweli Zakia aliondoka kwa kashfa, kama ulivyoweka hapo juu. Jaribu kuwa mkweli....wewe ni CCM kama sikosei. Wewe uko kundi gani??? Kwanini chama chenu kinakosa nguvu sasa ? Je ni uchu wa madaraka sababu moja wapo? Ni uongozi mmbovu wa katibu na mwenyekiti wake?

1. Mkuu heshima yako sana, Mama Meghji aliondoka kutokana na kashfa ya BOT iliyohumusu pia Gavana wa BOT ambaye na yeye Rais aliishia kumfukuza kazi akiwa nje ya nchi, sidhani kama hili linahitaji mjadala tena unless unajua something wengi hapa hatukijui sema tu mkuu ndio maana ya uwanja wa Great Thinkers!

2. Ni kweli mkuu mimi ni mwanachama wa CCM, kundi langu ni kundi lolote linalojali taifa kwanza. CCM haijakosa nguvu kwa sababu bado ni chama kilichoshinda wabunge wengi yaani majority bungeni tena kwa namba kubwa sana, uchaguzi wa majuzi umeonyesha kwamba tuna mapungufu ya muda mrefu ambayo wananchi wameanza kuchoshwa nayo baada ya kuahidiwa kurekebishwa kwa muda mrefu sana lakini bila mafanikio yoyote.

- Kwa kawaida kama unayajua mambo ya siasa na watawala huwa ni vigumu sana kwa chama ambacho kimeshika power for the last 50 years, kusikia maoni na maonyo ya wanachama wake, kwa hiyo ni matokeo ya uchaguzi kama huu na hasa kushuka kwa namba za Rais kwa almost 20%, ndio kunaweza kuwafanya watawala wa-pay attention. Unajua kwa maneno mengine ya kisiasa kupungukiwa huko kwa kura ni pamoja na kupigana na kivuli chako mwenyewe, maana ni wewe mwenyewe ndiye umewapa wananchi sababu ya kukupunguzia kura na sio anybody else!

- Ninaamini kwamba ujumbe umefika na kwamba kama alivyosema Rais Reagan, the buck stops with Mwenyekiti.


William.
 
Halisi,

Prof. Mbarawa aligombea kupitia chama kipi huko Mkanyageni? Nataka kujua kama ni CUF na hivyo kuwa matokeo ya muafaka.

Hi ni dalili kutokea Zanzibar hakuna wabunge wa maana wa CCM wanaoweza kuwa mawaziri na hivyo kuanza kuteua.

Pia kwa watu toka Zanzibar lazima tutegemee kwa asilimia karibu 100 watakuwa Waislam hivyo sidhani kama tunahitaji hata kujadili juu ya dini zao.

Nafikiri hapa hatujadili udini, ishu ni mafisadi wapo waislam, wakristo na wapagani. So tujadili utendaaji au vipi wana jf
 
2.jpg

Any one with good clarifications pleaseeeeeee!!!!!
 
Nahodha Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na mama mkwe "jikoni kumtayarishia babamkwe mahanjumati". Tehe-tehe-tehe!

Sure, naona hii nafasi ni special kwa wazanzibari na iko wazi baada ya Seif Idd kuwa makamu wa pili wa rais visiwani.
 
Sinta shangaa kutajwa Baraza jipya litakuwa na sura kama dodoki, walioshindwa kuperform in last cabinet na maswaiba waliopigwa chini na wananzengo ukawakuta wamepozwa humo. Msitarajie jipya ni yale yale maana sikio la kufa halisikii dawa!
 
Tangu lini mkwere akawa siriaz!!! Tumeamua kulikoroga basi tulinywe. Serekale itaendelea kuwa ya kishikaji!!!! Hata kama watu wataendelea kuichukia CCM. Washkaji lazima wawepo kwenye temu: Akina Masha, Kamala, Buriani na vigogo wengine mtawasikia!!!! Malalamiko yenu yeye hayamuhusu!!!Watajijua watakaokuwa CCM wakati huo.

Umemsahau Mbega, Mongela, Msekela, Kandoro na Mwakipesile
 
Hii website ni kwa ajili ya watu wote wenye maoni ya wazi kwa kuzingatia katiba ya nchi. hivyo katika jamvi hili kila mtu anafanya maamuzi nini au kitu gani anataka au yuko interested nacho kujadili, kama wewe utapenda dini wenzio watakuwepo, kama utaamua kujadili ujinga ujinga wenzio pia wapo, kama utaamua kujadili mambo ya kifisadi wenzio wapo, ukiamua kujadili mambo ya maendeleo wenzio pia wamo, ukiamua kujadili maisha ya watu wenzio pia wamo. kwa kifupi humu ndani kila kitu kinajadiliwa, fanya uamuzi unataka kujadili nini na kujifunza nini, yasiyokuhusu achana nao.

I like this. jibu zuri. Good show
 
Eti jamani nasikia mke wa Ridhwani Kikwete ni mtoto wa Zakia Meghji. Je ni kweli?
 
Makame Mnyaa Mbarawa
mechanical engineer, researcher

Location: Pretoria
Country: South Africa
Makame Mnyaa Mbarawa is recognized in Marquis Who's Who.:tape:

Habari zisizothibitishwa zinadai kwamba Muungwana akisafiri huko nje na kukutana na Watanzania huwauliza baadhi yao kwa nini wameamua kwenda nje. Baada ya hapo huwataka warudi nyumbani na kuwaahidi kwamba atawasaidia kupata ubunge na hatimaye uwaziri. Kama habari hizi ni za kweli basi huenda jamaa Mnyaa naye ni mmoja wa hao!
 
Back
Top Bottom