Kikwete azindua Windows 7 ya Kiswahili

Kikwete azindua Windows 7 ya Kiswahili

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Joined
Mar 10, 2006
Posts
33,771
Reaction score
41,027
UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS


Telephone: 255-22-2114512, 2116539

E-mail: press@ikulu.go.tz
Website: Mawasiliano Ikulu

Fax: 255-22-2113425


PRESIDENT’S OFFICE,

THE STATE HOUSE,
P.O. BOX 9120,
DAR ES SALAAM.
Tanzania.



TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI


Mfumo wa Mawasiliano ya Kompyuta kwa Kiswahili wazinduliwa


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete usiku wa jana, Jumanne, Mei 24, 2011 alizindua rasmi Mfumo wa Mawasiliano ya Komptyuta wa Windows 7 Kiswahili Interface Pack unaotumia lugha ya Kiswahili na unaotarajiwa kunufaisha zaidi ya watu 150 milioni wanaozungumza Kiswahili kote duniani.


Sherehe za uzinduzi wa Mfumo huo wa Mawasiliano zilifanyika kwenye Hoteli ya Kilimanjaro Kempinski Jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa miongoni mwa wageni wengine Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Profesa Makame Mbarawa na Meneja Mkuu wa Microsoft Kanda ya Afrika Mashariki na Kati.


Katika uzinduzi huo, Rais Kikwete amesema Mfumo huo wa Mawasiliano kwa njia ya Kompyuta unaotumia Lugha ya Kiswahili, umefungua ukurasa mpya wa historia ya maendeleo ya teknolojia ya habari na mawasiliano na ya matumizi ya Lugha ya Kiswahili, kwani kwa mara ya kwanza lugha hiyo inapewa nafasi sawa na lugha nyingine kubwa duniani zinazotumika kwa kupashana habari na mawasiliano kwa njia ya kompyuta.


Rais Kikwete ameipongeza na kuishukuru Kampuni ya Microsoft kwa kutambua na kuthamini umuhimu wa Lugha ya Kiswahili. “Uamuzi wenu huo utasaidia sana katika kukuza na kuendeleza Lugha ya Kiswahili”, amesema Rais Kikwete na kuongeza, “utawafanya wale ndugu zetu wanaobeza na kutotaka kuendeleza matumizi ya Lugha ya Kiswahili katika elimu, sayansi, teknolojia na shughuli za serikali na biashara kuwa na mawazo tofauti.


Amesema upatikanaji wa programu ya kompyuta ya Windows 7, utawawezesha watumiaji wa Kiswahili duniani kunufaika na matumizi ya lugha wanayoielewa zaidi katika kompyuta na hivyo kuondokana na kikwazo cha lugha, kwani watajipatia elimu na maarifa kupitia mitandao ya kompyuta na pia kurahisisha mawasiliano kwa njia ya baruapepe.


Mfumo wa Mawasiliano kwa njia ya Kompyuta unaotumia Lugha ya Kiswahili kwa kiasi kikubwa umetengenezwa na Watanzania wenyewe ambao wametafsiri zaidi ya maneno 300,000 ya kiufundi yaliyomo kwenye Microsoft Windows 7 Glossary kwenda kwenye Lugha ya Kiswahili wakishirikiana na Baraza la Kiswahili Tanzania (BAKITA) na Kampuni yenyewe ya Microsoft. Programu hii ya Kompyuta inategemewa kusambazwa kwenye taasisi zote za elimu hapa nchini.


Imetolewa na:


Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,

Ikulu,
DAR ES SALAAM.

25 Mei, 2011
 
sasa tusubiri misamiati mipya humo ndani, jirani zetu KE nimewahi kusikia kuwa nao wapo ktk harakati hizi.
 
Kuzindua haihitajiki pongezi kwa mzinduaji bali pongezi kwa msababishaji(microsoft) Ningefurahi sana na kujivunia lugha yetu nzuri kama ningesikia au kuona BAKITA wakiwa ni wahusika wakuu wa uratibu wa lugha hii ktk Afrika badala ya wakenya na kiswahili chao kibovu!!

Usishangae kuona mkweere kazindua kitu kilichotafriwa na wakenya bila ya yeye kujua wala bakita japo inatajwa kuwa wamehusika. Pale bakita ni kama kijiwe cha kahawa na nimefuatilia pana ukabila sana yani ukitaka kujua hilo nenda ukifika wasalimie kwakusema KAMWENE wote watakujibu !!!!!!
 
Naamini itakuwa ngumu kuitumia kuliko ya kingereza-mana misamiati yao huwa wanakaa bakita wenyewe na kuifeed-naamini itakuwa ni ajabu sana kwa sisi wa-tz wenyewe kushindwa kujua maana ya maneno mengine tutakayokutana nayo huko-
nilishwai tumia program flan kwa kiswahili-ikanishinda-misamiati haieleweki-mfano nilikuta neno password kwa kiswahili nikashngaa
 
hii kitu nishawahi kuitumia nikashidwa kuan maneno mengi mapya ambayo wengi hatuaytumii katika maisha ya kawaida , lakini nawapa pongezi hawa microsoft
 
Mimi nimesomea mambo ya IT, hivi vitu vya sayansi na teknolojia utavijua tu na si kwa muda mrefu, kadiri unavyotumia zaidi ndivyo utakavyoifahamu zaidi, suala la lugha au misamiati lisikusumbue kabisa utavijua na utavielewa barabara!
 
Naamini itakuwa ngumu kuitumia kuliko ya kingereza-mana misamiati yao huwa wanakaa bakita wenyewe na kuifeed-naamini itakuwa ni ajabu sana kwa sisi wa-tz wenyewe kushindwa kujua maana ya maneno mengine tutakayokutana nayo huko-
nilishwai tumia program flan kwa kiswahili-ikanishinda-misamiati haieleweki-mfano nilikuta neno password kwa kiswahili nikashngaa
Hilo neno hata mimi lilinizingua sana wenyewe wanaiita nywila!
 
.... amesema Rais Kikwete na kuongeza, "utawafanya wale ndugu zetu wanaobeza na kutotaka kuendeleza matumizi ya Lugha ya Kiswahili katika elimu, sayansi, teknolojia na shughuli za serikali na biashara kuwa na mawazo tofauti.

.... hii ni aina ya lugha za watu wanaoishi kwa kutegemea ajira zinazotegemea taasisi za lugha ya kiswahili na nadhani hata hotuba yenyewe itakuwaa imeandikwa na BAKITA & co. He's being used as a mouthpiece for them ...
 
mimi nina office 2003ya kiswahili misamiati yake sielewi wandugu
 
sina uhakika ila nadhani kimatumizi itakuwa na ugumu kidogo sababu misamiati mingi itakuwa migeni
 
Hilo neno hata mimi lilinizingua sana wenyewe wanaiita nywila!

password-nywila
keybord-baobonye
windows 7 - madirisha saba
mouse-kipanya
hard disk-diski ngumu
Hapa kazi ipo,hiyo ni mifano michache tu..kuna misamiati humo ambayo tangu nizaliwe sijawahi kuisikia kabisa!!
 
  • Thanks
Reactions: EMT
password-nywila
keybord-baobonye
windows 7 - madirisha saba
mouse-kipanya
hard disk-diski ngumu
Hapa kazi ipo,hiyo ni mifano michache tu..kuna misamiati humo ambayo tangu nizaliwe sijawahi kuisikia kabisa!!

Kwenye password hapo duh mi hoi. Kwanini wasingesema nenosiri ama ufunguo ama lolote linaloeleweka kirahisi? Aisee mi hoi
 
Hata mimi hoi. Wataalam wetu wanafikiri kila neno jipya lazima liwe gumu. Kuna warsha moja walibishania "TAB" baadhi wakisema iitwe "kichupishi" huku wengine wakitaka iitwe "kibonyezo chupi"...waliniumiza mbavu
 
Natamani kuiona hiyo Windows ya kiswahili. Kwa sisi tuliojifunza kompyuta zamani kwa hakika itatupa shida kidogo, lakini kwa vijana wanaoibuka sasa watazoea vizuri.
 
What is so special with Wondows 7 mpaka Rais wa Jamhuri ya Muungano akafungue? Seriously, there must be better things to do.
 
Inaitwa Window7 kiswahili Interface pack? Sasa hapo wamebadili nini?ubaya wake wale wasomi nguli wa lugha wanataka kuwadanganya watoto wetu watumie mineno migumu ya kiswahili! Siungi mkono hoja,mi ntaendelea na za lugha ya mtengenezaji yenyewe,watakaotaka watumio iyo iyo ya mchanyato!
 
password-nywila
keybord-baobonye
windows 7 - madirisha saba
mouse-kipanya
hard disk-diski ngumu
Hapa kazi ipo,hiyo ni mifano michache tu..kuna misamiati humo ambayo tangu nizaliwe sijawahi kuisikia kabisa!!

Hawa jamaa wa ajabu! wanatafsiri kama robot? Hawafikirii
Windows XP wanaiitaje?
Ukitafsiri kila jina la Operating system inayokuja utachemka!
Obama muite Obama. Wazazi wake hawakukosea kumpa jina hilo!
Vivyo hivyo Windows 7 ibaki Windows 7.
 
Hawa jamaa wa ajabu! wanatafsiri kama robot? Hawafikirii
Windows XP wanaiitaje?
Ukitafsiri kila jina la Operating system inayokuja utachemka!
Obama muite Obama. Wazazi wake hawakukosea kumpa jina hilo!
Vivyo hivyo Windows 7 ibaki Windows 7.
lugha yetu ndo inakuwa-haina maneno mengi-mimi sioni ulazima wakulazimisha kupata maneno ya kiswahili-hii ndo mana wanatuletea maneno magumu na ya ajabu-ingekuwa vizuri kama baadhi ya maneno yakaachwa vilevile-maana kutumia maneno ya lugha nyingine haina tatizo-
 
lengo la microsoft siyo windows 7 ya kiswahili,lengo kubwa ni kujipenyeza ktk public sector za Africa.huko ulaya na asia wameshaachana na microsoft products kwa sababu zifuatazo.
-All Microsoft products must be vetted by NSA,FBI,CIA and other agencies,kwa lengo la kuweka loophole za kuingia ktk computers bila kizuizi na mtumiaji hawezi jua.
2- microsoft products hazimruhusu mtumiaji/mtaalam kufanya mabadiliko yeyote ktk software zao(soma EULA licence yao)
3-products za microsoft zina licence ya gharama za kila mwaka ,na pia zipo prone to virus attacks.

nchi za europ wamehamia ktk linux,e.g ubuntu,kubuntu. mfano hai ni bunge la ufaransa linatumia kubuntu linux,brazil hivyo hivyo.tatizowataalam wake JK wapo bize na posho za safari hawataki kufanya maamuzi magumu ya kuachana na microsoft
 
Back
Top Bottom