Mwanza ndivyo walivyo, Wakiamua jambo lao hata malaika ateremke toka mbinguni hawamsikilizi. Nyerere aliwashindwa tena wakati wa njaa akiwahimiza kulima mtama wakakataa na kwenye hotuba yake mwaka 1980 pale Nyamagana aliishia kuwatukana kwamba "waskumuma mmekataa kula ugali mwekundu".
Mwaka 1985 Paulo Bomani aligombea Mwanza akashinda. Akafanya kosa la kuhamia Dar badala yake akaporomosha bonge la jumba pale pembeni ya katikati ya shule ya Nyakabungo na Lake Secondary jirani na Mama Matemba.
Mwaka 1990 wana-Mwanza wakasema hata akigombea na shetani basi watampa shetani. Akaibuka mgombea asiyejulikana aitwaye Paschal Kulwa Mabiti. Akamchakaza Bomani licha ya kujulikana kwamba aligombea uhuru, alianzisha Nyanza Cooperative Union.
Kunanguka huko hata Nyerere kwamba wana-Mwanza wamemuondoa Bomani kwa kura ya chuki.
Kikwete anawajua vizuri wana-Mwanza. Mwaka 2005 wakati anagombea ndani ya CCM wajumbe waliokuwa wanawasili Dodoma walikuwa wanapokelewa na kila mgombea. Walipokuwa wanafika Kigoda, Salim, Malecela, Sumaye na kila aliyegombea alikuwa anaenda kwenye basi au stesheni kuwapokea.
Treni ya Mwanza ilipofika Dodoma wana-Mwanza walikataa kupokelewa na mgomea yoyote na walibaki wakiimba "sisi ni JK tu hatutaki mwingine". Kigoda aliondoka kimyakimya na Dodoma nzima ilijua kuwa ni JK tu licha ya kwamba NEC ilikuwa bado haijachagua majina matatu.
Walipobaki JK, Mwandosa na Salima kundi hili la Mwanza ndilo lililosababisha hata kule Chimwaga (UDOM ya sasa) kumwage wanajeshi wa JWTZ wala siyo FFU wakihofia wataleta vurugu kama Kikwete angeshindwa. Msishangae JWTZ kumwagwa sasa hivi. Tulioona Dodoma ile 2005 hatushangai, tena wakiwa wao kwa wao CCM.
Hivyo Kikwete anajua tabia hii ya wana-Mwanza. Anajua walivyomuinua, anajua watakavyomtikisa.