Bluray,
With all respect, mkuu wangu ni lazima kwanza tukubali ukweli kuwa JK bado ana umaarufu huo..Pamoja na makosa mengi ya utafiti, lakini hata mimi ukiniuliza JK against Kivuli, nitasema bora JK..na binafsi nina hakika kabisa kwa Wadanganyika ukimweka JK against viongozi wa Upinzani bado atakuwa na umaarufu zaidi yao..
Tuchukue mfamo mdogo sana hapa hapa JF penye wanachama zaidi ya 3,000..weka jina la JK against mtu mwingine yoyote utakayempendekeza wewe tuone matokeo...trust me, bado JK atachukua kwa sababu hakuna mwingine zaidi yake ndani ya CCM..
Ukienda nje watu watafikiria Unazi na Uchama kiasi kwamba Mbowe, Lipumba na wengineo wote hawatakubalika kwa sababu ya vyama vyao na sii uwezo wa viongozi hao kuleta mabadiliko.