Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,771
- 41,027
MMkjj,Hilo ombi la kwanza; ombi la pili, naomba mwenye nakala ya sheria hii anitumie nakala kwenye email yangu ya mwanakijiji hapa jamiiforums.com ASAP. Ombi la tatu, tuache kusikiliza na kutukuza masuluhisho yanayopendekezwa na wazungu tukifikiria kwamba yote yana nia njema kwa sababu ni ya wazungu!
Mkuu mbona umenishtukiza! kuna hitilafu gani ktk mfuko wa Jimbo ambao umekupa kiamsho hicho!
Itakuwa vizuri kama ukituelimisha sote manake wengine hatuna hata habari ya mfuko huo ukoje na unalenga vitu gani...
No no no huu ni ufisadi mwingine ati pesa zitaenda vijijini , vijiji gani hivyo. Kama vyama vya ushirika vilishindwa kumkomboa mkulima pesa hizi za kugawana bila malengo zitasaidiaje? Ubadhirifu wa fedha za umma ndio wimbo wetu wa taifa. Kinachokufanya uamini kwamba hizi wataogopa kuzitafuna ni nini?Mkjj, JK ni lazima asaini huu muswada sababu ni wa kuwaendeleza wananchi vijijini.
Kila wakati ambao kuna uwezekano wa pesa za serikali kupelekwa moja kwa moja kwa asilimia kubwa vijijini ni lazima wapenda maendeleo wote wawe mstari wa mbele kushabikia hilo suala.
Kinachofuata hapa ni kuhakikisha kuwa hizo hela zitumike vizuri.
Serikali yetu ukiwaachia hela zitatumia kwenye semina ngurdoto, kempinski na kwenye five star hotels huko europe.
Ningekuona una msimamo kama ungekuja juu vitafunio vya 19bilion vifutwe ASAP na waheshimiwa wale majumbani kwao na wageni wote kwenye ofisi za serikali waambiwe wale makwao kabla ya kwenda huko maofisini.
MKJJ, kwenye hili umekosea na tafakari Pros na Cons, utaona kwa wanavijiji kama sisi hili litatusaidia, issue ni kumake sure tu hizo hela zitumike vizuri.
JK amekuwa Rais mwenye maono mafupi kweli, yeye kila mara anafikiria kugawa hela.
- Mabilioni ya JK (tathmini ya mafanikio au vikwazo hakuna anayejua)
- Mil 500 kwa kila mkoa (tathmini ya mafanikio au vikwazo hakuna anayejua)
- Na sasa mfuko wa jimbo. (sijui anatumia vigezo gani kuleta tena mfuko huu)
Nchi inaendeshwa na "Vibwagizo"...
Wamesema wanaipeleka bunge lijalo, lakini hawataki kuuweka muswada wazi ili ijulikane kama unajibu maswali na hoja zilizoibuliwa...wakati sheria ya madini ambayo ingesaidia sana jamii haijapitiwa kwa miaka 12 na sasa wanairusha rusha kama mpira wa dana dana.
Jk atasign kwani hakuna historia ya kukataliwa mswada na Raisi Tanzania!!!Bunge lina uwezo wa kutunga sheria tu, Rais halazimi kukubali na ndiyo sababu ya kuweka checks and balances. Sheria hii ni mojawapo ya sheria za kipuuzi ambazo zimewahi kuja kutoka Bungeni na kuungwa mkono kwa asilimia 100 wakati sheria ya madini ambayo ingesaidia sana jamii haijapitiwa kwa miaka 12 na sasa wanairusha rusha kama mpira wa dana dana.
Kama Kikwete atatia sahihi mswada huu kama ulivyo sasa basi atakuwa kwa mara nyingine tena kuchagua upande wa maslahi ya watu wachache kuliko yale ya taifa na ataendelea kuonesha kile ambacho tumekiandika kwenye Cheche kuwa ni "kushindwa kuongoza". !
Baadhi yetu hatukufatilia vizuri jinsi Mfuko ule utakavyokuwa managed.Mfuko huu unawaongezea nguvu wabunge. Wabunge wanataka wawe kama masultani. Wanataka wanyenyekewe na kuombwa ombwa. Chochote kinachowaongezea uwezekano wa kufika huko, wabunge hawewezi kukipinga. Huu mfuko ni mojawapo ya vikolombwezo vinavyowaongezea uwezo wabunge wa kuwa masultani.
Kimsingi, ikiwa mfuko huu umekubaliwa na wabunge, ni vigumu kuupinga. Hakuna mwenye ridhaa ya wananchi, mwenye uwezo wa kukataa wanachokitaka wawakilishi wao. Hatuna ujanja hapa!
Lakini mfuko huu ukisimamiwa inaweza kuwa kisu cha kuwachinjia wabunge wengi. Subirini mtaona yatakayotokea.
Huu mfuko vile vile unaiongezea serikali nguvu dhidi ya wabunge. Kimsingi mfuko huo, unaifanya serikali ipate nguvu ya kuwashughulikia wabunge; mmoja mmoja au kama kundi. Kimsingi mfuko huo unawafanya wabunge wawe karibu zaidi na utawala (serikali); serikali kwa hivyo haiwezi kuukataa. Ni mojawapo ya vyambo vya kuwakamatia wabunge.
Tusubiri na tuone, kupinga haiwezekani tena; serikali wana maslahi, wabunge wana maslahi. Njia pekee ya kupinga huu mfuko ni kutowachagua hao wanaoushabikia katika uchaguzi ujao. Tunaweza??