Mfuko huu unawaongezea nguvu wabunge. Wabunge wanataka wawe kama masultani. Wanataka wanyenyekewe na kuombwa ombwa. Chochote kinachowaongezea uwezekano wa kufika huko, wabunge hawewezi kukipinga. Huu mfuko ni mojawapo ya vikolombwezo vinavyowaongezea uwezo wabunge wa kuwa masultani.
Kimsingi, ikiwa mfuko huu umekubaliwa na wabunge, ni vigumu kuupinga. Hakuna mwenye ridhaa ya wananchi, mwenye uwezo wa kukataa wanachokitaka wawakilishi wao. Hatuna ujanja hapa!
Lakini mfuko huu ukisimamiwa inaweza kuwa kisu cha kuwachinjia wabunge wengi. Subirini mtaona yatakayotokea.
Huu mfuko vile vile unaiongezea serikali nguvu dhidi ya wabunge. Kimsingi mfuko huo, unaifanya serikali ipate nguvu ya kuwashughulikia wabunge; mmoja mmoja au kama kundi. Kimsingi mfuko huo unawafanya wabunge wawe karibu zaidi na utawala (serikali); serikali kwa hivyo haiwezi kuukataa. Ni mojawapo ya vyambo vya kuwakamatia wabunge.
Tusubiri na tuone, kupinga haiwezekani tena; serikali wana maslahi, wabunge wana maslahi. Njia pekee ya kupinga huu mfuko ni kutowachagua hao wanaoushabikia katika uchaguzi ujao. Tunaweza??