Wadau, mimi sioni tatizo lolote kuhusu chakula alichowaandalia Ivory Coast maana Kiafrika hilo ni jambo la kawaida kabisa ya kuwa mgeni anakaribishwa na kupewa chakula kizuri kabisa kinachioweza kupatikana kwa mwenyeji wake. Huo ndiyo ukarimu wa Kitanzania.
Pili, nampongeza Rais kwa alichofanya, amewaonyesha wageni ukarimu wa Kitanzania hasa ukizingatia wachezaji wengi wa Ivory Coast wanatoka na kuishi Ulaya kwenye maisha ya kibinafsi na kichoyo, tena hata watu wa huko Afrika Magharibi wana tabia za ubinafsi-ubinafsi kwa hiyo hilo ni somo tosha kwa wageni wetu.
Tatu, si kweli kuwa kuna mabilioni ya shilingi yameteketea kwa gharama za kuandaa mlo mmoja, naamini hata mapato yaliyopatikana siku ya mechi yenyewe badi ni makubwa kulinganisha na gharama za chakula walichoandaliwa.
Nne Wa-Ivory Coast, kwa kutambua ukarimu wetu wameahidi kuwa iwapo watatwaa kombe la CAN basi watalileta Tanzania. Kwa hiyo, tumeweza kuwa-impact.
Mwsiho, pamoja na mapungufu yake nimegundua kuwa JK anajua sana PR na ndo maana huwa anapata favor ya ahadi za misaada anapotembelea ughaibuni ingawa kwa kweli misaada haitaweza kutusaidia sana iwapo hatutakaza buti dhidi ya ufisadi na kuhakikisha kinachopatikana kinafanya kazi iliyokusudiwa.