Kikwete hulipwa appearance fee?

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Joined
Mar 10, 2006
Posts
33,771
Reaction score
41,027
Jamani, katika pita pita yangu kuna ka nzi kametua mahali fulani bongo na kuniuliza kama kwa kunidokeza kuwa inakuwaje kuna agency moja nchini ambayo inakusanya hizo appearance fees. Kwamba akienda kufungua au kuzungumza kwenye hafla fulani fulani (kama moja inayoandaliwa sasa) basi kuna tucharge fulani ambato huwa tunalipwa kupitia wakala huyo.

Sasa, katika kuchokoza ndiyo naomba niwaulize wakubwa mnaojua, hizi fee ni kiasi gani, hiyo agency ni ipi (maana nimeambiwa nikiuliza nitadokezwa tu) na kama utaratibu huo ni sawa na kulipia Urais wake kila anapotokea kwenye hafla binafsi? Je haya ya fee yasibakie kwa watu ambao wameshatoka madarakani kama kina Mwinyi, Sumaye, au Mkapa?

Je yawezekana kautaratibu haka kako kwenye nafasi nyingine vile vile?
 
Mkuu mwanakijiji, hii inayojishughulisha na Mkulu siijui,ila kuna ile ya Mdada Fina Mango,ili ufanye hafla/presentation kwa wabunge lazima upitiye kwake,anabaraka zote za spika na wabunge wetu wanalijua hilo!!
 
Mambo ya bongo bwana, ha ha ha aaaaa..............!!!!!!!!!!!!!!
 
Je, hizo fees zinazokuwa charge kama ni kweli, zinakatwa kodi? Hivi karibuni tumefahamu kwamba Wabunge hawatozwi kodi, je Rais naye mshahara wake hutozwa kodi!?
 
- Hebu tu-assume kwamba ni kweli wanalipwa au kupewa fees, sheria yetu ya jamhuri inasema nini on the ishu?

William.
 
Hauxtable,
Sijaelewa kabisa ile ya dada Fina Mango. Naomba ufafanue kidogo.
 
- Hebu tu-assume kwamba ni kweli wanalipwa au kupewa fees, sheria yetu ya jamhuri inasema nini on the ishu?

William.

Swali zuri sana hili, lakini sidhani sheria yetu inasema lolote kuhusu hili kuna uwezekano mkubwa iko kimya.
 
Mkuu mwanakijiji, hii inayojishughulisha na Mkulu siijui,ila kuna ile ya Mdada Fina Mango,ili ufanye hafla/presentation kwa wabunge lazima upitiye kwake,anabaraka zote za spika na wabunge wetu wanalijua hilo!!

I am abit lost here, Fee ya kufanya presentation kwa wabunge? naomba tufafanulie please
 
Ninachofahamu ni kuwa ukialika kiongozi fulani unamlipa posho ya kuja kwenye shughuli yako. lakini sikujua kuwa posho hii hata Mkuu wa Nchi na wasaidizi wake wa karibu (VP na PM) nao wanalipwa
 
Mtu na akili yako kweli unamwalika Kikwete aje aongee...?
 
- Hebu tuone mfano wa wenzetu US, katika hii ishu wamekaaje:-

Hauxtable,
Sijaelewa kabisa ile ya dada Fina Mango. Naomba ufafanue kidogo.

Fina siku hizi yupo kwenye PR firm ambayo moja ya majukumu yake ni kuandaa shughuli mbalimbali. kama unataka kuandaa shughyuli fulani na ukataka fulani awe mgeni wa heshima, ukikodi firm ya akina Fina mango inashughulikia hayo yote na wewe unawalipa wao moja kwa moja.
nadhani suala la wabunge linaingia kwa sababu wakati fulani, akiwa Cluds, waliwahi kutembelea Bungeni, nadhani hapo ndipo 'urafiki' wake na sita na wabunge ulipoanzia au kukomaa
 
Mkuu,asante kwa ufafanuzi huo ila kwa kuongezea tu ni kwamba Spika aliwatangazia wabunge kuwa 'wao wapo na Fina Mango' na wabunge waliupokea kwa furuha ujembe huo,na furaha ile ilithihirisha kuwa wameuelewa usemi wa spika.
 
Mkuu mwanakijiji, hii inayojishughulisha na Mkulu siijui,ila kuna ile ya Mdada Fina Mango,ili ufanye hafla/presentation kwa wabunge lazima upitiye kwake,anabaraka zote za spika na wabunge wetu wanalijua hilo!!

Mkuu Hauxtable, je inamaana hata nikitaka kumualika mbunge mimi binafsi siwezi mpaka niione hiyo firm ya Fina Mango,ama?
 
Mkuu Hauxtable, je inamaana hata nikitaka kumualika mbunge mimi binafsi siwezi mpaka niione hiyo firm ya Fina Mango,ama?

Si lazima uwatumie wao. kama una uwezo wa kualika mtu yeyote unafanya hivyo. lakini ukitaka kuondokana na usumbufu unaombatana na maandalizi, unawatumia akina Fina
 
Si lazima uwatumie wao. kama una uwezo wa kualika mtu yeyote unafanya hivyo. lakini ukitaka kuondokana na usumbufu unaombatana na maandalizi, unawatumia akina Fina

Ok asante kwa ufafanuzi MN.
 
Mkuu Hauxtable, je inamaana hata nikitaka kumualika mbunge mimi binafsi siwezi mpaka niione hiyo firm ya Fina Mango,ama?
Mkuu, la-hasha si lazima kupitia kwa hii firm ila issue hapa ni PR. Inategemea sasa walengwa wa shughuli yako ni wa aina gani,alafu wajiuliza je 'Mzee wa mikasi' anatosha au ni 'Mkulu mwenyewe?' ndo ubunifu wenyewe wa kujipatia vipato ati!!
 
Ninavyoelewa mimi ma rais au viongozi wa nchi hawatakiwi kua na appearance fee. Mara nyingi kiongozi wa nchi hana nafasi kama kweli ni mchapa kazi. Mfano rais akialikwa kwenye hafla ya kuchangisha kujenga shule. (hawezi kucharge app fee). Na rais pia hatakiwi kufanya hivi ili kuepukana na lobbies

ni wabunge tu au mke wa rais ndio wanatakiwa kucharge appearance fee.

Lakini rais akimaliza mda wake anaweza kufanya "lecture circuit" na mara nyingi unatakiwa uwe muongeaji mzuri, ie bill clinton ametengeneza sana hela kwa hili.
 
Hii imeanza lini? Julius naye alicharge app fees? Ndio maana waku wa mikoa na wa wilaya hawaonekani siku hizi kumbe hata kutemebelea vijiji na kuhamasisha maendeleo wanataka walipwe app. feees, Tumekwisha
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…