Kikwete, huu mtandao ni hatari! Be careful, otherwise waweza kuwa historia (Part 1)

Mkuu utanisamehe sikupata nafasi ya kukujibu hoja yako...

Mkuu sii swala la kutokukufahamu wewe bali nataka wewe ufikirie nje ya box...Na nilichosema hapo nyuma ni kwamba sisi WATU, Wadanganyika wapiga kura ukiweza kutushawishi kwamba Lowassa ndiye the answer kwa matatizo yetu baso tutachukua maamuzi hayo hadi ktk sanduku la kura. Hivyo kama leo mtaendelea kusema Lowassa is the answer basi ndiye atakuwa hadi kaburini maana tuna asili ya kuamini mizimu na ukitupa dawa ya chaguo la Mungu kiimani basi umetumaliza kabisaaa hata kama ulikuwa unafanya utani.

Kwa hiyo unachosema wewe unatazama udhaifu ndani ya CCM na ili wagombane, basi na achaguliwe Lowassa!.. Lakini umesahau moja tu ya kwamba siku hizi ndani ya CCM hakuna msafi tena na hakuna mtu anayependwa na wengi kama Lowassa isipokuwa kundi dogo sana na wale waliomkataa shetani, hawana tena nguvu wala mamlaka. Kinachotokea leo ndani ya CCM ni Mafia gang tu yaani control ya territory zao - wizara za Uwekezaji. Na Lowassa seems to be fair to all parties zinazoshiriki ktk UTAJIRISHO..wanajua vizuri kwamba ndani ya Lowassa kila mmoja waoa atakula lakini kwa kupimiwa sio Buffet!..

Ni sera ya Lowassa aliyetaka kujenga Mabillionea 100 kufikira mwaka 2010, yeye aliamini kabisa kwamba akiweza jenga mabillionea 100 ndipo tutaweza wekeza wenyewe ktk viwanda na uzalishaji lakini hao mabillionea 100 watatokana na wizi wa fedha za misaada Worldbank na za umma. Na kila kiongozi alijipanga nyuma yake mawaziri wote wa kwanza kila mmoja alijua anashika wapi na ataaachia wapi. Ni Lowassa aliyetuuza kwa mzee wa Loliondo nambie nani hakwenda huko wala kuamini kikombe cha babu?.. Ni wewe na mimi tu ambao tulifikiria inge back fire lakini badala yake akapata umaarufu zaidi hadi serikali nzima ikashjiriki kikamilifu ktk kamba za Lowassa..

Huyu jama hatari kweli kweli mkuu wangu anajua sana jinsi ya kuteka akili za watu utadhani anatumia uchawi (nasikia huenda Nigeria) lakini sii wa kumsabikia hata kidogo.. Ndicho nachosisitiza miye kwani Wadanganyika wataamini hivyo na tayari sasa hivi kisha yakutanisha makundi yote pamoja chini yake..waliobakia ni wachache sana na tatizo lake na JK ni kwamba JK haamini kama Lowassa atakubalika kinyume cha hapo JK na Lowassa hawana ugonvi..Na nimewasema Chadema kutokana na uvumi naoupata mjini kwamba nao wanamshabikia Lowassa kwa mfikra hizo hizo.. Haya ni makosa makubwa sana kum underestimate EL maana ni hatari kuliko wanavyofikiria..

Wee nambie mbali na kundi dogo la watu wanaotegemea JK atawachagua wao kusimama 2015, huyo Lowassa ana maadui gani zaidi ndani ya CCM ya leo? Nijuavyo mimi karibu wajumbe wote wa NEC wanamshabikia yeye!. Na kama chaguo lao ni yeye, fahamu pia RA yupo nyuma yake.. Hapa tunatakiwa kupiga vita bila kuwapa pumzi hata kidogo yasije tokea yale ya JK na sifa za chaguo la Mungu tukidhani kwamba makundi yao ingekuwa rahisi kwa CCM kusambaratika - Haikuwa!
 
Sidhani kama CDM wamekosa kazi hadi waanze kutafuta mtu wa kumnadi huku tayari wagombea wanafahamika. CCM kushinda wanapigana vikumbo kuhusu Urais ni kukosa uwajibikaji kwa wananchi.

we unabisha kitu ambacho kiko wazi,hudhani but ndio hali halisi,unataka kujifanya hujui kwamba wafuasi wa chadema nao wanacheza ngoma ya kumsaka mgombea urais wa tz kwa tikiti ya ccm?hujaona kuna mchangiaji mmoja mashuhuri humu ametengeneza mpaka bango linalosomeka mwishoni mwa kila ujumbe anaochangia humu "EDWARD NGOYAI LOWASSA FOR....."Tafuta huyo mtu utampata humu na ni CHADEMA damu,huo ni mfano hai lakini wapo wengine wa aina hiyo humu,fuatilia utaelewa nasema nini..
 
Riwaya zile zile za alinacha...miaka nenda miaka rudi kila mtu anakuja na tamthilia yake ya kufikirika. Hakika wabonge kwa ngano wapo mbele kwani kila mmoja ni mjuvi wa kila fani..km unabisha hudhuria mechi yeyote ya kimataifa uwanja wa taifa ili uone kila shabiki jukwaaani anashindana na mwenzie kuhusu mchezaji yupi afanye nini! Na bado tutasikia mengi kabla ya 2015 lakini lililowazi EL hawezi kuwa our next presidaa!!
 
Naona K una hasira na HH kwa kuchelewa kwake vuta subira mambo mazuri hayataki haraka vinginevyo kuna kila dalili kuwa upande wa pili wanataka kujua nini kinachojili.Wenye akili zao walioyaona haya ya bwana HH wakayafanyia kazi na hatua wakachukua na vipengere vikarekebishwa wasiojua wanatahamaki wakiuliza wanaambiwa mbona basi lilishapita ikizu lianelekea msoma mjini zamani hivyo.Uzuri uko upande ule ule wa wanawachezesha wenzao filamu ndio inaendelea tunasubilia part two ya safari kutoka musoma mjini kwenda suguti.
 
Duh! Mkubwa nakuwa kama nafunguka macho hivi, hebu endelea kutujuza maana mambo ya Jussa sio kidogo, huwa anatoa miropoko ambayo mtu wa kawaida hawezi kuifunguka! Tafadhari endele akutujuza
 
End will justfy the meaning..., My God may you grant me more days of living....
 
Lowasa ataliingiza taifa kwenye mzigo mkubwa wa madeni

Katika hili napingana nawe mkuu,
Huyu EL hawezi kukopa hovyo, yeye anatafuta kupitia uchumi wa ndani na kuiimarisha shilingi. Tazama jinsi alivyofanya hatua za kilimo cha mvua za kutengeneza na umwagiliaji alipokwenda Thailand ili ahamishie ujuzi huo uje hapa Tanzania. Si mtalii au muombaji au muhudhuriaji wa makongamano kama tuambiavyo sasa 'mikutano isiyoisha anayohudhuria mkulu ughaibuni'
 
kila shabiki wa Lowassa na kikwete ni muhalifu maana anashabikia waliopoteza maisha ya nyerere! ni upunguani kuamini hawa wauaji watafufua uchumi. kama watapata madaraka kwa sumu watatumia sumu hiyohiyo ya bone marrows kuyalinda. haya mashabiki wote jiandaeni kuuliwa mkikengeuka!
 
Huyo rais wenu mtarajiwa (el) siku hizi amekooondaa, ana matatizo gani au anaumwa nini, uso umemkongoroka! hatuwezi weka picha yake kwenye ofisi zetu

Wafuasi wa el naomba mnijuze baba yenu anagonjeka nini
 
Nchi hii watu wana nyeti kwelikweli, nadhani jamaa kaanika vitu vya maana, lakini yote na yote heri haizidi kudra
 
Mvua ya Thailand ulikuwa utapeli mwingine. Tanzania ilishapoteza zaidi ya dola millioni kumi katika kile walichokiita utafiti wa mvua hiyo. Na tushukuru kama yule waziri mkuu wa Thailand asingepinduliwa leo ingekuwa imekula kwetu tena na fisadi Lowassa akijiongezea pesa nyingine mfukoni.
 
Hivi tapeli kaishia wapi,tulitaka aje aelezee kilichotokea kwenye kikao cha NEC dodoma hivi karibuni ambako jk anaonekana kukidhibiti chama kwa kuwaondoa wazee wote kwenye vikao vya maamuzi na kuwaundia chombo chao kwa ajili ya ushauri tu..na pia hakuna mbunge kugomea ujumbe wa nec tena,hapa huyu atatuletea tetesi gani tena...
 
Huyo rais wenu mtarajiwa (el) siku hizi amekooondaa, ana matatizo gani au anaumwa nini, uso umemkongoroka! hatuwezi weka picha yake kwenye ofisi zetu

Wafuasi wa el naomba mnijuze baba yenu anagonjeka nini

Umeona eh, jana nimemuliza jamaa mmoja aliye karibu na familia hiyo akaniambia anadalili za stroke upande mmoja ingawa haijadhibitishwa kama ni kweli au la.
 
Hatupendi udaku, kwa nini wewe usimpinge kwa hoja kwamba anachosema kiko vipi? Ye kampa JK ushauri, na kwa manufaa yake na Taifa, nina uhakika atauzingatia. Mtoa maada anaonekana sio mtu wa kada ya chini, anaufahamu vizuri huu mtandao. Na huwa anahudhuria vikao vyao! Siwezi kumbishia bila sababu, part two itatupa mwanga zaidi. Unashindwa kuelewa, hii ni sehemu ndogo tu ya kilichotolewa. Subiri amalizie kisha ndo tuanze kumwaga maoni yetu. Be patient, its just a trailer, there is so much here. Hold and wait!!!
 
Nanukuu gazeti la mwanahalisi toleo na 276 la jumatano tar.11-7 2012 lilikuwa na habari maalim seif alishinda fuatilia kipengele kisemacho kama maalim alimsamehe salimin,pia alimsamehe karume akatangazwa mshindi ihali hata wewe jusa unajua seif alishinda urais zanzibar..................kwa mantiki hiyo basi hapa jf sio kila kitu cha kubeza hapa mtu anatoa dukuduku lake lililopo moyoni asikilizwe .
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…