Kikwete, huu mtandao ni hatari! Be careful, otherwise waweza kuwa historia (Part 2)

Kikwete, huu mtandao ni hatari! Be careful, otherwise waweza kuwa historia (Part 2)

Kati ya hao nani anafikia nusu ya akili za Polepole?
Nani ameshakuwa balozi nchi zaidi ya moja?
Nani ameenda Cuba?
Nani mjamaa?
Umemuelewa aliposema amejifunza mengi akiwa Cuba ameiva hasa?
Umemuelewa alipotoa kauli za kutetea Cuba kuwa wamewekewa vikwazo kwa uonevu?
Nani Kati yao amekuwa mkufunzi mzuri wakati akiwa Katibu wa uenezi katika idara ya habari, mavunzo na itikadi wa CCM?

Sijui unatumia kipimo gani kupima akili.
Nitakuuliza pia HP amewahi kuwa waziri zaidi ya wizara moja?
bila Shaka kabla ya HP kuwa Balozi Cuba wapo mabalozi waliopita hapo Cuba.
Kwani ujamaa ni sifa, itikadi kila mtu anachagua imfaayo.
Mkuu wapo watu wamekaa Russia, Israeli ,USA nk.
HP sio wa kwanza kuitetea Cuba, lakini pia kila mtu ana mtazamo wake juu ya Cuba lazima tuheshimu mtazamo wa kila mtu.
Ukufunzi ni majukumu tu kama ambavyo hao pia walikuwa na majukumu ambayo HP hajawahi kuwa nayo pia.
JM aliwahi kuwa mwandishi wa hutuba za Rais, hilo ni jukumu lake alilopewa hatuwezi kusema alikuwa genius.

ndani ya mitaa ya Hodeidah Yemen
 
Nchi inaongozwa na wenye mtandao,

sababu Lissu alisekwa ndani na matapeli wanadunda Mjini anyday kama si kitu.

Lissu alionekana ataenda kuharibu maslahi ya wakubwa, Ubelgiji na US wapi na wapi.

RA akubali kutolewa kwenye system na Lissu CIA wampumzishe ?

RA!!! ni Virus kwenye system
 
Sijui unatumia kipimo gani kupima akili.
Nitakuuliza pia HP amewahi kuwa waziri zaidi ya wizara moja?
bila Shaka kabla ya HP kuwa Balozi Cuba wapo mabalozi waliopita hapo Cuba.
Kwani ujamaa ni sifa, itikadi kila mtu anachagua imfaayo.
Mkuu wapo watu wamekaa Russia, Israeli ,USA nk.
HP sio wa kwanza kuitetea Cuba, lakini pia kila mtu ana mtazamo wake juu ya Cuba lazima tuheshimu mtazamo wa kila mtu.
Ukufunzi ni majukumu tu kama ambavyo hao pia walikuwa na majukumu ambayo HP hajawahi kuwa nayo pia.
JM aliwahi kuwa mwandishi wa hutuba za Rais, hilo ni jukumu lake alilopewa hatuwezi kusema alikuwa genius.

ndani ya mitaa ya Hodeidah Yemen
Unamfananisha Polepole na Makonda au Nape, au yule ***** aliyepelekwa morogoro unafurahisha sana.

HP ni mtu mwingine kwanza anajua na ana facts mdadisi wa mambo, Polepole unamfananisha sura duara(Baba Gabriel)

Nilikufutalia sana, nimegundua una chuki dhidi ya Polepole, acha uchawi
 
Pasco,
Kifupi kama utaisoma Historia ya nchi za East Africa utajua vizuri nguvu ya CIA ktk mataifa. Tunajidanganya sana kufikiria kwamba demokrasia ni sisi watu huchagua chama au viongozi tunaowataka lakini ukweli ni kwamba vitu vingi vinapangwa na kama ukikataa wanakuwekea vikwazo ambavyo unabidi uvikubali.. Nadhani unakumbuka Nyerere na maswala ya Zanzibar walimshtua kidogo tu na kuasi kwa Jeshi mwenyewe alirudi na kuwageuka kila Abraham Babu..

Tazama Zaire. Liberia, Kenya, Zambia, Libya, Iraq, Syria kote wanacheza na tawala kuhakikishia wanamweka mtu wao na lengo ni nini KULINDA MASLAHI ya AMERIKA... just imagine hawa watu wanalinda maslahi yao nje ya mipaka yao lakini sisi hatuwezi linda maslahi yetu hata ndani ya mipaka yetu!...Kabila leo katangazwa rais japokuwa ameshindwa uchaguzi, kila Mkongo analijua hili lakini hawana uwezo..Yule Kagame ana bahati ya kutetewa na Ufaransa japokuwa Waamerika waliitaka sana nchi yake hivyo wamewaachia Wafaransa na jana tu kasafishwa ati Wahutu extremist ndio waliomuua Habyalimana sio Kagame na Watutsi..

Isipokuwa kwetu sisi sasa ni kutazama what in real term uwekezaji wa hawa watu katika nchi hizo unavyoharibu amani ndani. They don't care as long as wanachukua utajiri wenu haraka na kwa nguvu zote huku wakisimika nguvu za tawala hawajali mtakufa wangapi au watapoteza maisha wangapi - Capitalism Principal - utapanda kwenda juu kwa kukanyaga wengine chini ukiwafanya ngazi!

Hivyo kama Lowassa ndiye teule la CIA kupitia Kingmaker itakuwa hivyo na pengine ni wakati muafaka wa kumpata CHE na mapambano yaanze mapema sio fikra za kupitia ballotbox...maana tunajidanganya sana kufikiria kama tunaweza kumshinda CCM kupitia sanduku la kura wakati mifano yote tumeisha iona na wazi kabisa..Au tuombe Mungu tumpate Kagame, Saadam au Nyerere anayekubali kuwekwa kisha anawageuka mbele ya safari..
Duh!
 
Kwa maelezo yote haya kuhusiana na Rostam, nchi pekee duniani anazoweza kuwa salama Polepole ni North Korea na Russia akikingiwa kifua na Putin, basi. Kwingine kote sio rahisi ku survive. Na nondo anazoendelea kushusha, hili jasusi la siku nyingi la C.I.A kushindwa kumfikia alipo ni ushindi tosha kwa Polepole na sisi wafuasi wake. Mungu wa mbinguni aendelee kumlinda Polepole. Kitu kimoja kilicho wazi, hata Polepole hayupo peke yake ndo maana tunakoelekea mchezo utakuwa mtamu sana.
 
RA ndio tafsiri sahihi ya TAIKUNI. Kwenye game kitambo mpaka leo. Tunatokaje?
 
Previously: Kikwete, huu mtandao ni hatari! Be careful, otherwise waweza kuwa historia (Part 1) - JamiiForums

Karume na Jussa ni wamoja na wanafahamiana vizuri sana kuliko wewe unavyofikiri. Kundi hili linao uwezo wa kuvunja Muungano muda wowote linaoutaka na kuanzisha serikali tatu na baada ya malengo kutimia likaanzisha serikali moja!. Ni vigumu kuelewa ni yapi majukumu ya Karume ndani ya hili kundi na nani kampa majukumu hayo na wapi kiburi cha Karume kimeegemea. Ni swala la historia ndefu sana ambayo nitaiunganisha vizuri baada ya kumchambua Rostam ambaye nitachukua muda mrefu kumchambua kuliko mwingine yeyote katika kundi hili.

Nafikiri urafiki wako na Karume waweza kuwa umeingia doa kipindi cha 2007 hivi wakati umeletewa zile briefcase zilizojaa dola na kumhukumu Karume kabla hujaenda uarabuni!. Hivi zile dola zilienda wapi Mh Rais?. Zilikuwa nyingi kwelikweli. Hata hivyo Karume anaweza kweli kusahau mchezo mliotaka kumfanyia wewe na Nahodha kuhusiana na mwafaka kabla ya kipindi chake kuisha na kupelekea kumtishia Nahodha nafasi yake ya Waziri Kiongozi? Nahodha akabaki analia wakati wewe umemruka tayari baada ya kuona umezidiwa nguvu?.

Mr President, unawafahamu waliokuwa nyuma ya mchezo huu? Basi hao hao kwa miaka mingi wangekwishakumaliza lakini Edward alionekana "kukupenda'" zaidi na yeye amekuwa akiwawekea ngumu yaani kukulinda lakini kwa bahati mbaya sana, amewakubalia hivyo kufanya "game'' kuwa kali. Edward anaweza kukulinda baadaye. Lakini hutaweza kufanya biashara yeyote ile na waweza kubaki na "njaa" kali sana baada ya kustaafu. "Game'' hii ni hatari kwasababu lazima imuweke Karume kwenye nafasi za juu za uongozi wa taifa hili 2015. Mh Rais naomba umuulize Mama Maria Nyerere akwambie vitisho alivyopewa na Karume na Mkapa kuhusiana na mwanaye makongoro wakati wewe unaendesha kikao cha NEC. Hata hivyo ni vizuri ukajiuliza swali la kitoto kama hili: Je ni kwanini Karume na wenzake walikushinikiza sana umteue Tom Apson kuwa mbunge wao wakikudanganya kwamba Tom amefanya kazi nzuri ya kuiba siri za Apson na malecela na wengine? Think twice Jakaya!.

3. Rostam ni nani?

Licha ya kuwa rais wa nchi hii tena Kamanda mkuu wa vyombo vyote vya usalama, umeshindwa kumfahamu Rostam kwa undani zaidi. Nikiri kwamba, bado hujamfahamu Rostam vizuri na sidhani kama &[HASHTAG]#8216[/HASHTAG];'vijana'' wako wanamfahamu vizuri. Kabla sijamwelezea vizuri, naomba nikukumbushe kitu kimoja. Hivi ilikuwaje mwaka 1995 wakati kambi yako inaomboleza baada ya kushindwa urais, Rostam alionekana kwenye sherehe ya kumpongeza Mkapa tena akiwa na Mkapa na kwa mazungumzo marefu sana?. Je aliwasaliti nyie washirika wake?.

Nikiri tena kuwa, Rostam aweza kuwa mtu hatari, mwenye akili ya haraka sana lakini mwenye kuzichezea kwa akili ya juu sana siasa za Tanzania kuliko mtu yeyote aliye hai niliyeweza kumfahamu hapa Tanzania. Huyu akiwa pale LSE UK, alijenga urafiki mkubwa sana na binti wa mkubwa mmoja na muhimu katika Tehran (siasa za Iran). Haikufahamika kwa haraka ni nini alichokuwa akikitafuta kwa huyo binti na nani alimtuma ajenge huo urafiki ghafla kiasi hicho. Hili ninalolisema kwa sasa hata Lowassa hawezi kulifahamu, si wewe peke yako.

Ni vigumu kuamini kuwa, Serikali ya Marekani imegharamia masomo ya Rostam LSE (baada ya hii task) na hii serikali kupitia Prof mmoja anayefundisha chuo kikuu kimoja UK huku akiwa ni mfanyakazi wa CIA iliweza kufanikisha urafiki mkubwa wa Rostam na huyu binti huku yeye (Prof) akiwaachia maelekezo vijana wa CIA baadhi kum-monitor Rostam na hatimaye urafiki ukawa mkubwa sana kiasi kwamba ukaweza kumfanya Rostam akubalike na Tehran.

Kwa udhamini na wito kutoka serikali ya US, Rostam akawa anakwenda mafunzo mahsusi ya ki-usalama marekani na huko alikutana na watu wengi sana muhimu wakiwemo wamiliki wa Symbion. Kwa kukudokezea tu, pesa za Kagoda ni msamaha wa deni lililofanikishwa na ushawishi wake pale Tehran. Kwa bahati mbaya sana hata Mariam (mke wa Rostam) hakuufahamu uhusiano ule akifikiri ni mapenzi mpaka pale alipojua vinginevyo (ingawa hawezi kujua behind the scene kuna nini). Malengo ya Marekani na huu urafiki (Rostam-Tehran) bado yako palepale na nilipokutana na rafiki yangu (huyu aliweza kufanya kazi nzuri sana na Shah Riza kule Middle East) wa siku nyingi sana pale Boston, akanihakikishia kuwa lengo lilipangwa kutimia 2018 au 2022 hivi!. Ni hatari sana na mtandao wa Rostam na wenzake unaweza kukufanyia lolote watakalo kama usipokuwa makini!. Kule Saudi Arabia na sehemu nyinginezo ameweza kutumiwa sana na hawa "mabosi'' wake kwenye masuala ya biashara.

Rostam anafanya kazi kubwa na nyingi za kibiashara na kisiasa na CIA kama agent wao muhimu sana Afrika huku yeye akisaidiana na mtandao wa CIA kule South Africa na ku-control sehemu kubwa Afrika Mashariki na Kati na sehemu nyingine za afrika ambazo US itakuwa na maslahi nazo. Mambo machache aliyoweza kufanikisha ni pamoja na kumfikisha Raila hapo alipo, mikataba ya kimaslahi na Salva Kiir achilia mikono ya Rwanda na Uganda kule Congo, Madagascar, mwafaka wa Zanzibar, kujivua gamba though kosa mojawapo ni wewe kukosea implementation hivyo kum-cost na kupelekea US kumwambia ajiuzulu ubunge na "kuacha'' siasa kitu kinachomfanya afanye siasa mara kumi ya aliyokuwa akiifanya awali.

Mr President, muulize Othman akueleze ukweli kwa kuwa hili alilifahamu ingawa hajui ni kwanini lilitokea. Kumbuka vizuri wakati Bush amekuja Tanzania. Kule Arusha, viongozi wa makampuni makubwa yanayomiliki migodi mikubwa ambayo Bush, US na CIA ina maslahi nayo kutoka karibu kila kona ya dunia walikusanyika na walielezea ni kwanini biashara haiendi vizuri. Hakuna mtanzania yeyote Yule hata Deo aliyehudhuria except Rostam. Nani alimwalika na alihudhuria akitokea wapi?! Pale waliazimia mambo makubwa na ya hatari sana. Rostam anajua vizuri what happened na maazimio yale yalilenga nini.

US imeona wewe ni shida kwa kuwa nchi ni kama inakushinda vile na haioni tena mvuto wako kwa wananchi na hii ni hatari kwa maslahi yao hasa mafuta ya Zanzibar ambayo imeshayalia timing kwa maana ya kwamba imeshirki kikamilifu kucheza "game'' ya Rostam-Jussa-Karume-Shein kwa haraka sana. Nimekwambia kwamba, Muungano waweza kuvunjwa na baada ya muda ukarudi tena nakuwa serikali moja. Jiulize ni kwanini Mwamunyange anakudharau kiasi hicho?. Hicho kiburi anakitoa wapi?. Mr President, usikurupuke, cheza karata vizuri!

WAPENDWA WANA JF, MNIVUMILIE KWA MPANGILIO MBOVU. NITAENDELEA NA ROSTAM KWA UPANA ZAIDI, THEN APSON, MKAPA, EDWARD NA OTHMAN
Mkuu Salama!! Lete updates!! Uzi huu wa 2012 lakini una aksi kinachoendelea leo 2025, takribani miaka 13 iliyopita!!. Hatari sana.
 
Exaggeration tu
Huwezi exaggerate kwa mtiririko huo!! Mdau aliyeleta huu uzi 2012 inaonekana alikuwa na mkono kwenye habari nyeti (mtiririko wa thread hauna shaka hata kidogo). Kama yupo hai atupe mwendelezo. Maana ni kitambo!!
Members kama akina Saint Ivuga simuoni tena, sawa na akina Lizaboni. Watu wanapotea aisee hapa JF.
 
Kati ya hao nani anafikia nusu ya akili za Polepole?
Nani ameshakuwa balozi nchi zaidi ya moja?
Nani ameenda Cuba?
Nani mjamaa?
Umemuelewa aliposema amejifunza mengi akiwa Cuba ameiva hasa?
Umemuelewa alipotoa kauli za kutetea Cuba kuwa wamewekewa vikwazo kwa uonevu?
Nani Kati yao amekuwa mkufunzi mzuri wakati akiwa Katibu wa uenezi katika idara ya habari, mavunzo na itikadi wa CCM?
Nyinyi ndio vilaza wa hii nchi....
Huyo kichwa pumbu sloslo ni mpuuzi fulani anaetafuta maslahi yake...
Alishakuwa kwenye mfumo, je nini aliwafanya Chadema?
Huyu mbwa ndie aliemjaza upupu Jiwe adili na upinzani ili yeye nafasi yake iwe salama...
Leo hii wamemchoka ndio anajifanya mtetezi wa wa wanyonge(sic)
 
Huwezi exaggerate kwa mtiririko huo!! Mdau aliyeleta huu uzi 2012 inaonekana alikuwa na mkono kwenye habari nyeti (mtiririko wa thread hauna shaka hata kidogo). Kama yupo hai atupe mwendelezo. Maana ni kitambo!!
Members kama akina Saint Ivuga simuoni tena, sawa na akina Lizaboni. Watu wanapotea aisee hapa JF.
Hakuna kitu,2015 aliingia magu, rostam alikimbilia kenya,magu akawavuruga barrick na acacia ya akina Bush, acacia chali, angekua na nguvu hizo haya yasingetokea
 
Back
Top Bottom