Kikwete kainua uchumi wa Tanzania

Ndugu, hizi si data za uchumi si za waislam peke yao. Hizi ni data za watanzania wote. Sasa sijui hayo mambo ya mashura wa maimamu na intellectual muslims yanakujaje?

Kwa muhtasari nimeelewa kuwa somo limelewka kwako vizuri sana. Ukweli umeufahamu na kwa muujibu wa maelezao yako nahisi nawe unamuunga mkono Kikwete. Hatua nzuri! Sasa tuungane pamoja kuziendeleza na kuzikuza hizo data. Naona tupo pamoja, kwasababu hakuna aliyepinga yale maendeleo ya kiuchumi niliyoyaorodhesha katika #85.

Haluta kontinua!!! Kikwete anaweza.
 
They will come in all kinds of sizes. 2010 is around the corner and ari mpya, kasi mpya, and whatever mpya has brought nothing. So send some spinners to the rescue.
 
Jamani, hebu angalieni wenyewe, hizo data nilizoziandika zikuzichukua CCM, CUF, CHADEMA au Serikali ya Tanzania. Takwimu zote nimezichukua www.aneki.com. Ni shirika linalopata Takwimu zake toka UN na CIA. Hapa hakuna cha mkono wa Kikwete , CCM wala Serikali. Sasa mtanihukumuje katika kampeni za uchaguzi 2010?

Wengine wameniita mwanasiasa na kwamba nimekuja hapa JF kama msaliti na mchafuzi wa wapenda maendeleo. Hayo yanasemwa bila kutoa uthibitisho. Kumbukeni JF imejitangaza kama uwanja ambao watu wana dare to speak their mind and trueth openly. Wengine wamekuja na mapya kabisa, kuwa hizi takwimu za hawa jamaa tusiziamini, na hawa hawa waliposema uchaguzi wa TZ 2000 ulikuwa na kasoro tuliwakubalia sana. Sasa sisi watanzania ni watu wa aina gani?

Njia pekee na nzuri sana ya kumuumbua Zawadi, ni kutoa takwimu na vyanzo vyake zitazoonyesha kuwa uchumi unashuka. Zawadi kaingia www.aneki.com akapata GDP per capita ya $1400. Kuna mwingine kaingia www.cia.gov na akapata GDP per capita $1300. Haidhuru, tofauti kidogo lakini bado uchumi umekua toka $600(2005) mpaka $1300(2008). Sasa dhambi yangu iko wapi? Kinachotakiwa na cha msingi ni kuchacharika katika vyanzo mbali mbali na kutafuta kile kitachoonyesha kuwa GDP per capita ni $500(2008). Hapo nitatokea hapa tena na kuwaomba msamaha. Naninahakika hamtakipata chanco hicho, tiara haishikiki inatereza kama kambale iko juuuuu.

Tusipende kuzungumza kama wanasiasa wenye kuficha ukweli bila kutaja Takwimu. Utawasikia, uchumi umekua, mauzo ni makubwa, umeme ni mwingi, ujambazi umepungua. ilimradi katika maelezo yao yote hakuna hata takwimu moja. Sasa ni wakati wa kuzungumza kwa NAMBA. Kama tuliweza kusema kuwa Mkapa alishinda kwa 52% ni lazima tuweze kusema kuwa ameondoka madarakaani huku GDP per capita ni $600. Vile vile tuweze kusema kuwa Mkapa aliingia madarakani akiwa na Benzi 2 na nyumba 2, na anatoka madarakani akiwa na Magari........, makampuni........., na pesa taslimu TZ SH........., na pesa taslimu nje $................

Tukiweza haya tutazungumza lugha moja. Kikwete anaweza!!!!!!!
 

Bado hujaorodhesha chochote ... cha kupingwa.
 

Hakuna cha "Haluta Kontinua" wala babake "Haluwa Kontinua" (kama wenzetu Waislamu msemavyo).

Hata kama ni kweli pato la Taifa limeongezeka baada ya JK kuchukua madaraka, ukweli ni kwamba itakuwani sawa na kupiga hatua moja mbele na hatua mbili nyuma kwani huduma za jamii zimelemewa maradufu kama unavyoona kwenye picha ya watoto ombaomba waliokithiri kila sehemu ya jiji licha ya kwamba Kikwete kuunda Wizara maalum ya MAENDELEO YA JAMII JINSIA NA WATOTO alipoingia madarakani. Na hapo bado hatujaenda mikoani na vijijini ambapo wengi wa watoto hawa na wazazi wao wanakotokea.

La msingi ni kwamba takwimu kavu na tupu za "ongezeko" la pato la Taifa unazosoma kwenye makaratasi na mtandaoni si za kuaminika na hazina maana yoyote wakati hali halisi ndiyo kama unavyoona. Kalagha Baho!
 
Usiseme hata ni kama uchumi umekuwa, tafadhali lete Takwimu. Hivi ni vigumu kuongea lugha ya Takwimu? .Mbona nimeelezea kirefu sana jinsi unavyoweza kunishutumu juu ya habari yangu. Nami nikaandika kuwa nitawaomba radhi wana JF kwa ujumla ikiwa itaonekana kuwa Takwimu hizo ni za kubabaisha.

Sasa kua mwanangu, na tuzungumze lugha ya kisomi hapa JF. wAOMBE HATA WASOMI wa mlimani WAKUSAIDIE. Ukifanya hivyo nitafurahi sana. Sina haja ya kurudia Takwimu, tumia hizo hizo nilizokwishaandika.

Takwimu tafadhaliiiii. Kikwete anaweza!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…